HABARI PICHA: KILICHOTOKEA KANISA KATOLIKI PAROKIA YA MTAKATIFU JOSEPH, ARUSHA

imetoka gospel kitaa blog

Wananchi wakikimbia kuelekea barabarani kutoka Kanisa katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph iliyokuwa izinduliwe jana na balozi wa kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedict, Askfou Francisco Montecillo Padilla.
Sehemu ya mbele ya kanisa katoliki Parokia ya  Mtakatifu Joseph, Olasiti, Arusha.
Huzuni ikiwa imetanda kwa masista kanisani hapo.

Askari Polisi wakichukua sampuli eneo la tukio.
Wapelelezi wakiendelea na kazi yao eneo la tukio.

vikosi vya kila aina, ndani ya uniofrm na bila uniform.
Ufute wa polisi ukizungushiwa kuzuia watu kuingia eneo la tukio.
Taswira ya ndani ya kanisa hilo jipya,
Waandishi wa WAPO Radio, Gadlod Mg'ang'a na Masau Bwire wakiwahi eneo la tukio.


Msaada u katika Bwana aliyezifanya mbingu na nchi.
Sista akisikitika huku akimuelezea tukio lote mwandishi wa WAPO Radio FM, Gadlod.


Balozi wa Papa nchini Tanzania, Askofu Mkuu Francisco Padilla akisindikizwa nje ya kanisa na wanausalama kumuondoa eneo hilo.


Askofu Francisco Padilla akiwa ndani ya gari tayari kuondolewa eneo la tukio.
Escort ya jeshi la Polisi ikisindikiza gari iliyombeba balozi wa Papa nchini Tanzania.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Bwana Magesa Mulongo akiwasili eneo la tukio.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu tukio hilo.
Mkuu wa mkoa akiwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati jeshi la Polisi  likiendelea na uchunguzi wake.
Wanausalam kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa eneo la tukio kung'amua kiini cha mlipuko huo.

Wabunge Joshua Nassari na Godbless Lema wakiwasili eneo la tukio

Mbunge Godbless Lema akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, akilitaka jeshi la polisi kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kwenye vyombo husika kwa haraka kama ambavyo nguvu kubwa ilitumika kumkamata mapema kwenye kesi ya uchochezi dhidi ya mkuu wa mkoa wa Aeusha, Bw. Magesa Mulongo. 

Police line, do not cross.






Gari la kikosi cha zimamoto na ukoaji likiwa limekwama kwenye matope yaliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha jijini Arusha mfululizo.

Wananchi wakiwasindikiza wabunge wa CHADEMA kutokea kanisani hapo.

kazi ya wanatarumbeta ikiwa imekatishwa na mlipuko huo, jambo ambalo limepelekea kumaliza siku mapema.


Askari wa Umoja wa Matiafa akitokea eneo la tukio katika juhudi za kuokoa na kuweka mambo sawa, nyuma yake akiwa askari wa jeshi la polisi nchini


Comments