Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Labels

Wednesday, April 03, 2013

MAMBO SABA(7) MUHIMU KUHUSU BIBLIA

NIKIWA KANISANI KAWE PENTECOSTAL CHURCH {KPC} KWA MCHUNGAJI ELLY BOTO WAKATI WA IBADA YA SUNDAY SCHOOL.Ndugu katika BWANA YESU shalom, MUNGU ni mwema na ametupa uzima ndio maana tuko hai hata leo sifa, heshima, adhama na utukufu wote tunampa yeye. Nakukaribisha katika mambo haya muhimu kuhusu BIBLIA TAKATIFU au neo hai la MUNGU aliye hai.na jambo muhimu zaidi mstari wa katikati ya BIBLIA ambao una maana kubwa sana kwa wanadamu wote
1.Sura/mlango/chapter fupi kabisa katika BIBLIA ni Zaburi 117 inayosema ''Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni BWANA, Enyi watu wote, mhimidini. Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu, Na uaminifu wa BWANA ni wa milele''.

2.Sura ndefu zaidi katika BIBLIA ni Zaburi 119 ambayo sura hii au mlango huu una mistari 176.

3.Kuna sura au milango 594 kabla ya Zaburi 118 na kuna sura au milango 594 baada ya Zaburi 118. na ukijumlisha hizo sura 594 + 594 unapata sura 1188 na ukiongeza na hiyo sura ya katikati ya BIBLIA unapata sura au milango 1189. Hivyo BIBLIA ina sura au milango 1189.

3. Sura ya katikati ya BIBLIA ni Zaburi 118.


4.Mstari wa katikati ya BIBLIA ni Zaburi 118:8 unasema ''Ni heri kumkimbilia BWANA Kuliko kuwatumainia wanadamu. ''

5.BIBLIA ina mistari au aya 31,102 kutoka MWANZO hadi UFUNUO

6. Mstari wa kwanza kwenye BIBLIA unasema ''Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi'' mwanzo1:1 na mstari wa mwisho kwenye BIBLIA unasema '''Neema ya BWANA YESU na iwe pamoja nanyi nyote.Amina.'' ufunuo 22:21

7.BIBLIA ina vitabu 66 ambavyo ni 39 Agano la kale na 27 Agano jipya.na Sura ya katikati ya BIBLIA ni Zaburi 118.


MUNGU awabariki sana na pia kama hujampa BWANA YESU maisha yako wakati wa kufanya hivyo ni sasa tafuta kanisa wanapofundisha neno la kweli la MUNGU na waeleze watumishi wa MUNGU hao na watakusaidia.

{The next time someone says they would like to find GOD's perfect will for their lives and they want to be in the centre of His will, Just send them to the centre of HIS WORD.}


0 comments: