TAMANI SANA URAIA WA MBINGUNI.*sehemu ya nne*





MTUMISHI WA MUNGU GASPER MADUMLA


Bwana Yesu asifiwe…

Karibu tuendelee pale tulipoishia katika fundisho lililopita;


… Alikadhalika,Huko mbinguni kipo kitabu kimoja kinachowatambulisha waishio huko mbinguni.

Kitabu kinachowatambulisha raia wa mbinguni hujulikana kwa jina la KITABU CHA UZIMA.
Kitabu cha uzima kipo kwa utambuzi wa watu waishio huko mbinguni,maana kama ikitokea kwamba mtu hajaandikwa katika kitabu hicho,Basi ni dhahili kabisa mtu huyo atatupwa katika ziwa la moto,
Tunasoma
Ufunuo 20 : 15.
“ Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto. ”

*Kitabu cha usajiri kinajulikana kwa jina la KITABU CHA UZIMA

Mtu anapookoka tu,kitu cha kwanza ni jina lake linaandikwa katika kitabu cha uzima. Tunaona hata majina ya wana wa Israeli yalikuwa yameandikwa katika kitabu cha UZIMA (Kutoka 32:31-33).

Swali moja lakujiuliza hapo ni hili;

*Kwa nini majina ya Waisraeli yalikuwa yameandikwa,hali Mungu alikuwa akijua watamuasi (Kutoka 32:1-33)?

JIBU;

*Majina ya Waisraeli yalikuwa yameshaandikwa katika kitabu cha Uzima,kwa sababu Wa-Israeli ni wana wa Mungu,ni wazaliwa wa kwanza wake Mungu.

Tunasoma

Kutoka 4 :22
“ Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;”

Hivyo waisraeli walipewa uwezo wa kufanyika WANA WA MUNGU ,ambapo katika uwezo huo majina yao yakaandikwa katika kitabu cha uzima.

Na ndivyo ilivyo kwako wewe ikiwa umeokoka kwamba siku ile ulipookoka tu,ulipewa uwezo wa kufanyika mtoto wa Mungu,

Hii ikiwa na maana kwamba bado hujafanyika mtoto /mwana wa Mungu bali umepewa uwezo tu,Hivyo kadri utakavyodumu katika fundisho la kumtafuta Mungu ndipo unafanyika Mwana.
Sasa tazama Bwana Mungu amwambiavyo Musa kuwa,
“ Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.” Kutoka 32 :33

Ooh,Kumbe ile namna ya kufanyika mwana wa Mungu kwa kuandikwa jina lako katika kitabu cha UZIMA aikugalantii/haikudhamini kufanyika RAIA wa mbinguni

kama ikiwa utatenda dhambi kwa kumuacha Bwana na kushindwa kutubia makosa yako,Ukifanya hivyo hata kama umeokoka ujue kwamba Bwana atafuta jina lako katika kitabu cha UZIMA.

• Jina lako litasalia katika kitabu cha UZIMA endapo Utashinda kwa kuilinda IMANI uliyoipokea mara moja. Maana maandiko yako wazi kabisa juu ya jambo hili.


Tunasoma Ufunuo 3: 5;

“ Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

*Kumbe maovu na dhambi zinatufanya kufutwa majina yetu katika kitabu cha Uzima.


Mpendwa uliye-okoka tafadhali nakuomba urejee kwa Bwana ikiwa umefanya dhambi yoyote,tubu pale pale maana hatujui saa wala siku,

huu ndio wakati wa kufanya toba halisi ili jina lako lisifutwe katika kitabu cha uzima.

*Wakristo wengi hudhania kuwa wanapookoka kisha majina yao kuandikwa katika kitabu cha uzima basi wako salama hata kuishi watakavyo wao na kuanza kujihesabia haki muda wote.


Kumbe! wange’lijua kwamba Mungu aliyeyaandika majina yao baada ya kuokoka tu,ndiye huyo huyo Bwana Mungu awezaye kuyafuta majina yao,

ikiwa kama watamuacha Bwana Mungu.
Sasa hapo utagundua kwamba,leo hii ,wapo watu waliookoka wakidhania kuwa majina yao yameaandikwa katika kitabu cha uzima kumbe yalishafutwa muda mlefu pasipo wao kujijua,Hii ni hatari sana.

*Katika nchi mbali mbali,zimejiwekea taratibu tofauti tofauti za namna ya mtu kufanyika RAIA wa nchi


Mfano;

Wengine,ili mtu awe raia wa nchi Fulani basi ni lazima azaliwe katika nchi hiyo,Au wengine hupata uraia kwa kuoa au kuolewa na raia wa nchi husika,Wengine hupata uraia kwa njia ya KUASIRI,

( mfano wa kufanyika raia kwa njia ya KUASIRI,

chukulia familia ya ndoa ya baba na mama wakiwa wamekosa kupata mtoto katika ndoa yao kwa muda wa miaka mingi sana ,
hivyo wanatafuta mtoto labda kutoka Afrika kisha wanaishi na huyo mtoto kama mtoto wao wa kuzaa,hivyo mtoto huyo akikua mkubwa anajikuta tu ni raia wa nchi hiyo.)

Hivyo kila nchi ina utaratibu wake wa kupata uraia.

*Lakini sivyo hali ilivyo kwa habari ya uraia wa Mbinguni,kwa maana mtu hufanyika kuwa raia wa mbinguni kwa KUZALIWA MARA YA PILI TU,
na hakuna njia nyingine kama ziliozopo katika Dunia.

-Tazama Bwana Yesu akimuambia Nikodemo mambo haya haya ya kuzaliwa mara ya pili ili afanyike raia wa mbingu yaani ili aone Ufalme wa Mungu.


Yoh.3:3

“Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”

ITAENDELEA…

UBARIKIWE.

Comments