Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
Je!
Wakristo wana haki ya kuchinja kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu? .
Jibu ni ndio, kwa mujibu wa Qur-an 5:5 nainukuu. Leo mmehalalishiwa kila
vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa kitabu kabla yenu ni halali
kwenu na chakula chenu ni halali kwao. Mwisho wa kunukuu. Mahali popote
katika Qur-an inapotaja waliopewa kitabu, wanakusudiwa ni Wayahudi na
Manasara yaani Wakristo, hili halina ubishi kwa msomi yeyote wa Qur-an.
Pengine kuna madai ya uongo kusema waolipewa kitabu sio Wakristo wa
sasa ni wale wa zamani, hii hoja sio ya kweli kwa wapenda haki na utii
wa maneno ya Mungu. Katika Qur-an takatifu ya Kiswahili, iliyo tafsiriwa
na Kadhi na shekhe Abdulla Saleh Farisy chapa na 7. 2004. Ufafanuzi
katika hiyo sura ya 5:5 surat maidah. Nanukuu. Chakula cha kuchinja
hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na (a) Mwislamu au na (b)
Myahudi au (c) Mnasara (Mkrito) kwa sharti ile ya kuchinja sio
kuwanyonga. Mwisho wa kunukuu.
Katika kitabu cha waislamu kiitwacho
“Halali na haramu katika uislamu” kilichoandikwa na Ustadh Yusuf
al-Qaradhawi. Ukurasa wa 67. Nanukuu. Na ikadhaniwa kuwa baadhi ya
Waislamu wata- wachukulia Wayahudi na Manasara (Wakristo) kama wenye
kuabudu sanamu na mizimu, Mwenyezi Mungu alitoa ruhusa ya kula chakula
chao na kuoa wanawake wao ili kuwatofautisha na washirikina, akasema
Mola mtukufu. Mwisho wa kunukuu.


Pengine kuna madai ya uongo kusema waolipewa kitabu sio Wakristo wa sasa ni wale wa zamani, hii hoja sio ya kweli kwa wapenda haki na utii wa maneno ya Mungu. Katika Qur-an takatifu ya Kiswahili, iliyo tafsiriwa na Kadhi na shekhe Abdulla Saleh Farisy chapa na 7. 2004. Ufafanuzi katika hiyo sura ya 5:5 surat maidah. Nanukuu. Chakula cha kuchinja hakiwi halali kwa Waislamu ila kichinjwe na (a) Mwislamu au na (b) Myahudi au (c) Mnasara (Mkrito) kwa sharti ile ya kuchinja sio kuwanyonga. Mwisho wa kunukuu.
Katika kitabu cha waislamu kiitwacho “Halali na haramu katika uislamu” kilichoandikwa na Ustadh Yusuf al-Qaradhawi. Ukurasa wa 67. Nanukuu. Na ikadhaniwa kuwa baadhi ya Waislamu wata- wachukulia Wayahudi na Manasara (Wakristo) kama wenye kuabudu sanamu na mizimu, Mwenyezi Mungu alitoa ruhusa ya kula chakula chao na kuoa wanawake wao ili kuwatofautisha na washirikina, akasema Mola mtukufu. Mwisho wa kunukuu.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments