MAISHA YA NDOA





Mwanzo 2:24 "Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja." Ukiangalia (Zaburi 45:10-11 anasema, "Sikia, binti, utazame (maana yake anazungumza na msichana), utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana

wako, nawe umsujudie." maneno haya "Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako" yana maana kuwa kwenu ndo unatoka maswala ya kurudi kwenu au tatizo kukimbilia kwenu hairuhusiwi ni sawa watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, ambacho ni kitu hakiwezekani. Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mume wako.

Uamuzi wa kuoa au kuolewa unamtaka mtu aingie katika ndoa asilimia mia moja. Ikiwa hautakuwa tayari kuingia kwenye ndoa kwa asilimia mia moja, tafadhali usiamue kuoa au kuolewa. Utampotezea tu mwenzako muda maana hakuna ndoa isio na matatizo. Lakini pia hakuna tatizo ambalo Mungu hawezi kulitatua. Lakini, je, uko tayari kushirikiana na Mungu katika ndoa kwa kiwango cha asilimia ngapi?.

Comments