Biblia ni nini?

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Kuna majibu mengi juu ya dhana ya Kitabu hiki, kiitwacho Biblia. Moja wapo ya majibu haya ni pamoja na
-Biblia ni kitabu cha Kikristo, yaani kinawaongoza wakristo. Licha ya kuwa ni kitabu cha zamani sana, ila ni kitabu cha adhimu na muhimu sana. Thamani ya Biblia ni zaidi ya pesa, dhahabu au mali yoyote uipendayo.
-Kitabu hiki, kina uvuvio wa Mungu moja kwa moja kwa kuwa, maneno yaliyoandikwa huko, ni pumzi ya Mungu kamili. Tofauti na vitabu vingine, biblia ni kitabu kinachoishi na kinahuisha kwa kuwa kina pumzi ya uhai.
Ushahidi wa Kibiblia, unaweza kufasili kuwa Biblia inaelezwa katika namna tatu ambazo ni:-
(a) BIBLIA – Ni “Maandiko matakatifu ya Mungu” uKifungua
Biblia Ukurasa wa kwanza kabisa, utakutana na maandishi yanayosema” Maandiko matakatifu ya Mungu yaitwayo BIBLIA yaani Agano la Kale na Agano Jipya”. Pia Ukisoma (2Timotheo 3:15)... na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu,amabayo yanaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
(b) BIBLIA- Ni “Neno la Mungu lenye uzima, Hudumu hata milele” (Yohana 1:1&3)”
Hapo mwanzo kulikuwepo Neno,naye Neno alikuwepo kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. (Ufunuo 6:9)”...nikaona chini ya madhabahu, roho zao waliochinjwa kwaajili ya NENO la Mungu....”
(c) BIBLIA- Ni “Neno lenye pumzi ya Mungu, na lipo kwaajili ya mwanadamu”
(2Timotheo 3:16&17) “Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho,na kwa kuwaonya, watu makosa yao, na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadibisha katika haki ili mtu wa Mungu awe kamili....”

Ni dhajiri kuwa, Biblia, ni kitabu kitakatifu, chenyekusheheni Busara na Hekima ya Mungu. Ni neno linaloishi, lenye nguvu, uweza,na linafaa kwa mafundisho. Linamwongoza mwanadamu katika njia ya kweli, huku akimwelekea Mungu.
Ukiiamini Biblia, unapata uwezo na mamlaka juu ya vitu vyote, na ukiomba lolote kwa kulitumia neno la Mungu, utafanyiwa, kwa maana Neno la Mungu, ndiye Yesu mwenyewe.(Ufunuo 19:13).
“Mkiniomba neno lolote kwa jina langu nitalifanya(Yohana 17:14).

Swali la Kujiuliza, Kama Biblia ni neno la Mungu, na pia ni pumzi ya Mungu, ilandikwa na nani na iliwezekana vipi?
Biblia iko wazi juu ya hilo kuwa, pamoja na hayo yote, Biblia iliandikwa na wanadamu, tena tofauti tofauti. Pengine hata utamaduni wao ulikuwa tofauti, sijui, ila ni dhahiri kuwa, hapakuwa na upendeleo juu ya ukoo fulani, pengine wa Kifalme au la, juu ya uandishi wa Biblia.
Maandiko matakatifu yanasema” Biblia ni maandiko yaliyo andikwa na watu tofautiwalioongozwa na Roho Mtakatifu, Yaani Manabii. (Yohana 17:17). Biblia siyo hadithi za kutungwa kama vilivyo vitabu vingine, siyo katiba ya nchi wala haijaandikwa kiujanja ujanja tuu, (2Petro 1:16-21) “Maana hatukufuata hadithi ziizotungwa kwa werevu.Tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake, bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.......18Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa naye.......20mkijua neno hili kwanza kuwa hakuna unabii katika unabii upatao kufasiliwa kama apendavyo mtu fulani tu. 21Maana unabii haukuletwa popote kwa kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Watu hawa awaliongozwa na Roho wa Mungu katika kuyaandika maneno haya ya Mungu. Pia Malaika walikuwapo ili kuwaelekeza namna ya kuandika (Ufunuo 1-3:22, Soma tafadhari).

Lengo la Biblia ni nini?
Ukweli ni kuwa, Mungu aliwekeBiblia kwa lengo kuu moja, ambalo ndilo mahususi na maalum kabisa, kuwa ni UKOMBOZI wa mwanadamu(Mwanzo 3:15). Pamoja na kuandikwa na watu tofauti tofauti, wenye elimu na utamaduni tofauti na mazingira tofauti, ila wote, walielekezwa katika kumkomboa mwanadamu kwa kumuonya, kumwelekeza na kumwongoza katika njia iliyo ya kweli ambayo ni Yesu Kristo.

Mungu akubariki na kukuinua, akufunulie zaidi na zaidi umjue sana na kumpenda, Katika Jina la Yesu Kristo nimeomba.
Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

Comments