MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU,BALI JAWABU LA ULIMI HUTOKA KWA BWANA. (Mithali 16 :1 ) * Sehemu ya kwanza *

Mtumishi Gasper Madumla

Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Andiko hilo katika Biblia ya New King James version,NKJV Limeandikwa hivi :
'' The preparations of the heart belong to man, But the answer of the tongue is from the LORD ''

Sote twafahamu kwamba, kiumbe hai chochote kina kiungo ndani ya mwili wake ambacho kiungo hicho husukuma damu katika mwili,na kiungo hicho ni MOYO.
Moyo ni kiungo muhimu sana ,maana ikiwa kama moyo utasimama kushindwa kufanya kazi yake,Basi ni dhahili kabisa kuwa uhai wa kiumbe hicho upotea.

Lakini MOYO unaozungumziwa katika andiko hilo sio moyo huo wa nyama.Bali MOYO unaozungumziwa hapo huwakilisha ROHO.

Ikumbukwe kuwa :
Biblia mara nyingi inapozungumzia kwa habari ya MOYO huwa inamaanisha ROHO Mfano :
Soma andiko hili Warumi 10 :10 Biblia inasema :
“Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. ”

Moyo wa mwanadamu kama kiungo hakiwezi kuamini.Maana moyo kama kiungo,ni sawa na kiungo kingine katika mwili ambacho hakiwezi kuamini,
Hatuwezi kumuamini Bwana Mungu kwa kwa kutumia kiungo chochote kile katika mwili wetu.

Bali moyo unaozungumziwa hapo kwamba “ Kwa maana kwa moyo mtu huamini…”. Sio moyo kama moyo tuujuao Bali ni roho ndiyo inayozungumziwa.Katika andiko hilo tunajifunza kuwa Imani ni tendo la rohoni,maana kwa roho mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

Okey :
Turudi katika andiko letu lisemalo '' Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.''

Sasa hapo tuanjifunza kuwa Maandalizi ya roho ya mtu,ni ya mtu mwenyewe bali majibu ni ya Bwana.
Mtu ambaye anamuendea Bwana Mungu,hupaswa kuandaa moyo wake,Moyo unaoandaliwa ni roho.

 Katika kipindi cha maombi,mtu hupokea maombi yake pale aombapo,na hii sio kana kwamba mtu huyo anajua kuomba impasavyo ,lasha ! Bali ni kwa sababu ya MAANDALIZI ya roho yake.!

Tukiijua siri hii iliyofichika hapa,Basi tutakuwa kila tuombapo twapokea kwa kadri ya Roho mtakatifu apendavyo Yeye.
Mwanadamu amepewa jukumu la kuuanda amoyo wake ili apokee kile anachoomba.

ITAENDELEA...
UBARIKIWE.

Comments