NDOA NA NDUGU WA MUME

Pastor Donis and Nnunu Nkone

Kuolewa na mwanaume ambaye anategemewa kwao na ndiye mtoto kipenzi cha mama, inahitaji mwanamke mvumilivu na aliyeokoka kweli kweli. Mwanaume ambaye ni kipenzi kwa mama yake na anayempenda saaana sana mama yake, lazima aombe sana busara kwa Mungu ili ajue namna ya kuiongoza ndoa yake, kumlinda na kumsikiliza mkewe. Mwanamke anayeolewa mwanaume wa hivi, anahitaji kuombewa sana ili aweze kuvumilia mpaka hapo mambo yatakapokuwa yametulia. Kama wewe msomaji ujumbe huu unakuhusu, Mungu akutie nguvu na kukuongezea hekima huku akikuponya na machungu. Kama ndoa ni changa, basi mume wa namna hii ajitahidi kuishi nyumba ambayo ni mbali na wazazi. Wewe mume usithubutu kumsahau mama yako, na wewe mke usithubutu kumfanya

mume wako asimjali mama. Mtapata laana mbaya. Ombeni uvumilivu kwa Mungu na yeye Mungu atawasaidia.

Pata Kitabu chetu ili ujifunze namna ya kuishi na ndugu wa ukweni kwako.
By Pastor Donis and Nnunu Nkone

Comments