TAMANI SANA URAIA WA MBINGUNI.*sehemu ya tatu*

MTUMISHI GASPER MADUMLA


Bwana Yesu asifiwe….

Karibu tuendelee.
…Bwana Mungu ametuandalia makazi ya kudumu huko mbinguni.Ndio maana ninakuambia utamani sana maisha ya Mbinguni,maana ukiweza kuyatamani maisha ya mbinguni basi ni lazima utajitayarisha kiimani,
hata maandiko matakatifu yanatuambia tuwe tayari muda wote,tukimngojea Bwana maana hatujui siku wala saa.( Luka 12:35-36),1 Wathesalonike 5:2

*Uraia wa Mbinguni umewekwa tayari kwa ajili ya watakatifu waliopo hapa hapa Duniani.

*Biblia inathibitisha uwepo wa uraia wa mbinguni.
-Watu wengine wanaweza kudhani kwamba,Uraia wa mbinguni ni maisha ya kufikirika tu.
Kama inge’likuwa ni hivyo, basi hata mimi nisinge’kufundisha mambo haya,sababu ukiona mpaka nakufundisha haya yote ujue kwamba uraia wa mbinguni sio jambo la kufikirika Bali ni jambo lililothibitishwa kimaandiko,
na hapa
tunasoma sasa,;

Wafilipi 3:20;
“ Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; ”

Naipenda tafsiri ya andiko hilo katika lugha ya kiingereza,Ukisoma katika Biblia ya New King James Version (NKJV ) imeandikwa hivi ;
“ For our citizenship is in heaven, from which we also eagerly wait for the Savior, the Lord Jesus Christ,”

Sasa angalia;
Neno “Wenyeji wetu”limetafsiriwa kuwa ni “Our citizenship”
Hivyo neno wenyeji katika andiko hilo ni “ Uraia”.Hivyo mtu mmoja anaweza kusema;
“ Kwa maana sisi, URAIA WETU uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; ” (Wafilipi 3:20)
Badala ya kusema ;
“ Kwa maana sisi, WENYEJI WETU uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; ” Bwana Yesu pia anathibitisha juu ya uwepo wa Uraia wa mbinguni,

Tunasoma Yoh.14 :2-3;
“Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”

Anachokisema Bwana Yesu hapo ni kwamba,anawatambulisha Uwepo wa maisha ya mbinguni,na ndio maana anasema “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi;…”
Tena anasisitiza kwamba kama isingekuwa ni hivyo ange’tuambia,Lakini kwa sababu ni jambo lililothibitishwa kimaandiko ndio maana Bwana Yesu naye anazungumza maneno hayo kwa ujasiri kabisa.

• Huko mbinguni ,kipo kitabu kimoja cha usajiri ambapo majina ya wote waishio huko yameandikwa katika kitabu hicho.
Ikiwa mtu hakusajiriwa katika kitabu hicho hawezi kutambulika kuwa ni raia wa Mbinguni,naye mtu huyo kamwe hawezi kuishi mbinguni kwa sababu jina lake halikuandikwa katika kitabu hicho cha usajiri.

• Mfano :
Tuangalie jambo hili katika mtazamo wa kawaida kabisa,
Tazama katika nchi nyingi leo hii zimeshtuka na kuweka mtazamo wa kuwa na kitabu cha UTAMBULISHO wa raia wake.

*Kitabu cha utambulisho wa uraia kina kazi moja kubwa ya msingi ambayo ni kuwatambulisha wakazi waishio ndani ya inchi husika.
Alikadhalika,Huko mbinguni kipo kitabu kimoja kinachowatambulisha waishio huko mbinguni.Kitabu kinachowatambulisha raia wa mbinguni hujulikana kwa jina la KITABU CHA UZIMA.

*Kitabu cha uzima kipo kwa utambuzi wa watu waishio huko mbinguni,maana kama ikitokea kwamba mtu hajaandikwa katika kitabu hicho,Basi ni dhahili kabisa mtu huyo atatupwa katika ziwa la moto,

Tunasoma Ufunuo 20 : 15.;
“ Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. ”

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments