JE MUNGU AMETOA UHURU WA KUJITAWALA?


VICENT MWENGO


Ili tujue maana ya kichwa cha habari hii lazima tujue maana halisi ya neno utawala.

Utawala maana yake ni sheri a, kanuni na taratibu ambayo jamii fulani inafuata ambayo ndio katiba&muongozo wake, kujua maana ya neno hilo sasa turudi kwenye kichwa cha habari hii Mungu anapenda kutumia neno "lakini watu wengi hawajui" hili neno ni kubwa sana kwani leo jamii ya watu wengi sana ktk hii dunia hawalijui hili neno.

Kwa nini watu wengi ktk hii dunia hawajui, hii ni kutokana na kauli zao zakupenda kusema kuwa Mungu ametuumba wanadamu na akatupa uhuru wa kujitawala wenyewe, hii ni kauli mbaya mbele ya Mungu na ni kauli ya kumkataa Mungu, malaika wake, mitume wake na vitabu vyake.

Kwa sababu Mungu angetoa uhuru huo asingelileta vitabu ambavyo ni muongozo kwa watu ambavyo ndani yake mna sheria, kanuni zitakazo wafanya watu waishi kwa matakwa ya Mungu na ukifuata hivyo ina maana utakuwa unatawaliwa na Mungu je, utakuwa na uhuru?

Tukirudi nyuma inabidi tufahamu maana ya neno uhuru;-uhuru maana yake ni kufanya jambo lolote unalolitaka,sasa ikiwa umewekewa sheria,kanuni na taratibu za kufuata utakuwa nao huo uhuru?,kwa sababu ili sheria,kanuni na taratibu yoyote ile ili ifanye kazi lazima iwe na wasimamiaji ambao wameikubali ile sheria ndio waisimamie kwa wengine.

Kwa hiyo utaona manabii na waumini waliisimamia sheria,kanuni na taratibu ya Mungu vilivyo baada ya kukubali kutawaliwa na Mungu, kinyume chake ni kutawaliwa na shetani ambaye naye ana sheria, kanuni na taratibu ambazo ni kinyume na za Mungu ambazo nazo hazitoi uhuru kwa mtu kufanya analolitaka na wanakuwapo watu wa kuzisimamia ili zifuatwe kwa nguvu-zote tena kwa mali na nafsi zao.

Hiyo ndio maana halisi ya kuonyesha kuwa hakuna uhuru wa kujitawala iwe kwa Mungu au kwa shetani, sasa tuje kwenye neno uhuru wa kuchagua;-Mungu ametoa uhuru wa kuchagua na ndio maana akaonyesha njia mbili(2) ama Ushukuru au ukaidi, hapo ametoa uhuru ktk moyo wako na ndio akasema habadilishi yaliyo moyoni mwa mtu mpaka mtu abadilike mwenyewe.
Anachofanya Mungu ni kutoa elimu yake kupitia kwa watumishi wake ili watu wajue njia ya kufuata ama umfuate Mungu kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zake kisha umuepuke shetani na sheria,kanuni na taratibu zake au umfuate shetani na umkatae Mungu kwa sheria,kanuni na taratibu za kati ya njia hizo mbili.
Hii ni misingi 2 ya uhuru wa kuchagua kwa wanaadamu wote ktk hii dunia tangu wa mwanzo hadi leo hii na kuendelea hadi mwisho wa dunia,baada ya kuchagua njia yako ya kufuata kinachofuata kwa kila upande ni kuhakikisha kwa kila mwanadamu aliyechagua njia yake anaisimamia juu ya wanadamu wenzake(huu ndio utawala) na haya ndio makundi 2 ya utawala ktk hii dunia;-kundi la Mungu na kundi la shetani

Juu ya hali hizo mbili lazima kuwe na wasimamizi ambao ni viongozi na watendaji wote kiutawala, hao ndio wanaohakikisha ule uhuru wa mtu kufanya jambo atakalo usiwepo, kwani watathibitiwa na sheria,kanuni na taratibu zilizopo ikiwa ni za Mungu au ni za shetani inategemeana na jamii ilivyoshikwa, ikiwa imeshikwa na shetani kama ilivyo sasa ktk sehemu kubwa duniani basi watalazimishwa kufuata ya shetani, na ikiwa wameshikwa na sheria,kanuni na taratibu za Mungu watahamasishwa kuzifuata, kwa hiyo hakuna hiari ya kujitawala hapa duniani.

Jiangalie umo kwenye kundi gani lililokushika?-moja linapeleka motoni na moja linapeleka peponi (litafute hilo).

Kutokana na mada hii fupi ni kuwa Mungu hakutoa uhuru wa kujitawala bali ametoa uhuru wa kuchagua, kwa hiyo basi ukikataa kutawaliwa na Mungu basi, ujue utatawaliwa na shetani ktk sheria,kanuni,taratibu na mipango yako yote ya maisha hapa duniani.

Ndugu yangu sasa naomba ujitathmini kwenye maisha yako, kama hujaokoka fanya hima, mtafute Kristo ungali na muda.

MUNGU AKUBARIKI KWA KADRI YA AHADI ZAKE.

Na Vucent Mwengo

Comments