NAOTA NDOTO ZA KUFA KILA SIKU





                                      
Mtu wa MUNGU, BWANA YESU asifiwe. Mimi ni mzima ila tatizo kuu na kubwa maishani mwangu ni kuota ndoto za kufa kufa kila siku na kama ikititokea sijaota nakufa au nimekufa au niko kwenye jeneza ni mara chache sana ila kila mara naota nakufa au nimekufa au niko kwenye jeneza. Je jambo hili ni nini? Naomba msaada wako au kwa sababu wewe unafahamiana na watumishi wengi basi omba majibu ili kunisaidia maana jambo hili huniletea woga sana na kuna siku hadi nilijiandaa kwa kutubu ili hata nikifa niende mbinguni. Nimeokoka tangu 2010  na jambo hili nimemwambia rafiki yangu wa kike akaniambia niombe tu kwa MUNGU ili kuvunja mpango wa shetani maishani mwangu, nimeomba lakini hupungua tu kidogo yaani naweza nikapitisha siku 4 au 5 lakini jambo hilo hurudi tena na mambo ya kupungua kwa tatizo langu hili yameanza siku za karibuni tu ila mwanzo haikua hivyo. Jambo kubwa nataka nijue ‘’KUOTA NDOTO ZA KUFA INAMAANA GANI?’’. Pia naomba msaada wako kama unafahamu maana kuna rafiki yangu yeye ameota anakimbizwa na nyoka  na pia kuna dada yangu yeye kuna siku aliota nakimbizwa na mbwa na hatimaye yule mbwa akamng’ata mguuni. MUNGU akubariki sana na  naomba majibu sahihi maana mimi naamini kabisa ndoto ni ujumbe haijalishi ni ujumbe mzuri au mbaya, ni hayo tu. Ni mimi Lucy Khamis niko manyoni singida.



MAJIBU  KUTOKA MAISHA YA USHINDI BLOG.



Lucy ubarikiwe kweli kweli na umeuliza mambo ambayo hakika yanagusa wengi sana na ni wengi sana wametokewa na mambo hayo. Na majibu haya naomba yamsaidie kila mmoja atakayesoma haya. Ni kweli kabisa ndoto ni ujumbe na ndoto ni tukio la ulimwengu wa roho na ulimwengu wa roho unaweza kuwa ni ulimwengu wa roho wa nuru chni ya ROHO MTAKATIFU au ulimwengu wa roho wa giza ambao shetani na malaika zake ndio wahusika.
Kuna aina 3 za ndoto anazoota mwanadamu.
1: Ndoto au ujumbe kutoka kwa MUNGU
2:Ndoto za shetani
3:Ndoto ambazo zinatokana na mtu mwenyewe. yaani yawezekana kwa kuliwazia sana jambo fulani inapelekea unaota jambo hilo, au mfano unafiwa na mtu muhimu sana kwako inapelekea kumfikiri mtu huyo kila muda nayo inaweza kupelekea kumwona kwenye ndoto.

 KUOTA NDOTO ZA KUFA :
ni ishara ya kufa kiroho kwa mtu aliyekua amesimama katika imani ya KRISTO pia wakati mwingine yawezekana kuna vitu vya shetani vimekufunga ambavyo umewahi kuingia navyo maagano mfano matambiko au kwenda kwa waganga wa kienyeji au hata kurogwa hivyo unapoota uko kwenye jeneza inamaana uko kwenye kifungo fulani ambavyo kinasababisha kushindwa  kutimiza lengo la MUNGU kwako hivyo unapewa taarifa  ili kwa njia ya maombi wewe mwenyewe au kwa kutumia watumishi wa MUNGU waaminifu ufunguliwe kutoka kwenye maagano hayo ya shetani. Pia ishara ya kufa ni kuonyesha huwezi kufanikiwa maana shetani amekufunga hivyo hadi utoke kifungoni au kwenye hilo jeneza. Wapo watu wengi wanashindwa wako kwenye majeneza ya shetani ya magojwa , wengine wako kwenye majeneza ya mikosi, wengine wako kwenye majeneza ya kukataliwa na wachumba yaani kila akipata mchumba wakitaka tu kufunga ndoa anamkataa , wengine wapo kwenye majeneza ya kuonekana wabaya mbele za watu kwa sababu jini shamsu anakua amevaa sura ile ndio maana mke wake au mme wake anampenda kwa muda tu na baada ya muda ni vita, wengine wako kwenye majeneza ya hasira, uongo n.k. na hii chanzo chake ni shetani ambaye katika Yohana 10:10 huwa anakukuja kwa watu ili kuvunja, kuharibu na kuua na kwa kusudi hilo ndio maana Mwana wa MUNGU, YESU KRISTO alidhihirishwa ili azivunje kazi zote za shetani (1 Yohana 3:8b). Ndugu nenda kwenye maombezi na utakuwa huru mbali na kuonewa na shetani na kwa wewe uliyeokoka ukiona yanakutokea hayo basi tambua kuwa kuna mlango umeufungulia ndio maana unaonewa maana pia kumbuka kuwa MUNGU ni mtakatifu.


KUOTA  UNAKIMBIZWA NA MBWA:
Ni ujumbe kwako kwamba roho ya uasherati au uzinzi inakunyemelea , hii ni hatari sana na kuna rafiki yangu kazini aliwahi kuota anakimbizwa na mbwa na baadae mbwa huyo akamng’ata na nilimwambia afunge na kuomba avunje roho hiyo lakini kwa bahati mbaya hakufanya hivyo na hakika miezi 2 baadae alijikuta ameanza uasherati na dada mmoja na ikawa na ngumu sana kuacha  na ikafika kipindi akitaka kuachana na dada yule yule dada anamwambia akimwacha atajiua hadi siku za karibuni tu ndio ameacha tabia hiyo kwa maombi mengi sana ya watumishi . hivyo usipuuzie unapoota unakimbizwa na mbwa tambua kuwa dhambi ya uzinzi inakunyemelea na kumbuka kuwa ndoto ni jambo la ulimwengu wa roho hakuna jambo hata moja linalotima katika ulimwengu wa roho hata kama unaona ajali zinatokea hilo ni mpango wa shetani ulioandaliwa katika ulimwengu wa roho ndio baadae unakuja kutimia katika ulimwengu wa mwili. Hivyo mbwa katika ulimwengu wa roho ni roho ya ukahaba au roho ya yezebeli.

KUOTA UNAKIMBIZWA NA NYOKA :
 ni ujumbe kwako kwamba roho ya uongo inakunyemelea maana nyoka katika ulimwengu wa roho ni roho ya uongo na kumbuka shetani alivaa umbo la nyoka na kuwadanganya hata akina Adamu na Hawa  katika bustani ya edeni wakatenda dhambi (Mwanzo 3:4)  na katika Ufunuo 20:2 shetani anaitwa nyoka wa zamani yaani aliyewadanganya akina Adamu na Hawa. Hivyo ni kuwa makini sana na kuvunja roho hiyo kwa jina la YESU KRISTO na mpango huo wa kuzimu hautafanikiwa. Na mfano mzuri ni mimi siku moja nikiwa kanisani tunaomba nilimwona nyoka anazunguka na kwa sababu nilikua sijajua kwamba hiyo ni roho ya uongo unanyemelea watu wa MUNGU hakika kesho yake ulizuka uongo mkubwa na kusababisha hadi baadhi ya viongozi wa kanisa kukosana  na ndio ikawa mwanzo wa mimi kujua kwamba nyoka anamaanisha nini katika ulimwengu wa roho.
MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kuwa suluhisho pekee la yote haya na yote yanayowasumbua wanadamu ni YESU KRISTO na yeye mwenyewe katika Mathayo 11:28 anasema

Comments

Anonymous said…
Asante kwa ufafanuzi wako,ila kuna wengine wanashauri kuwa nyoka ni roho ya uzinzi pia.Ndugu mtumishi kama una huduma ya kutafsiri ndoto weka blog yako vizuri kwa sababu yani kuna ndoto kila siku-ubarikiwe
Peter Mabula said…
ubarikiwe sana ndugu na nauhakika hakuna jambo linaloshindikana kwa MUNGU na kwa jambo ambalo nalifahamu lazima nilisema na hata kama wewe una swali au ndoto tuambiane tu ili tujifunze pamoja