KUTOKA MGANGA WA KIENYEJI HADI MWALIMU WA KWAYA




                         

RESPIS MASANGO
MOJA YA SIKU ZA MAZOEZI YA KWAYA NA PIA MUNGU AMEMBARIKI KUMPA HUDUMA YA KUPIGA VYOMBO VYA MZIKA KAMA GITAA NA KINANDA
Shalom watu wa MUNGU, Naitwa Respisius Masango nimeokoka na nampenda BWANA YESU pia huduma yangu kanisani ni mwalimu wa kwaya kuu ya kanisa la Pentecostal Assemblies of GOD(PAG) Kawe hapa jijini Dar es salaam nina miaka 37, Namshukuru MUNGU maana naendelea vizuri kiafya na kihuduma pia. Napenda kuwashuhudia jinsi nilivyokuwa kabla ya kuokoka kama ilivyo kwa watu wengi huokolewa kutoka kwenye mambo mengi ambayo hayampendezi MUNGU BABA wa mbinguni, Mimi nimezaliwa katika kijiji cha kaseke huko kigoma vijijini na ni motto wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto 6 wa mzee Masango ambaye pia mwezi uliopita yaani mwezi wa 4 mwaka huu 2013 alifariki dunia. Ndugu kitu ambacho kinanisukuma kukushuhudia ni jinsi nilivyokua mganga maarufu wa kienyeji huko kigoma na baadae nilipohamia shinyanga  bado niliendelea na kazi hiyo. Nilianza uganga wa kienyeji baada ya kuishi kwa babu mmoja  mzee Mhoja ambaye alinifanya kuwa msaidizi wake wa kumletea dawa yaani mimi nilikua wa kuchimba dawa tukiwa porini pia nilikua natumika katika matambiko na kuchanja watu chale. Mzee Mhoja alinichagua mimi kwa maana alisema naweza kutunza siri bila mimi ni mchapa kazi  sana hasa wa kulima kwa kutumia jembe hivyo tukiwa porini kuchimba mizizi ya miti ambayo ilikua dawa asingepata taabu yeyote, mwanzoni alikua tu ananituma kusogeza vifaa vyake vya kazi katika kinyumba cha nyasi kilichokua pembeni kidogo ya makazi yake maana kwake kulikua na nyumba 6  lakini hii nymba maalum ya uganga ilikua kwa pembeni kama mita 50 kutoka pale nyumbani na katika kijumba hicho hakuna aliyekua anaruhusiwa kuingia isipokua yeye na mimi ambaye nilikua nampelekea vifaa vya ambavyo ni dawa za mitishamba, hirizi,pembe za ng’ombe, ngozi za chui na fuvu la mnyama ambaye hata sijui ni myama gani. Mzee Mhoja alikua msiri sana na ajabu ni kwamba waganga wengi akiwemo mzee mhoja siri zao hata wake zao hawawezi kujua siri hizo na mganga wa kienyeji lazima awe pia mchawi na nilijifunza hayo kwa huyu mzee, na ni matukio mengi sana niliyoyafanya na huyu mzee na tukio la ajabu zaidi la kwanza ni siku moja ambapo aliniambia kuwa usiku saa 6 kuna sehemu tutaenda kuchimba dawa maana mkuu wa anga amempa maono ya dawa ambayo hakusema ni ya kazi gani, ilipofika usiku hata sijui kama ilikua saa 6 au ni kabla ya hapo au hata ni baada ya hapo maana sikuwa na saa aliniamsha na tukatoka nje na kwenda kwenye kile kijumba cha kufanyia uganga na uchawi na siku zote chumba hiki kina utisho wa ajabu sana na utisho huo huwafanya wagojwa au wenye mahitaji kuogopa na kudhani kuwa mganga Yule ana nguvu sana za kuponya kumbe kuna mizimu6 na majini 3 na hii nilikuja kujua baadae maana kuna wakati alikua ananipaka dawa machoni na naona. Mle
 chumbani alimeza maziwa ya mbuzi na kuyatema kwa staili ya kuvuvia kidogo kidogo kila upande wa chumba huku akiongea maneno ambayo hata sikuyaelewa huku sauti za mizimu zikisikika pia. alipomaliza tuliondoka na kutoka nje na tukatembea kama hatua 10 wakatokea fisi wawili ambapo tulipanda juu kama watu wanavyopanda ngamia au punda na wale fisi wakubwa kama punda walianza kukimbia kuelekea porini na tulipofika mbele kidogo tulikutana na kundi jingine la wachawi ambapo kwa ajabu walituona lakini mzee Mhoja alifanya ishara Fulani kwa kutumia pembe ya mbuzi aliyokua nayo na wale wachawi hawakutuona tena ila sisi tuliwaona na wakaanza kusema kwa kuwa mzee mhoja amewaua wenzao 4 na lazima wampate tu n kumwua. ITAENDELEA
Mwl Respis Masango akiwaelekeza jambo wanakwaya wa kwaya ya kanisa la Kawe Pentecostal Church (KPC0 wakati wa mazoezi




Comments

Unknown said…
Mungu ambari sana,

ila tunasubiri mwendelezo wa shuhuda hii.