Skip to main content
VIZUIZI VYA KUSHINDWA KUFANYA HUDUMA YA MUNGU IPASAVYO.* sehemu ya kwanza*
 
  | 
| 
 | 
 Vipo vizuizi vingi vinavyotufanya kushindwa kufanya huduma ile 
tuliyoitiwa,hudumu  ya kazi ya Mungu.Vizuizi ni vikwazo au mambo 
yatuzuiayo kufanya huduma ya Mungu ipasavyo.
 Nasema hivi,kupitia 
vizuizi vilivyopo katika maisha yetu ya utumishi, vinatufanya kushindwa 
kufanya kazi ya Mungu ipasavyo,na sio tu kufanya kama kufanya kazi ya 
Mungu  Bali KUFANYA  KAZI YA MUNGU IPASAVYO,yaani kufanya vile Mungu 
atakavyo Yeye,wala sio sisi tutakavyo.
 
 Kwamba tulistahili 
kuifanya kazi ya Bwana katika viwango vya juu,lakini gafla tunashtuka 
hatufikii kile kiwango kinachohitajika.Basi ikiwa hali ipo hivyo,ni 
ukweli kwamba zipo sababu zinazotufanya kushindwa kuifanya kazi ya Bwana
 Mungu ipasavyo.
 
 • Vizuizi hivi hivitoki kwa Bwana Mungu,bali vyatoka kwa shetani na ufalme wake.
 
 Vizuizi  havitoki kwa Bwana Mungu kwa sababu Mungu ndie aliyekupa 
huduma  yake uifanye,hawezi tena kukuwekea kizuizi chochote,maana kama 
ange’likuwa ndio amekuwekea vizuizi basi asinge’likupa huduma hiyo.
 
 Mfano;
  Huwezi kumpa kazi mtoto wako aifanye,kisha ukaweka vizuizi juu ya kazi hiyo.
 
 Hivyo vizuizi ni sababu zinazoletwa na ufalme wa giza ili kuharibu kazi ya Mungu iliyopo ndani yako.
 Ikumbukwe kuwa Kila mtu aliyepo hapa Duniani,amekuja kwa MADHUMUNI na 
MAKUSUDI MAALUMU  yaliyotoka kwa BWANA MUNGU na ndio maana amezaliwa.
 
 Ipo KAZI moja tu ndani ya makusudi na madhumuni yaliyo ndani ya mtu  ambayo  KAZI hiyo ni kuliinua jina la Bwana.
 KAZI HIYO NI KAZI NJEMA MACHONI PA BWANA (Matendo 10 :38)
 Pia ufalme wa giza upo,ukienda kinyume na kazi ya Mungu,ili kusudi la Mungu lililopo ndani yako lisitimie ipasavyo. 
 
 • Vizuizi sio majaribu,wala vizuizi sio mitihani kana kwamba yanatoka kwa Mungu,la hasha !
 
 • Vizuizi ni  sababu za ILA mbaya zitokanazo na Ufalme wa giza,Tena 
kama vile mtu wa Mungu alivyopewa silaha za vita vya kiroho dhidi ya 
shetani na ufalme wake,Alikadhalika VIZUIZI ni  silaha ya ibilisi dhidi 
ya mtu wa Mungu,Vizuizi ni mali ya shetani.
 
 Mfano wa sababu/Vizuizi vinavyotufanya tushindwe kutekeleza kazi ya Mungu  kwa viwango vya juu.
 Tunasoma ;
 Mathayo 17 :14-21
 “  Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema Mbona sisi hatukuweza kumtoa? 
   Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, 
amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia 
mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno
 lisilowezekana kwenu. 
  [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] ”
 
 Katika andiko hilo tunaona vipo vizuizi viwili au sababu mbili kuu zilizowafanya wanafunzi wa Yesu kushindwa kufanya huduma. 
 
 Sababu hizo ni ;
 01.Upungufu wa imani
 02.Kushindwa kuishi maisha ya kufunga na kuomba.
 
 Kwa kupitia sababu hizo mbili ziliwapelekea wanafunzi wa Yesu kushindwa kufanya uduma ya Mungu jinsi ipasavyo.
 Si kana kwamba hawakuifanya,no!
  Walifanya ,lakini bila mafanikio yoyote yale.
 
 Leo sababu hizo zipo kwa watumishi wa Mungu,nazo ni vikwazo vya kutekeleza huduma ya Mungu ipasavyo..
 
 ITAENDELEA…
 UBARIKIWE.
 
 
 
 
 
 
  
 
 
 
 
 
Comments