VIZUIZI VYA KUSHINDWA KUFANYA HUDUMA YA MUNGU IPASAVYO.* sehemu ya pili *

Mtumishi Gasper Madumla





Nakusalimu ndugu mpendwa katika jina la Bwana,
Bwana Yesu asifiwe…
Jina la Bwana liinuliwe…

Karibu tuendelee kujifunza fundisho hili la msingi katika maisha ya mkristo haswa wewe na mimi tuliyepewa kazi ya kuzaa matunda yaani kazi ya kuinjilisha/kuleta watu kwa Kristo.
Kumbuka kwamba tunachoangalia katika fundisho hili ni sababu za msingi zinazowafanya watumishi au mkristo yeyote Yule kushindwa kufanya kazi ya Mungu ipasavyo.

Sababu hizo zinazozuia huduma ya Mungu ni VIKWAZO.
Kumbuka nilikuambia VIKWAZO ni VIZUIZI.
Vizuizi havitoki kwa Bwana Mungu.
Maana Vizuizi sio MITIHANI wala sio MAJARIBU.

Katika kitabu cha Mathayo 17 :14-21,
Biblia inatupa aina mbili za msingi za vizuizi/Sababu zilizowafanya wanafunzi wa Yesu kushindwa kufanya huduma ya Kristo Yesu Ipasavyo.

Nasema hivi,hawa wanafunzi wa Yesu walishindwa kufanya huduma ya Kristo ipasavyo pale walipoletewa mgonjwa mwenye pepo.
Maana kama suala la kuomba waliomba lakini hapakuwa na majibu kwa yale maombi waliyoyaomba na ndio maana nakuambia hawakuifanya kazi ya Bwana IPASAVYO.

Basi ikiwa hali ilikuwa ni hivyo,ni ukweli kuwa zipo sababu zilizowapelekea wanafunzi wa Yesu kushindwa kuifanya kazi ya Bwana ipasavyo maana walishindwa kutoa pepo hali ni wanafunzi wa Yesu.
Sababu hizo ndio leo hii tunaziangalia kiundani maana yamkini hata wewe zinakuhusu sana katika huduma yako.

Sababu hizo ni ;
01.Upungufu wa imani
02.Kushindwa kuishi maisha ya kufunga na kuomba.

01.UPUNGUFU WA IMANI '' Unbelief; for assuredly ''

Neno PUNGUFU lina maana ya :
(i) Isiyokamilika
(ii) Isiyotimia
(iii) Ndogo
(iv) Isiyojitosheleza
(v) Ya viwango vya chini.N.K

Sasa tazama Yesu anawaambia ni kwa sababu ya
“ Upungufu wa imani”
Tunasoma Mathayo 17 :20 :
“Yesu akawaambia, Kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu”

• Imani inayozungumziwa hapa ni IMANI inayotokana na kusikia neno la Kristo (Warumi 10 :17) na wala si vinginevyo.
Hivyo kitu walichokikosa wanafuzi wa Yesu ni KUSHINDWA KUISIKIA SAUTI YA KRISTO KWA YOTE, NA KWA UKAMILIFU.
Ambayo sauti ya Kristo/Neno lake ndilo liletalo imani ndani yao.

Maana kile walichokuwa wanakisikia kutoka kwake Bwana Yesu kilikuwa hakiwaingii chote ipasavyo na kusababisha wawe na imani pungufu.
Kwa sababu msikiaji wa neno ni mtendaji wa neno.
Hivyo kama wangelikuwa ni WASIKIAJI WA NENO wange’likuwa ni watendaji wa lile neno walilolisikia,
hivyo wange’weza kufunya huduma hiyo ya kumtoa pepo kwa Yule kijana aliyepagawa.

Kwa habari ya IMANI Biblia inatueleza kuwa
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. ” Waebrania 11 :1

• Hivyo IMANI PUNGUFU ni imani isiyokuwa na uhakika ya mambo yatarajiwayo.

Sikia;
Wanafunzi wa Yesu walikuwa na imani isiyokuwa na uhakika ya mambo wanayoyatarajia.
Hii ina maana kuwa,Wanafunzi wa Yesu walikuwa wakimfanyia maombi Yule kijana mwenye pepo pasipokuwa na uhakika kwa kile walichokuwa wanakiomba kwa sababu ya UPUNGU WA IMANI YAO.

Haleluya…
Jina la Bwana liinuliwe sana…

Naipenda Biblia ya kiingereza ya New King james Version (NKJV),jinsi ilivyotafsiri andiko hilo,inasema :
“ So Jesus said to them, "Because of your unbelief; for assuredly…”Mathew 17 :20

Ikiwa na maana kwamba “ Kwa sababu ya kutokuwa na imani isiyo na Uhakika”

• Kwa sababu hii moja tu, iliwapelekea kushindwa kumtoa pepo kwa yule kijana.

Na sio kana kwamba wanafunzi wa Yesu walikuwa hawana IMANI bali walikuwa nayo lakini imani yao ilikuwa ni PUNGUFU/a little faith.

• Imani pungufu ni Imani isiyoleta hathari katika jamii.

Yule mwenye imani kamili ni lazima alete hathari katika jamii yake alipo.Kuleta hathari katika jamii maana yake ni kuchafua hali ya hewa katika ulimwengu wa roho kwamba kila aina ya nguvu ya giza ni lazima ziondoshwe sio kwa hiyari yao bali ni kwa lazima.
Tena kila wanachokipanga hao wachawi,kinapanguliwa na IMANI KUU iliyo ndani yake yeye mwenye imani .

Mfano ;


Ikiwa wewe ndio mwenye Imani kamili,
wakipanga kukuletea jaribu la mapepo au wakita kukuuwa yaani waondoe maisha yako,gafla wewe unachafua hiyo hali kwa mishale ya moto,kwa imani katika Kristo Yesu,ile iliyopo ndani yako.

Hivyo baadaye utawakuta wanakuchukia tu ,maana wameshindwa kwa kila mpango,Na hiyo ndio maana ya hathali katika jamii yako.Mambo haya hayawezekani kwa kutumia akili zako Bali kwa IMANI katika Kristo Yesu,
Tena ni lazima uwe na IMANI KAMILI inayotokana kwa kusikia sauti ya Kristo tu.

Okey;
Sasa turudi kwetu sisi ambao tumekuwa Wakristo kwa IMANI katika Kristo Yesu.Ni ukweli kwamba tumejikuta nasi tumeshindwa kutekeleza huduma ya Mungu ipasavyo kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI YETU...

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments