Katika matukio yaliyotokea pale kawe pentecostal 
church(KPC) karibu na lugalo jeshini jumapili iliyopita ilikua ni pamoja
 na muujiza wa MUNGU kwa mtumishi wa MUNGU Paulo Kusayo ambaye ni mzee 
wa kanisa kiongozi  na mkewe Ester Kusayo baada ya MUNGU kuwabariki 
mtoto wa kike baada ya miaka mingi kupita maana ndoa yao yenye mika 12 
walijaaliwa kupata mtoto 1 tu na kwa mika 10 hawakupata mtoto lakini 
muujiza wa MUNGU ulipotokea wamefanikiwa kupata mtoto tena. ni jambo la 
kumshukuru MUNGU sana na hawakuficha furaha yao maana walisema mbele ya 
kanisa kuwa huo ni muujiza mkuu sana kwao kwani hawakudhani kama 
wangefanikiwa kupata mtoto tena maana kwa mika 10 walitaka mtoto lakini 
haikutokea na kwa kumwamini MUNGU walijua tu kuwa wakati wa BWANA 
ukifika watafanikiwa na MUNGU alikua amekwisha sema tayari na mtumishi 
Paulo lakini imechukua miaka mingi kutokea.  | 
Comments