NA BARAKA HIZI ZOTE ZITAKUJIRIA NA KUKUPATA USIKIAPO SAUTI YA BWANA,MUNGU WAKO.(Kumb. 28 : 2 ) * Sehemu ya pili *







Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe…

Karibu mpendwa katika sehemu ya pili ya somo hili zuri. Dhumuni la somo hili ni kukujenga kiimani kwa kufahamu kuwa BARAKA HAZIOMBWI,maana maandiko matakatifu yako wazi kabisa yakituambia “ na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. ” Kumb.28 : 2

Labda tujiulize kuwa Baraka ni nini ?
• Baraka ni kutii sauti ya BWANA MUNGU na kuyafanya maagizo yote akuagizayo.
Tunasoma
Kumbukumbu la torati 30 : 8
“ Nawe utarudi, uitii sauti ya Bwana, na kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo. ” 8 (And you will again give ear to the voice of the Lord, and do all his orders which I have given you today. )

Kwa lugha nyingine ni kwamba, ili uwe na BARAKA maishani mwako ,Basi yakupasa kwanza UTII sauti ya Bwana Mungu wako kwa bidii.
Kama ukiendelea kusoma katika andiko hilo ( la kumb. 30 : 8) utaona baada ya kutii sauti ya Bwana Mungu ,ndipo BARAKA zinakujilia pasipo kuomba.

Tunasoma Kumb. 30 :9
“ Na Bwana, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng'ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa Bwana atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako; ”

Okey,
Baraka kwa lugha ya kiingereza ni Blessing na neno BLESSING asili yake ni neno la kiyahudi ( Hebrew word ) ambalo ni “BARAK ” lenye maana ya kuachilia nguvu iliyokuwepo ndani kwa Yule anayebariki ( To give permission for ability to be released ) Ndio maana ukisoma katika kitabu cha Mwanzo 1: 28. Biblia takatifu inasema :

“MUNGU AKAWABARIKIA, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. ”

( AND GOD BLESSED THEM, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the earth, and subdue it: and have dominion over the fish of the sea, and over the fowl of the air, and over every living thing that moveth upon the earth. {moveth: Heb. creepeth}From KJV ) Gen 1 : 28

BWANA MUNGU anapoachilia Baraka kwa watu wake,maana yake anaachilia utawala/mamlaka ambapo mamlaka katika eneo hili huwakilisha nguvu itokayo ndani yake ya kumiliki/Kutawala.
Hivyo ni lazima maelezo ya Baraka yafuate,mahali ambapo Bwana Mungu hubariki Mfano :
Tumeona hapo katika kitabu cha Mwanzo 1 : 28. MUNGU AKAWABARIKIA, Mungu akawaambia,…
Baada ya kuwabarikia Adam na Hawa tunaona akitoa maelezo juu ya BARAKA hiyo.

Hivyo ndani ya Baraka imo nguvu ya pekee inayotoka kwa Yule anayebariki. Ukimbariki mtu inamaana kuwa ,kuna nguvu itokayo kwako inayoambatana na kile unachokibariki.

Sikia ;
BARAKA hupatikana katika kuliishi neno la Mungu.
Hivyo basi unapowaona watu wa mataifa wakimiliki vitu vya thamani kubwa haimaanishi kuwa wamebarikiwa la hasha!

Maana upatiakanaji wa vitu hivyo havikutokana na neno la Mungu,hiyo sio BARAKA bali ni Neema na Rehema za Mungu alizoachilia kwao kwamba akiwasubili siku moja watubu kisha ndipo wapokee BARAKA ya kweli iliyomo ndani ya Yesu Kristo.Tazama maandiko yatuambiavyo hapa :

“ Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;” Waefeso 1 : 3

Baraka hutoka kwa BWANA MUNGU nazo huanzia rohoni katika ulimwengu wa roho, ndani ya Kristo. Hii inamaanisha kuwa mtu wa mataifa hana Baraka,maana Baraka zimo ndani ya Yesu Kristo na ndio maana ni muhimu sana kumpokea Bwana Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako ili urithi Baraka za za kweli.

Labda tuangalie wale waliobarikiwa :
01.IBRAHIMU

Tukimtizama Ibrahimu anatupa mfano mzuri wa mtu aliyebarikiwa.Kamwe hutaona Ibrahimu akiomba BARAKA kwa Bwana Mungu bali yeye aliishi maisha ya Imani tu ,akilishika neno la Mungu na yote ambayo Bwana Mungu amuagizayo na Baraka za Mungu zikamfuata pale alipo.

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments