“ANGALIENI,MIMI NAWATUMA KAMA KONDOO KATI YA MBWA-MWITU”(Mathayo10 :16) *Sehemu ya kwanza*

 na Mtumishi Gasper Madumla

BwanaYesu asifiwe….
Nakukaribisha mpendwa katika Bwana,karibu ujifunze fundisho hili la msingi sana katika maisha yako.
Neno la Mungu linasema;
“ Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.”Mathayo 10:16

*Bwana Yesu ametutuma kama KONDOO kati ya mbwa-mwitu.
Labda waweza kujiuliza kwamba kwa nini sisi tuliookoka tunatumwa kama KONDOO kati ya Mbwa-mwitu,na tusitumwe kama SUNGURA kati ya Mbwa mwitu?

-Au basi tusinge’litumwa kama SIMBA kati ya Mbwa-mwitu?
Haleluya…
*Katika andiko hilo (Mathayo 10;16),kondoo anawakilisha wafuasi wa Kristo Yesu,wale walio upande wake,yaani wale ambao Bwana amewatuma kwa ajili ya kazi ya injili na kwa ajili ya jina lake.
*Mbwa-mwitu anawakilisha lile kundi la wana wa uovu.
-Sifa moja wapo aliyokuwa nayo kondoo ambaye anawakilisha sisi tuliomkubali Bwana Yesu,ni hii;
*Kondoo hana maamuzi yake mwenyewe.
Na ndio maana kama umeshawahi kumuona kondoo aliyekuwa akichungwa,alafu kisha itokee gafla mfugaji amuache sehemu Fulanihivi,
Basi uwe na uhakika kondoo huyo hataondoka mahali pale mpaka mchungaji wake aje,

Tena atakaa pale pale pasipo kufanya maamuzi yake mwenye,huku akisubili aangozwe na bwana wake.
Sisi wakristo tunafananishwa na KONDOO kwa sababu hiyo ,ya kwamba yatupasa kutochukua maamuzi yetu wenyewe juu ya jambo lolote lile tulifanyalo,

Bali tumsubili kiongozi wetu yaani ambaye ni mchungaji,mwalimu wetu,dira yetu,naye ni Yesu Kristo ,Yeye ndiye atatuongoza katika sehemu sahihi,Tazama siri hii DAUDI aliifahamu hata akasema;
“ Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.” Zaburi 23 :1-2

Inabidi tufike wakati ambapo tumtegemee Bwana tu,maana yule amtegemea Bwana hatapungukiwa kabisa,na muda wote ataongozwa katika njia sahihi.
Kondoo ni wa pole sana tofauti na mbwa –mwitu,Maana Kodoo wanamtegemea mchungaji wao muda wote….

ITAENDELEA..
USIKOSE.
UBARIKIWE.

Comments