AGIZO KUU LA BWANA YESU KWA MITUME WAKE. * sehemu ya pili *

Mtumishi Gasper Madumla


Tunasoma Mathayo 28 : 19-20“ Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. ”

Haleluya…
Bwana Yesu asifiwe sana…

Kushindwa kuhubiri injili ni kwenda kinyume na agizo la Bwana Yesu.Bwana Yesu anakutaka akuone ukifanya kazi yake kwanza kabla ya kufanya kazi yako,maana hata hiyo kazi yako uifanyayo sasa huiwezi kuifanya mwenyewe pasipo Yeye Mungu.

Tena kazi zote tuzifanyazo duniani ni ubatili tu mbele ya uso wa Bwana Mungu,ikiwa tutamuacha Yeye aliyetuumba na kugeuza sura zetu,Isipokuwa ipo kazi moja tu isiyokuwa batili mbele za Bwana nayo ni kazi ya kuwafungua watu walioteswa na kuonewa na ibilisi.
Kazi hiyo ya kuwaleta watu kwa Mungu ndio kazi ya pekee iliyo njema.Katika Biblia tunayoisoma kila siku imebainisha wazi ya kuwa ipo kazi moja tu iliyokuwa njema usoni pa Bwana nayo ni hiyo,Kuhubiri injili na Kuwafungua wale wote waloteswa na ibilisi,

Tunasoma Matendo 10 : 38
“ habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko,
AKITENDA KAZI NJEMA NA KUPONYA WOTE walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.”
( how God anointed Jesus of Nazareth with the Holy Spirit and with power, WHO WENT ABOUT DOING GOOD AND HEALING ALL who were oppressed by the devil, for God was with Him.)

Tazama andiko hilo vizuri,na utagundua kwamba ipo kazi iliyo njema machoni pa Bwana,ambayo kazi hiyo yatokana na agizo la Bwana Yesu (Mathayo 28 :19-20 ).

Kilichokuwapo hapo ni kuhubiri injili na kuwafungua wale wote walioonewa na ibilisi,kwa msaada wa roho mtakatifu,na nguvu zitokazo kwa Mungu Baba mwenyewe.
Mtume Paulo aliijua Siri hii ya ajabu na akasema
“ Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! ” 1 Wakorintho 9 :16

Anasema ole ni kwa wale wasiohubiri injili,maana hata yeye Paulo amewekewa sharti.
Neno “ Sharti”sio hiyali bali ni lazima,kwamba anawajibu wa kuhubiri injili ya Kristo,Kadhalika na hata kwako pia wewe mkristo,yakupasa kuanza kumtangaza Bwana Yesu katika habari njema ziletazo wokovu.Zipo njia tofauti tofauti za kuhubiri injili ya Bwana

Mfano,
• Kutoa mali zako kwa ajili ya kazi ya Bwana iende mbele.Yoh.12 :3
“ Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.” Pia soma Mathayo 26: 7,Matendo 10 :1-4 N.k

• Kuhubiri kupitia kinywa chako kama wafanyavyo watumishi wa Bwana Mungu. 1 Wakorintho 9 :16

• Kwa njia ya ushuhuda
• Kuinjilisha kwa uuimbaji.N.K

Ukweli ni kwamba hakuna hawezaye kuifanya kazi hii ya kulitangaza neno la Bwana kwa akili zake mwenyewe ,Au kwa uwezo wake binafsi,isipokuwa ni rahisi kuifanya kazi hii iwapo Roho mtakatifu mwenyewe atakapokuwa kazini.

Sasa tuje katika uhalisia wa maisha yetu ya leo,utagundua kuwa kazi hii haifanyiki ipasavyo maana wakristo wa leo,
wengi wao hushindwa kutambua kazi hii kwa kudhani ya kuwa ni wachungaji ndio wanaopaswa kuifanya peke yao.

Kazi ya kuhubiri injili ni kwa kila aaminiye katika Kristo,Ikiwa wewe mpendwa usomaye ujumbe huu waamini katika Kristo,Basi agizo hili linakuhusu sana la kufanya kazi ya kuwaleta watu kwa Yesu.

Mimi nasema inawezekana yote katika Yeye Bwana atutiaye nguvu.Kumbuka kwamba,ikiwa utaongozwa na Roho mtakatifu katika maisha yako ya wokovu ,basi yakupasa kukumbuka kwamba :

• Usitafute watu kwa ajili ya Mungu bali tafuta Mungu kwa ajili ya watu.

Maana yeyote atafutaye watu kwa ajili ya Mungu hufanya kwa matakwa yake binafsi,Bali Yule atafutaye Mungu kwanza kwa ajili ya watu,
huyu huongozwa na Mungu,maaana hata maandiko matakatifu yako wazi kabisa yakisema
“ Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. ”Yoh.4 :23

Wale wanao abudu katika roho na kweli Mungu anawatafuta wao,na sio wao humtafuta Bwana Mungu,sasa ikiwa wewe utashughulika na kuutafuta uso wa Bwana Mungu,Bwana Mungu naye atakutafuta wewe pamoja na watu wake wanaoabudu katika roho na kweli.

Labda nikupe mfano :
Tazama watu wawili katika jamii uliyopo wewe,Mtu wa kwanza wa kumtazama ni Yule asiyesoma kabisa na wala hana mpango wakujiendeleza kielimu.Na mtu wa pili ni Yule aliyesoma katika kiwango cha elimu ya juu sana.Sasa chukulia kwamba wote hawa wawili wanatafuta kazi ya kufanya.

Ni ukweli usiopingika kwamba huyu wa kwanza asiyesoma kabisa,itakuwa ngumu kwake kupata kazi hivyo ni lazima jasho limtoke kwa kutafuta kazi hiyo,Bali huyu wa pili kwake si yeye atafutaye kazi bali kazi ndio inamtafuta yeye.Yaani kazi ipo tu kwa ajili yake,maana aweza kuchagua afanye kazi gani,

Ni tofauti na Yule wa kwanza,yeye hana chaguo la kazi bali inambidi afanye kazi yoyote itakayo kuja kwake,
Halikadhalika kwa wale ambao wanamuabudu Bwana katika roho na kweli,watu kama hawa,
Mungu sasa ndio huwatafuta,tofauti na wale wasiomuabudu Mungu katika roho na kweli,hawa hutumia nguvu nyingi kumtafuta Bwana Mungu na wasimpate.

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments