TAMANI SANA URAIA WA MBINGUNI.* sehemu ya kwanza *


Mtumishi Gasper Madumla.
Uraia tulionao hivi sasa wanadamu ni uraia wa kupita tu.
Uraia usiokuwa na makazi ya kudumu,
Uraia usiokuwa na uzima wa milele ndani yake.
Uraia wenye kuaharibika.

Lakini leo hii nina kutangazia rasmi kwamba upo URAIA usiofanywa na wanadamu,URAIA wa kudumu uliokusudiwa na Mungu Baba mwenyewe,Uraia wenye maana ,Uraia wa umilele,nao ni URAIA WA MBINGUNI.

*Uraia wa Minguni ni urithi wa watakatifu waliopo hapa hapa Duniani .
Nasema ni Urithi wa watakatifu waliopo hapa hapa Duniani
kwa sababu watakatifu hawa waliopo Duniani kwanza Mungu ndio hupendezwa nao (Zab.16:3).
Sasa watakatifu hawa pindi waendapo kwa Mungu Baba,si kana kwamba wanakwenda mbinguni kuanzisha URAIA wao binafsi bali wanakwenda kurithi uraia wa mbinguni walowekewa tayari.

* Yapo maisha yaliyokusudiwa na Mungu tuishi baada ya maisha haya yenye kuharibika kupita. Mungu amekusudia tuishi katika mfumo mwingine wa maisha ya umilele,baada tu ya sisi kuondoka katika Dunia hii chafu.

* Maisha hayo yaliyokusudiwa ni maisha yasiyokuwa na mwisho.
Hivyo basi Urithi haswa wa Mkristo ni maisha ya Mbinguni, Na ndio maana ninakuambia utamani sana uraia wa mbinguni.

Mkristo aliyesafi hutamani sana hata aachane na URAIA huu wa Duniani kisha aungane na watakatifu katika URAIA wa mbinguni.
Nami nipenda nikupe mifano michache ya baadhi ya watakatifu ambao kwa moyo mmoja waliamua kuishindania IMANI,
kwa ajili ya kuupata URAIA wa mbinguni. Wakristo wa namna hii ni wakristo waliokubali kupoteza maisha yao ya hapa Duniani.Ili kupata maisha ya mbinguni kwa njia ya Kristo Yesu.

Tena ni Wakristo waliokubali kupoteza URAIA wa Duniani uliofanywa na wanadamu ili waupate URAIA wa Mbinguni usioharibika WENYE KUTOKANA NA MUNGU BABA.
Kumbuka ,
hata Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuhusu habari ya mtu atakaye kuiponya nafsi yake,pamoja na Yule ambaye mwenye kuiangamiza nafsi yake kwa ajili ya Bwana.

Tunasoma Marko 8 :35 35;
“ Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.”

* Kwanza kabisa napenda tumuangalie Stephano mtu aliyejaa IMANI,pia mtu aliyejaa Roho wa Bwana,mtu mwenye hekima za ki-Mungu,mwenye kujaa UPAKO,nami napenda kumuita Mtakatifu Stephano.

Stephano alikuwa sio mtume,
bali alikuwa ni miongoni mwa watu saba waliochaguliwa wenye kushuhudiwa kuwa ni watu wema,
wenye kujawa na Roho,na hekima.
Mtu huyu aliona ni afadhali sana kuuwawa akimshuhudia Bwana na Utukufu wake.
Hivyo alitamani sana kuvikwa vazi lisiloharibika,yaani alitamani sana URAIA wa mbinguni.

Tunasoma Matendo 7 :54-56;
“ Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno.
Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.”

- Tazama huo mstari wa 54 wa andiko hili tulilolisoma “ Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno ”
Hapa tunaona watu hao ambao Stephano aliokuwa akizungumza nao,
kwanza walikuwa na nia mbaya kwa Stephano maana waliposikia tu wao hawakukubaliana na Stephano hata wakamkazia macho.

Lakini ingawa kuna hali kama hiyo Bado Stephano tunamuona akikaza macho yake mbinguni ,maana yake ni kwamba aliona maisha mengine mazuri kuliko haya,ndio maisha ya mbinguni kwa kufanyika raia.
Tena tunamuona Stephano akipaza sauti yake na akiona Utukufu wa Mungu,pamoja na mwana wa Adamu akisimama mkono wa kuume wa Mungu.

- Haikuwa ni rahisi kuona watu wemekusagia meno yao wakiwa na mawe mikononi mwao tayari kabisa kukupiga hata kufa,Kisha uzidi
kupingana nao tena zaidi ya yote upaze na sauti kuubwa kwa maneno ambayo unajua kabisa kama wakiyasikia ndio yatawachoma mioyo yao na kupelekea kukuuwa.

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments