TAMANI SANA URAIA WA MBINGUNI.*sehemu ya mwisho*

MTUMISHI GASPER MADUMLA


Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tule pamoja chakula hiki cha kiroho ;
Kumbuka fundisho lililopita,tuliishia kusoma Yohona 3:3
Sasa endelea….

Yoh.3:3
“Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”

-Kwa lugha nyingine Yesu alikuwa akimwambia Nikodemo kwamba , “ Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, HAWEZI KUWA RAIA WA MBINGUNI.”

*Leo ni siku maalumu kwako wewe ambaye bado hujampa Bwana Yesu maisha yako ili awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako.
Ili kwanza jina lako liandikwe katika kitabu cha Uzima pia upate uwezo wa kufanyika raia wa mbinguni.

Unajua Mungu wetu ni Mungu asiyekulazimisha kufanya maamuzi maana hata asema ;
“ Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; ” Kumb.30:19.

Hivyo Bwana Mungu amekuwekea mambo mawili uchague,Yaani uamuzi ni wako ndugu !
Lakini kwa sababu Mungu wetu anatupenda sana kiasi kwamba hataki hata mtu mmoja apotee bali afikilie toba na ndio maana siku ya leo Mungu anakushauri uchague UZIMA,

ili uwe hai wewe na uzao wako,
Uzima anaosema ni UZIMA WA MILELE ambao kwa huo ukiupata,utafanyika LANGO kwa kizazi chako.

*Tamani uraia wa mbinguni kwa kuzaliwa mara ya pili,kwa kuokoka.

Mpendwa,maisha ya hapa Duniani ni ya kupita tu,tupo safarini. Ipo siku hatutakuwepo Duniani kabisa,Sasa nikuulize kwamba;

Je roho yako itakuwa wapi wakati huo?

*Yesu anakualika uende kwake,Umtwike mizigo yako yote,maana yeye ndio Njia,Kweli na Uzima (Yoh.14:6)

• Furaha halisi ya mkristo ni kufanyika Raia wa mbinguni,na ndio maana hata Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa “ Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Luka 10 :20

*Furaha halisi ya mristo sio kuomba sana,sio kufundisha sana,sio kujaa UPAKO ,wala sio kutoa pepo kwa jina la Yesu,Bali ni kuandikwa kwa majina yetu mbinguni.

-Ninapokuambia TAMANI SANA MAISHA YA MBINGUNI nina maanisha UCHUKIE DUNIA NA MAMBO YAKE.

*Mimi sielewi kabisa pale ninapoona mkristo aliyeokoka akishiriki mambo ya Dunia mfano Uvaaji wa nguo za ajabu ajabu na mambo kama hayo.Ya nini ujidhalilishe,kisha uikose mbingu?

Hivyo vinguo,vitakupeleka wapi?
Maana wale wa Dunia wavaapo wanamtumikia baba yao Ibilisi,
wewe Je unapovaa vinguo hivyo unamtumikia mungu au Mungu ( ibilisi au Mungu)?

*Imefika wakati ambapo Dunia ikuige wewe na sio wewe uige Dunia.Wakati huo ndio sasa wa KUTAMANI SANA KUWA RAIA WA MBINGUNI.

Haleluya…
Jina la Bwana liinuliwe…

Tumtizame Mtume PAULO mtu aliye-spend(Aliyetumia)maisha kwa kuliuzi kanisa la Mungu,pale alipokuwa akiitwa SAULI,Ukweli ni kwamba,kama mambo ya dunia aliyafanya zaidi yako wewe.Tazama baada ya kufanywa kuwa mtume anasema ;

“ Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;” Wafilipi 3 :8

*Mambo yote aliyaona kama mavi- kwa ajili ampate KRISTO,

• Mtu huyu Paulo alikuwa akitamani maisha ya umilele,alikuwa ni mtu mwenye SHAUKU ya kweli ,
pamoja na FURAHA kama ile ambayo Bwana Yesu aliyowaambia wanafunzi wake,kwamba ;
“ Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Luka 10 :20

*Tena Paulo anawaambia watenda kazi wenzake hapa;
Wafilipi 4:3;

“ Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.”

*Ukweli ni kwamba miili tuliyonayo ni kama nyumba tu yenye kuharibika,leo ipo,lakini kesho uharibika.

Lakini ipo nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni,nayo wale walionayo miili hiyo ya mbinguni ni wale ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha Uzima cha mwanakondoo,ambao kwanza walimpokea Bwana Yesu kwa KUOKOKA,

pili waliishi na Kristo wakiwa hapa hapa Duniani kwa miili ya damu na nyama,kisha sasa wakafanyika nyumba ya milele,
Tunasoma,
2 Wakorintho 5 :1;

“ Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.”

Wito wangu kwako mpendwa ni,Kuomba neema ya wokovu ikifunike,Ufanye maamuzi ya kumpokea Kristo Yesu ,Uokoke,Kisha uishi maisha ya utakatifu, Maana pasipo huo utakatifu hakuna atakaye muona Bwana( Waebrania 12:14).
*Utakatifu ndio tiketi yenyewe ya kuwa Raia wa mbinguni.

MWISHO.
UBARIKIWE.

Comments