Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
![]() |
Mtumishi Gasper Madumla |

Bwana Yesu Asifiwe…
Haleluya….
Kwanza kabisa ieleweke wazi kuwa yeye asiyeokoka yampasa afe mara mbili,yaani lazima apitie mauti hizi mbili :
01.Mauti ya mwili.
02.Mauti ya kiroho.
* Tunasoma habari za Nikodemo.
Huyu alikuwa ni mwalimu wa Waisraeli lakini alikuwa hajui habari za
kuzaliwa mara ya pili,Hii inamaanisha kuwa ,yeye Nikodemo alizaliwa kwa
mwili tu,hivyo ilimpasa afe mara mbili.
Neno la Mungu linamuelezea kuwa Nikodemo alikuwa ni Mfarisayo na tena alikuwa mkuu wa Wayahudi.
Kwa hiyo sifa yake ya kwanza alikuwa ni MFARISAYO na pili MKUU WA WAYAHUDI.
Labda tuangalie sifa za MFARISAYO japo kwa ufupi.
01. Hunena wala hawatendi kile wakinenacho
02. Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.
03. Matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu
04.hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,
05.Hupenda kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.
*Je wewe unatabia kama hizi,ikiwa ni ndio basi U Mfarisayo !!.
Tunasoma Mathayo 23: 1-7 :
'' Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema,
Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;
basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano
wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.
Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. ''
Sikia:
Nikodemo alimfuata Yesu usiku kwa maana alijua akimfuata Yesu mchana
,labda ataonekana na wanafunzi wake maana yeye Nikodemo alikuwa ni
mwalimu,hivyo walikuwepo wanafunzi wake.Wanafunzi wake wasije kujua kuwa
mwalimu wao hayajui mambo ya kuzaliwa mara ya pili.
Sisi
Mwanadamu,tumeivaa miili ya kuharibika miili hii ni miili ya damu na
nyama *Hivyo mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, amewekewa kufa mara moja
na baada ya kufa ni hukumu.
Tunasoma :
Waebrania 9 : 27 : 7 '' Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu ''
*Mwanadamu aliyezaliwa kwa mwili wa damu na nyama ,yaani amezaliwa mara moja basi zipo mauti mbili zinamsubili,ambazo ni :
01Kifo cha mwili,kama ilivyoandikwa katika Waebrania 9 : 27
02.Kifo cha kiroho cha kutupwa katika ziwa la moto. ( Ufunuo 20 :14)
Ikumbukwe kwamba :
Mtu anapookoka tu jina lake linaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo.
Hawa sasa walioandikwa katika kitabu cha mwanakondoo hawahitajiki kufa mara ya pili.
Tunasoma Ufunuo 21 : 27
'' Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala
yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu
cha uzima cha Mwana-Kondoo. ''
Kifo cha mara ya pili ni kutupwa katika ziwa la moto.
Ufunuo 20 : 14-15
'' Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. ''
ALIYEZALIWA MARA MBILI ,ALIYEOKOKA, HAITAJIKI KIFO CHA MARA YA PILI:
Yule aliyeokoka kisha akadumu katika wokovu na jina lake likaandikwa
katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo,Huyo atakufa mara moja tu ,yaani
ataubadilisha mwili huu wa damu na nyama.
Hapa ieleweke kuwa
hata huyu aliyeokoka kama Paranda ikilia ile siku ya unyakuo,pale
atakapo nyakuliwa ndio itakuwa ni mauti yake ya kwanza, maana hataweza
kwenda mbinguni kwa mwili huu wa damu na myama lakini hatakufa tena bali
U na uzima wa milele.
Na kifo chake ni kwa ajili ya KUBADILISHA MWILI HUU WA NYAMA na kupata mwili mwingine usioharibika.
Tunasoma 2 Wakorintho 5 : 1
“ Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii
ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa
mikono, iliyo ya milele mbinguni.”
Sasa tukirudi kwa habari za Nikodemo,Tunaona Bwana Yesu akibainisha haya mambo wazi wazi kabisa.
Tunasoma Yoh 3 : 3
'' Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. ''
* Hapo tunaona kuwa IPO KUZALIWA MARA YA KWANZA na IPO KUZALIWA MARA YA PILI.
* Yeye aliyezaliwa mara ya pili ijapokuwa atakufa,atakuwa anaishi
Yohana 11 : 25
“Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;”
Sikia :
Kinachofanyika ni kuwa Yule aliyeokoka atakuwa na uzima wa milele;
wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Mauti apitayo ndio hiyo ya kuubadilisha mwili huu wa nyama na kuuvaa
mwili usioharibika,yaani kufa mara moja tu na kuishi milele.
Tunasoma Yohana 5 : 24.
“ Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye
aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita
kutoka mautini kuingia uzimani. ”
* Maisha halisi yamo ndani ya Yesu Kristo.
Nje ya Yesu Kristo ,hakuna maisha maana sisi wenyewe hatuwezi kufanya jambo lolote lile kwa akili zetu ( Yoh 15 : 5)
Lakini tunayaweza yote katika Yeye atutiaye nguvu.Ndani yake tunaidhi,twaenda na kuwa na UZIMA wa milele.
* Sio mpango wa Mungu kwamba mwanadamu afe mara mbili,Bali atutaka sote tutubu na kurejea kwake,tuwe na uzima wa milele.
Hii ni fursa ya pekee ambayo ametupa
Tazama hata maandiko matakatifu yatuambiavyo :
Katika Yoh 3 : 16
“ Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. ''
Wito wangu kwako,ni UKABIDHI MAISHA YAKO KWA BWANA YESU ILI AWE MWOKOZI
KWAKO,YAANI UOKOKE,NAWE USIJE UKAINGIA KATIKA MAUTI YA MARA YA PILI
UBARIKIWE.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments