Kumbuka kwamba tunachoangalia katika fundisho hili ni sababu za msingi
zinazowafanya watumishi au mkristo yeyote Yule kushindwa kufanya kazi ya
Mungu ipasavyo.
Sababu hizo zinazomzuia au kumfanya mtu aliyeyebeba huduma ya Mungu isiweze kuifanya katika viwango vya juu. Sababu hizi hujulikana kama VIZUIZI au VIKWAZO. Basi sasa nianze kwa kukusalimu wewe mpendwa,nikikuambia,
Bwana Yesu asifiwe… Haleluya…
Karibu sasa tuendelee na fundisho letu. Kumbuka tulikoishia katika sehemu ya pili. Kupitia kitabu cha Mathayo 17 :14-21
Tulifanikiwa kubainisha sababu/Vikwazo viwili vinavyotupelekea
kushindwa kuhudumu vizuri kwa habari ya kazi ya Bwana katika shamba
lake.
Sababu hizo ni : 01. Upungufu wa imani. 02. Kushindwa kuishi maisha ya kufunga na kuomba.
Tulijifunza kiundani moja wapo ya sababu /Kizuizi kinachomfanya mtu wa
Mungu kushindwa kutekeleza huduma ya Mungu iliyomo ndani yake. leo tunaendelea kuchambua sababu hiyo ambayo ni :
01.UPUNGUFU WA IMANI.
( Kwa maelezo ya awali ,tafadhali tafuta sehemu zilizopita ) “ Yesu akawaambia, Kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI yenu.
Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali
mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala
halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.” Mathayo 17 :20
• IMANI inapokuwa ni pungufu kwa mkristo anayefanya huduma,Basi ujue hawezi kupata mpenyo. Mfano kama mtu huyo mwenye imani pungufu akiwa ni muombaji,Basi ujue hakuna uponyaji utakaotokea baada ya maombi yake.
Tuendelee kutazama habari hiyo ya wanafunzi wa Yesu waliposhindwa kufanya huduma kwa sababu ya kuwa na upungufu wa IMANI. Tunaona Yesu akajibu, akasema, :
“ Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata
lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu. Yesu
akamkemea pepo, naye akamtoka; yule kijana akapona tangu saa ile. ”
Mathayo 17 :17-18
Mgonjwa yule alipoletwa kwa Yesu , Yeye Bwana Yesu hakutumia nguvu ya kumkemea kama walivyofanya wale wanafunzi wake, Bali alimuamuru pepo mchafu amtoke Yule kijana, naye huyo pepo akamtoka saa ile ile.
Nalipenda andiko hilo katika Biblia ya Bible in Basic English (BBE)
Andiko hilo linasema hivi : “And Jesus GAVE ORDERS to the unclean
spirit, and it went out of him: and the boy was made well from that
hour.” Matthew 17 :18
Alichokifanya Bwana Yesu ni kutoa TAMKO/AGIZO juu ya Yule pepo. Bwana Yesu alikuwa haitaji kutumia nguvu zake kwa kijipepo hicho. Ilikuwa ni rahisi sana kwa Bwana Yesu kutoa pepo,na wala si tu kwa sababu Yeye ni mfano wa Mungu Baba la hasha!
Bali pia Yeye alijaa IMANI KAMILI na hii ndio sababu ya msingi,maana
wanafunzi waliposhindwa kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI Yeye Bwana Yesu
akaweza kwa sababu ya kuwa na IMANI ILIYOKAMILI. Hapo tunajifunza
kuwa,haitajiki kumkemea pepo muda mlefu pasipo majibu,Bali tunahitajika
kutoa AGIZO lenye utiisho ndani yake juu ya kila aina ya mapepo na
ufalme wao wa giza.
Sikia;
Bwana Yesu alikuja awe
mfano na kielelezo kwetu sisi tulio ndani yake,na ikiwa Yeye aliyekuwa
ni mfano wetu.Tazama namna alivyomtoa pepo mchafu kwa AGIZO/ORDERS,
Halikadhalika sisi yatupasa tutoe agizo tu kwa pepo pasipo kutoka jasho
katika kukemea. Wengi tunasumbuka kushindwa kufanya huduma ya kutoa
pepo kwa usahihi kama vile Bwana Yesu alivyofanya.
Ikiwa tunashindwa kufanya hivyo,basi ni dhahili kabisa tuna UPUNGUFU WA IMANI.
• Kiwango chako cha Imani kitajidhihilisha kwa kazi huifanyao. • Kizuizi/Kikwazo namba moja cha mkristo kinachomfanya ashindwe kupata mpenyo/ break through katika yale ayaombayo ni UPUNGUFU WA IMANI.
• Mungu anatutizamia tuishi kwa IMANI ili tuhesabiwe haki, lakini
endapo kama tunasuasua katika Imani,Roho ya Bwana haitakuwa na furaha
nasi.
“ Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. ”Waebrania 10 :38
JE NINI DAWA YA IMANI PUNGUFU ?
01.Kusikia mara kwa mara neno la Kristo.( Warumi 10 :17) *Imani ni mbegu inayostahili kupandwa na kumea ndani ya roho zetu. Nasema ni mbegu, Mbegu ndio yaweza kumea na kuwa mti,mti mkubwa mithili ya mti wa mbuyu.
Kuna gharama kubwa unazotakiwa kulipa ili imani yako iwe kama mti wa
mbuyu,Ghalama ya kwanza kuacha vyote kwa ajili ya Bwana na sio kumuacha
Bwana kwa ajili ya vyote.
Nasema ghalama ya kwanza ya kutibu ugonjwa wa UPUNGUFU WA IMANI ni KUACHA VYOTE KWA AJILI YA BWANA.
-Maana ya kuacha vyote ni kukubali kumtegemea yeye kuwa ni Mungu pasipo
kumtegemea yoyote Yule,ni kumtanguliza Mungu kwanza katika kila jambo
ulifanyalo,Maana yake ni kuwa na Mungu mmoja tu…
Comments