KWANINI WATU WENGI WANAPISHANA NA BARAKA ZAO?





Watu wengi wanapishana na baraka zao kwa sababu wanaomba na wakiwa katika kusubiri majibu ya kile walichoomba wanatenda dhambi na ndio wakati huo huo ambapo malaika analeta baraka. inakua ni ngumu kupewa baraka yako maana inakua ni kama mama na mtoto wake ambapo mtoto anamwambia mama kwamba akirudi kutoka sokoni amletee zawadi na wakati mama akiwa sokoni ananunua zawadi hiyo nzuri kwa ajili ya mtoto wake na wakati mama ananunua zawadi mtoto anajisaidia haja kwenye nguo na pia kwa sababu mvua imenyesha mtoto anajichafua kwa matope mwili wote, mama akirudi atawaambia wamsafishe na kumwosha kwanza yule mtoto ndipo ampe zawadi aliyomtuma. Hata kwa MUNGU ni hivyo baraka anatuletea lakini akifika anatukuta tuko wachafu kwa sababu ya dhambi hivyo anasubiri tuwe safi kwanza ndipo tupokee. Ndugu tudumu katika kumwomba MUNGU na wakati huo huo tudumu katika utakatifu ili tupokee baraka zetu tulizoomba kwa MUNGU wetu. MUNGU awabariki sana

Comments