KUTOKA MGANGA WA KIENYEJI HADI MWALIMU WA KWAYA


RESPIS MASANGO


Respis Masango anaendelea kusimulia matukio ambayo aliyafanya na mzee mhoja aliyekua mganga wa kienyeji, na baada ya kuishi kama msaidizi wa mganga mhoja na baadae kufundishwa jinsi ya kufanya katika kazi za uganga na uchawi amefika katika tukio ambalo waliondoka usiku wa mamane yeye na mzee mhoja kwa kutumia usafiri wa fisi kwenda porini kutafuta dawa.Huyu hapa anaendelea.
…………alipomaliza tuliondoka na kutoka nje na tukatembea kama hatua 10 wakatokea fisi wawili ambapo tulipanda juu kama watu wanavyopanda ngamia au punda na wale fisi wakubwa kama punda walianza kukimbia kuelekea porini na tulipofika mbele kidogo tulikutana na kundi jingine la wachawi ambapo kwa ajabu walituona lakini mzee Mhoja alifanya ishara Fulani kwa kutumia pembe ya mbuzi aliyokua nayo na wale wachawi hawakutuona tena ila sisi tuliwaona na wakaanza kusema kwa kuwa mzee mhoja amewaua wenzao 4 na lazima wampate tu na kumwua. Tulikaa katika hali hiyo ya wao kutokuona kwa muda  kwa muda kama wa dakika 10 huku mzee mhoja akiniambia kuwa wsiku hiyo ni mbaya na anaona njia imezibwa japokua wale wachawi hawatuoni.Wale wachawi walianza kuongezeka na kuwa wengi sana na jambo ambalo nilishangaa ni kitendo cha wachawi kutafutana wao kwa wao, baadae kidogo nilianza kuona mwili mzito na giza kuongezeka hadi nikawa sioni na jambo la ajabu wale fisi wetu waliganda chini ya ardhi na hakuna hata mmoja aliteweza kusogeza mguu mbele, mzee mhoja alijitahidi sanakutumia maarifa ili tukimbie kurudi nyumbani maana hali ilianza kuwa mbaya lakini ilishindikana na na kushindikana na akaanza kusema hakika wakituona watatuua akaamua kunipa hirizi Fulani iliyokua ndani ya mkoba wake na akaniamuru nishuke juu ya fisi na nianze kukimbia nilifanya hivyo na yaani nilishuka haraka na kuikamata ile hirizi na kuanza kukimbia ,nilikimbia bila kuonekana kwa muda kama wa dakika 5 na kwa mbele kidogo giza lilipungua na baadae kuisha na kwa kwa sababu ya ile dawa aliyonipaka kabla ya safari kuanza ilikua na uwezo kunifanaya nione kila kitu japokua ilikua ni usiku, nilikimbia hadi nyumbani japokua nilikua umbali kama wa vijiji 3. Nilifika saa 11 asubuhi huku nimechoka sana nilimkuta mzee mhoja ameshafika tayari na ajabu hata wale fisi walikua wameshafika, baada ya hapo sikumwamini tena mzee mhoja na pia nilidhani alinitoa sadaka siku ile maana aliondoka na usafiri wa fisi huku mimi nikitembea kwa mguu, baada ya tukio hilo kupita niliendelea kuwa msaidizi wa mzee Yule huku nikifanya kazi moja tu ya kuiandika majina miti yote tuliyokua tunaenda  ili baada ya mwaka mmoja nitoke pale na kwenda mbali na mimi nikafanye kazi hiyo ya uganga ila nifanye bila uchawi, nilifanya hivyo ila kwa bahati mbaya sana baada ya miezi 4 mzee mhoja alifariki ghafla na mimi hadi leo naamini alizidiwa uchawi na hakika walimuweza. Baada ya kifo cha mzee mhoja pale nyumbani paligeuka kuwa uwanja wa kifo maana baada ya kifo cha mzee mhoja alifuata mke wake siku chache tu baadae watoto wawili walifuata na pia wagojwa au watu wenye mahitaji walikoma kuja niliogopa sana na kutoroka pale nyumbani na kwenga Maswa shinyanga ambako kwa sababu ya mazoea nilikwenda kutafuta kibarua cha kulima huku nikiwaambia watu kwamba mimi ni mganga wa kienyeji na kuna baadhi ya watu niliwapa dawa  lakini hata hawakupona lakini MUNGU alinihurumia kwa kuniokoa nikiwa huko huko Maswa shinyanga baada ya kuugua sana kifua kikuu lakini nilipoombewa nilipata nafuu na baadae nilipona. Na ndio ukawa mwisho wa uganga wa kienyeji.MUNGU awabariki sana na ni kwa neema yake tu maana siku ile nikiwa na marehemu mzee mhoja ningekufa ila MUNGU akanihurumia.



BAADHI YA WAIMBAJI WA KWAYA YA KPC WAKIWA KATIKA HUMA KANISANI,

Comments