MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU,BALI JAWABU LA ULIMI HUTOKA KWA BWANA. (Mithali 16 :1 ) * Sehemu ya pili *

Mtumishi Gasper Madumla
Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Karibu katika sehemu ya pili ya fundisho hili la msingi,Dhumuni kuu la fundisho hili ni kukupa ufahamu kuwa wewe mpendwa yakupasa uandae moyo wako pindi uendapo kwa Bwana Mungu.Sasa ni jinsi gani waweza kuandaa moyo wako ? Karibu tujifunze pamoja :

Nilikuambia kuwa Katika kipindi cha maombi,mtu hupokea majibu yake pale aombapo,Ikiimaanisha kuwa ukikaa kimya,usitegemee kupokea kitu chochote ,kwa sababu hujaomba,
Bali ukiomba utapata,na hii sio kana kwamba mtu huyo aombaye na kujibiwa kwamba anajua kuomba sanaa,au anajua kuomba impasavyo ,Bali ni kwa msaada wa Roho mtakatifu,kwanza akiwa AMEFANYA MAANDALIZI YA MOYO WAKE.

Katika suala la '' Maandalizi ya Moyo '' Katika eneo hilo ,ndipo lipo tatizo letu tulio wengi,na laiti kama tutaijua siri iliyofichika hapa,Basi tutakuwa kila tuombapo twapokea kwa kadri ya Roho mtakatifu apendavyo Yeye.

Mwanadamu amepewa jukumu la kuandaa moyo wake ili apokee kile anachoomba.Moyo usioandaliwa hauwezi kupokea yale ambayo mtu aombayo,Ndio maana andiko linatuambia '' Maaandalizi ya moyo ni ya mwanadamu '' Hii ikimaanisha kuwa Mungu hausiki kwa maandalizi ya moyo wako,Yeye anahusika kukupa jawapu la ulimi wako kwa kadri apendavyo Yeye.

Hakuna awezaye kumpokea Roho mtakatifu ikiwa hajafungua moyo wake kumpokea,Kitendo cha kufungua moyo ni suala la maandalizi,na maandalizi haya ni jukumu la mtu binafsi.
Ndio maana hata Bwana Yesu asema “ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.” Ufunuo 3 :20.

Jambo la kwanza ni KUSIKIA SAUTI YA BWANA MUNGU maana kusikia kwaleta IMANI (Warumi 10 :17),
Pili ,ili umpokee Bwana Yesu,ni sharti UFUNGUE MOYO WAKO.
Naye Mungu wetu tazama alivyokuwa ni MUNGU wa Demokrasia maana hakulazimishi ufungue mlango wako ,bali ukipenda waweza kufungua,naye ataingia.

Namna ya kufungua mlango ni jambo la maandalizi ya moyo, baada ya kusikia sauti ya BWANA MUNGU,labda tuangalie maandalizi ya moyo huwaje ? kulingana na andiko letu la Mithali 16 :1.

MAANDALIZI YA MOYO/ The preparations of the heart.

Kumbuka,nilikuambia Moyo unaozungumziwa katika Biblia ni ROHO,na sio moyo kama kiungo katika mwili wa binadamu,maana moyo wa mwanadamu ulio kama
kiungo,hauwezi kuuandaa KUPOKEA MAMBO YA KI-UUNGU.
Wenyewe unakazi yake maalumu ya Kusukuma damu tu katika mwili ,Hivyo hausiki kabisa kwa kufanya maandalizi ya kiimani.

Najua hapa pia kuna tatizo sana ,maana watu hufikiri moyo unaotajwa katika andiko hili ni moyo wa damu na nyama wenye kusukuma damu mwilini,la hasha! Moyo ni ROHO kibiblia

Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Hivyo basi nisemapo '' Maandalizi ya moyo '' ni sawa na kusema '' Maandalizi ya ROHO ''

Maandalizi ya awali ya MOYO/ROHO ni kuilisha chakula.
Maana ROHO ndio itiayo uzima nafsi na mwili.
ROHO ikiwa haina chakula itakuwa dhaifu kiasi kwamba yavamiwa na chochote na pia baadaye hufa.

Sikia :
Kinachomuongoza mtu kutenda jambo lolote atendalo ni NAFSI au ROHO kutegemea ni nani kati ya nafsi au roho aliyepo juu ya mwenzake.
Yaani ikiwa NAFSI atakuwa juu ya roho,basi ni dhahili mtu ataongozwa kwa NAFSI,na mtu huyo ndio anayeitwa mtu wa MWILINI,ambaye hutawaliwa na matendo ya mwilini.

Tunasoma Wagalatia 5 : 19-21 :
“ BASI MATENDO YA MWILI NI DHAHIRI,NDIYO HAYA , uasherati, uchafu, ufisadi,
ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.”

Lakini ikiwa ROHO iatakuwa juu ya nafsi ndani ya mtu,Basi mtu huyo ataongozwa na ROHO naye ndie mtu wa rohoni,mtu wa rohoni atatawaliwa na TUNDA LA ROHO Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Wagalatia 5 : 22-23

Mpaka mtu aongozwe kwa roho,ipo kazi ya ziada,sio rahisi,wala si mchezo mchezo tu,bali ni kuacha yote kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
Mungu anapokuwa namba moja katika maisha yako,unakuwa sio mtu wa kawaida.
Roho ili iwe kiongozi katika mwili ni lazima iwe na nguvu,Nguvu hupatikana katika chakula,Chakula cha roho ni NENO LA MUNGU.

ITAENDELEA...
UBARIKIWE.

Comments