FANYA HAYA UNAPOTEMBELEA MGONJWA HOSPITALINI





Ni utamaduni wa kiafrika kujuliana hali tunapokuwa tunaumwa, na mara nyingine ni kutokana na ukarimu wetu, uliojaa huruma, utu wema na upendo. Kwa kawaida, mtu anapoumwa, kila mmoja hupenda kwenda kumjulia hali, hata hivyo, yafaa unapoenda kumwona mgonjwa, ufanye yafuatayo:-

1. ULIZA MASWALI
Andaa maswali ya kuuliza kabla hujaanza safari yako kwenda hospitalini, na muhimu zaidi ni kuuliza maswali yatakayokufahamisha ugonjwa wake na matibabu yake ili mazungumzo yaenende kiroho zaidi.

2. SOMA MAANDIKO
Iwapo hujui cha kufanya wala kuongea, basi ni vizuri ukatoa Biblia yako na kusoma maandiko, hakikisha una Biblia kabla ya kwenda hospitalini.

3. OMBA/ ENEZA INJILI
Utakapofanya maombi ya injili, kuna fursa ya neno kusikika kwenye chumba cha wagonjwa, kwa waliokoka, na ambao bado, nafasi ambayo inaweza kuokoa watu zaidi.

4. HAKIKISHA UWEZO NA AHADI ZA MUNGU
Waeleze wagonjwa ukuu wa Mungu na uwafahamishe kuhusiana na ahadi ambazo Mungu ametuahidia.

5. AMINIA MIPANGO YA MUNGU
Unapokuwa na imani kuhusu mipango ya Mungu, basi atafnaya kazi kupitia imani yako na kukupa maneno ya kuzungumza kwa wakati muafaka.

6. ACHA UJUMBE
Iwapo hutomkuta uliyemtembelea, basi ni muhimu ukaacha ujumbe kuwa ulikuwepo. Hii itasaidia kumfariji kipindi haupo, maana atajua kuwa kuna mtu yuko pamoja nae.

7. SIKILIZA KWA MAKINI
Usiwe mwepesi wa kuchukua maamuzi, muhimu zaidi ni kusikiliza kwa makini anachosema mgonjwa, ila epuka kuchukua maamuzi – muachie Daktari sehemu yake.

8. MGUSE MGONJWA
Mguso wa kibinadamu ni muhimu nyakati kama hizi, kulingana na ugonjwa wake, unaweza kumshika mgonjwa ipasavyo na akajisikia faraja, yaweza kuwa kichwani, mkono, ama hata bega, itamfanya ajisikie mko pamoja, na kusaidia kuvunja kuta za kutojisikia salama.

9. MTAZAME MACHONI
Jitahidi kutokwepesha macho unapokuwa na mgonjwa, bali mtazame machoni. Hii itamfanya ajisikie kujaliwa, na ndicho kitu kikuu anachohitaji mgonjwa.

10. ANDAA MOYO WAKO
Jiandae kwa utakachokutana nacho, na kwamba unamtembelea kwa upendo, si kama sehemu ya jukumu lako.
Wagonjwa hospitalini juwa wanatilia maanani kama upo hapo ilimradi tu, ama kwa dhati. MUNGU akubariki sana

Comments