Tarehe 8 june 2013 kulifanyika ibada ya ubatizo wa waamini wape walioamua kumpa BWANA YESU maisha yao katika kanisa la Kawe Pentecostal Church maarufu kama K P C karibu na lugalo jeshini na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Rev. Elly Boto ndiye aliyeongoza zoezi hilo, watu saba walibatizwa na kuanza maisha mapya yenye ushindi ndani ya YESU. akifundisha somo la utangulizi kabla ya ubatizo Mchungaji Boto alifundisha kuwa KUBATIZWA NI KUITIMIZA HAKI YOTE YA MUNGU kama BWANA YESU alivyomwambia Yohana mbatizaji alipokua anataka kumbatiza. baada ya hapo Mchungaji Boto alifundisha somo fupi kwamba.
MTU YUPI ANAYETAKIWA KUBATIZWA?
Huyu ni mtu aliyetubu dhambi,
kama hujatubu dhambi ubatizo wako si wa kibiblia. Matendo ya Mitume 2:37, hivyo kanuni ya Mungu ni kwamba mtu anatubu
kwanza ndipo anabatizwa, lakini maeneo mengi watu hubatizwa wakiwa watoto
wachanga ambao hawawezi kutubu. Hivyo kama ulibatizwa ukiwa mtoto mchanga, huo
sio ubatizo wa kibiblia. Marko 16:15-16,
Na ndio maana Yesu aliagiza kwa kusema aaminiye na kubatizwa, kumbe kinachoanza
ni kuamini alafu unabatizwa.
Tumeona mambo kadhaa yanayoendana
na ubatizo wa kibiblia, yaani unatubu kwanza, ndipo unabatizwa. Matendo ya Mitume 8:12, Biblia
inaendelea kusema kuwa wakaamini wakabatizwa, huwezi kusema umebatizwa kama
hujaamini bado. Matendo ya Mitume
8:35-38, katika biblia hakuna aliyebatizwa bila kuamini kwanza, na ndio
maana Filipo alimwambia Yule towashi kwa habari ya ubatizo “ukiamini
inawezekana” kumbe ubatizo wa kibiblia unaamini kwanza ndipo inawezekana
kubatizwa. Ni swali la kujiuliza kuwa ulipobatizwa uliamini kwanza. Matendo
ya mitume 19:1-. ona tukio hilo katika picha ambapo wengine walipokee nguvu za MUNGU na kuwa wapya.
 |
Mchungaji Elly Boto akifundisha neno la MUNGU kama utangulizi kabla ya jukumu la ubatizo kuanza |
 |
Mchungaji Elly Boto akiwaelekeza jambo waliokuja kubatizwa
 |
watu walimsifu MUNGU kwa nyimbo kabla ya ubatizo
 |
watu walimsifu MUNGU kwa nyimbo kabla ya ubatizo |
|
|
 |
MAMA NASHONI TAYARI KWA KUBATIZWA NA BAADA YA KUBATIZA ALIPOKEA NGUVU ZA MUNGU NA KUJIONA WA TOFAUTI |
 |
ASANTE YESU KWA MATENDO YAKO MAKUU |
 |
DIANA TAYARI KWA KUBATIZWA |
 |
MARTHA BAADA YA KUBATIZWA |
 |
HONGERA SANA KWA KUBATIZWA NA KUITIMIZA HAKI YOTE YA MUNGU |
 |
ELIZA AKIOMBEWA BAADA YA KUBATIZWA |
 |
HONGERA SANA KWA KUBATIZWA NA KUITIMIZA HAKI YOTE YA MUNGU |
 |
NIMEAMUA KUMFUATA YESU NA NYUMA KAMWE SITARUDI |
 |
BAADA YA UBATIZO MIMI BLOGGER NIKIWA NA MCHUNGAJI ELLY BOTO WA KANISA LA PENTECOSTAL ASSEMBLIES OF GOD (P A G) KAWE NA HAPA PALIKUWA NA KAWE BEACH KATIKA BAHARI YA HINDI |
Comments