JE, NGONO NDIYO DHAMBI YA KWANZA AMBAYO ADAMU NA HAWA WALIFANYA KATIKA BUSTANI YA EDENI?

Mwinjilist Newdaudimakubi




Watu wengi hufikiri kwamba
tunda ambalo Adamu na Hawa
waliambiwa wasile katika
bustani ya Edeni lilimaanisha
uhusiano wa kingono.

Lakini
Biblia haifundishi hivyo.
Hebu fikiria hili: Hata kabla Hawa
hajaumbwa, Mungu alimwamuru
Adamu asile matunda ya “mti wa
ujuzi wa mema na
mabaya.” (Mwanzo 2:15-18) Amri
hiyo haikumaanisha uhusiano wa
kingono kwa sababu Adamu
alikuwa peke yake. Zaidi ya hayo,
Mungu aliwapa Adamu na Hawa
amri hii iliyo wazi: “Zaeni, muwe
wengi, mjaze dunia.”
(Mwanzo 1:28).

Je, Mungu mwenye upendo
angewapa wenzi hao wa ndoa
agizo la ‘kujaza dunia’ – jambo
ambalo bila shaka, lingehusisha
uhusiano wa kingono – kisha
awahukumu kifo kwa kutii
maagizo yake? – 1 Yohana 4:8.
Kwa kuongezea, Adamu
hakuwepo Hawa ‘alipoanza
kuchukua na kula kati ya
matunda aliyokatazwa. Baadaye
alimpa mume wake pia
alipokuwa pamoja naye, naye
akaanza kula.’ Mwanzo 3:6.
Mwishowe, Mungu
hakuwahukumu Adamu na Hawa
walipofanya ngono na kuzaa
watoto. (Mwanzo 4:1,2)
Kwa
hiyo ni wazi kwamba tunda
ambalo Adamu na Hawa walikula
halikumaanisha tendo la kufanya
ngono bali lilikuwa tunda halisi
lililokuwa mtini.

Comments