Nakusalimu katika jina la Bwana nikikuambia, Bwana Yesu asifiwe… Haleluya….
Karibu tuendelee pale tulipokuwa tumeishia katika fundisho letu. Tuliona mfano mmoja wapo wa Stefano mtu aliyejaa Roho mtakatifu, mtu aliyejaa Neema na uwezo,mtu aliyejaa hekima,
jinsi alivyotamani sana kufanyika raia wa mbinguni maana mtu huyu
aliuona utukufu wa Bwana Mungu pamoja na Bwana Yesu ameketi katika mkono
wa kuume wa Mungu,angali akiwa bado anaishi kama mwanadamu wengine
kabla ya kuuwawa. Tazama hata kifo cha Stephano, Biblia inasema ;
“ wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo
zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli.” Matendo 7 :58
Nguo za Stefano ziliwekwa miguuni mwa Sauli,
Hii ina maana kuwa utumishi aliokuwa nao Stefano uliwekwa miguuni mwa
Sauli ikiwa ni ishara ya kuendeleza upako aliokuwa nao Stefano,
Maana nguo za Stefano zilikuwa sio kama nguo tu za kawaida,Bali
zilikuwa ni Upako/Utumishi aliokabidhiwa Sauli ambaye baadae kidogo
tunamuona anatokewa na Bwana Yesu njiani kisha hata jina lake
linabadilika na kuwa mtumwa wa Kristo Yesu,aliyeitwa kuwa mtume na
kutengwa aihubiri injili ya Mungu.
• Maisha ya mkristo haswa ni maisha ya umilele baada ya maisha haya kupita.
-Mitume wa Bwana Yesu nao ni mfano mzuri wa watumishi waliokubali
kupoteza maisha ya damu na nyama ili kupata uraia wa mbinguni Karibu mitume wote waliuwawa kwa kuishindania Imani, maana waliona maisha haya ya kawaida ni maisha yenye kuharibika tu,hivyo walitamani sana kuvikwa vazi la umilele.
Tazama mfano mmoja pale Herode aliponyoosha mikono yake kuwatenda
mabaya baadhi ya watu wa kanisa Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa
upanga. Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro.
Sasa tazama Bibila inasema katika MATENDO 12:5 “ Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.”
Hawa watu wa kanisa walijawa na ujasiri wa namna yake usioelezeka.Kwa
sababu sio rahisi kwa kukamatwa kwa mwenzao na kuuwawa kwa upanga,
kisha kukamatwa tena mwingine naye akipangiwa kuuwawa kwa upanga,Tena
Kisha wao muda huo huo wakakutana wote na kuaanza kuomba ,
Hii
inamaanisha kuwa hata wao waliona ni afadhali kuuwawa kwa ajili ya
Kristo Yesu na kwa ajili ya injili,maana kilichomfanya Yakobo ndugu yake
Yohana kuuwawa ni injili ya Bwana yesu,na kanisa hawakukoma kuomba
mpaka Petro walipomuona kwa macho yao.
* Jambo moja
tunalojifunza kupitia mitume wa Bwana Yesu ni kwamba walidhalau maisha
haya yasiokuwa na maana kabisa na kutamani sana uraia wa mbinguni.
Mfano wa tatu. Mtazame Paulo ambaye anasema kufa kwake ni faida. Anasema “ Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.” Wafilipi 1: 21
*Tamani sana uraia wa Mbinguni,ambapo kila kitu cha hapa duniani,yaani
vile ambavyo havina utukufu kwa Bwana hivyo utaviona kama mavi,na ndivyo
Paulo alivyoona “ Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa
hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana
wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu
kuwa kama mavi ili nipate Kristo;”Wafilipi 3:8
• Hivyo basi
utagundua kwamba wanafunzi wa Bwana Yesu Kristo,waliteswa na hata
wengine waliuwawa wakiishindania IMANI maana walitamani sana kuishi
pamoja na Mungu Baba Mbinguni. Hawa wote waliona thamani ya maisha ya umilele katika utumishi wao waliokuwa wakiufanya.
• Ndio maana wakailinda IMANI waliyoipokea mara moja tu,kwamba
wasiipoteze,wakaitetea na kuitunza IMANI waliyokuwa nayo mfano wa KITO
CHA THAMANI.
Waliona maisha ya mbele,na wakatiwa nguvu kwa kile walichokiona, Na ndio maana hata Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake mfano wa ufalme wa mbinguni akiufananisha na hazina iliyositirika.
Tunasoma Mathayo 13 :44
“ Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika
shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda
akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.”
Sikia ;
Bwana Yesu,Kitu anachowaambia wanafunzi wake katika andiko hili ni
kwamba ufalme wa mbinguni ni “uraia wa mbinguni”ambao unafanana na
HAZINA iliyofichika. Hazina ya mfano huo,haikufichwa na yeyote Yule bali ilifichika,Tuchukulie mfano mdogo wa maisha haya ya sasa hapa duniani.
Dhahabu na almasi ni moja wapo ya vito vya thamani ambavyo vimefichika katika ardhi.Upatikanaji wa Dhahabu ni wa shida sana. Hivyo Yeye anayetaka hazina ya dhahabu inambidi aache vyote kwa ajili ya kuitafuta kwa moyo mmoja.
Nami nakuambia mtu akiipata dhahabu kamwe hawezi kuiweka hadharani ni
lazima aifiche,Ndivyo ilivyo ufalme wa mbinguni haupatikani kwa urahisi
yatupasa kuiilinda imani kama kito cha thamani…
Comments