THAMANI YA WATOTO TULIOPEWA NA MUNGU



Mzazi yeyote mwenye hekima, ambaye ametumia maisha yake yote kujenga utajiri mkubwa na kujipatia mali nyingi, kusaidia watu wenye shida na kujipatia heshima kubwa kwenye jamii. Anapofanya maamuzi ya kuwarithisha wanae ile fahari yake, Kamwe hawezi kumpa usimamizi wa mali zake mwana mkaidi, asiye na adabu, asiyejua kuthamini utu wa mwanadamu wala kumjua mungu. siku zote mzazi mwenye hekima humrithisha mwana mwenye mwelekeo kama wa kwake, na kimsingi humuandaa mwana huyu mapema kwa ajili ya majukumu haya makubwa ya kulinda heshima yake.

Kwa mujibu wa Biblia nisomayo, KATIKA ZABURI 127:3 "TAZAMA WANA NDIO URITHI WA BWANA, UZAO WA TUMBO NI THAWABU"

Mungu anapokupa mtoto, anakuwa amekupa zawadi na amekurithisha kitu cha thamani zaidi katika ulimwengu huu. sielewi ni kwa nini sisi wanadamu tunafikiri Mungu anaweza kumpa tu mtu yeyoye vitu vyake vya thamani pasipo kutathminini ni nani mwana mwenye hekima astahiliye kupokea urithi na zawadi hii Muhimu.

Lakini pia sijui ni watu wangapi ambao wanapopata mtoto wanatambua kweli Kiwango cha heshima na dhamana waliyopewa na Mungu. Naamini kama watu wote wangetambua thamani ya mtoto na heshima waliyopewa na Mungu kusingekuwa kile kinachoitwa "mtoto wa mitaani" kwa kwa unayemwita mtoto wa mitaani can as well be the most powerful man on earth miaka ijayo. Unayemwita "Mbwa" kwa kuwa tu umelewa bia ulizokunywa kwa hela za mkopo can as well be the next Bill Gates.

Dada amechezea ujana wake na dunia, akatoa mimba 3, kisha akili ikamjia akatulia akapata jamaa mmoja akamwoa, huyo jamaa naye amechezea ujana wake na dunia akawakana watoto watatu, na kusababisha mimba kutolewa au watoto wakazaliwa lakini wakaishi katika mazingira magumu. Hawa watu wakakosa kupata watoto katika ndoa yao na bado wakawa hawana adabu ya kutafuta rehema za Mungu. Hivi kwa nini tunafikiri Mungu hana feelings? kwamba haimsumbui hata ukichezea kile alichokupa bado anaweza akakupa tu?

Mungu kakupa mtoto mmoja, Unamgeuza kuwa ndiyo sababu ya wewe na maswahiba zako kufanya kufuru zote za ulevi, Ubatizo, Kipaimara, Graduation ya chekechea, zote ni kufuru tupu za ulevi na anasa. Why would God give you another child? ili naye umharibu kwa anasa?

Ikiwa sisi wanadamu tulio waovu, tunathamini sana heshima tuliyojijengea na Jina tulilonalo kiasi kwamba hatuwezi kumrithisha fahari yetu na jina zuli tulilojijengea mwana mkaidi na mpenda anasa. si zaidi sana Mungu?

NINAMUOMBA mUNGU AKUPE KUTAMBUA THAMANI YA WATOTO ALIOKUPA, NA KIWNGI CHA HESHIMA ULIYONAYO MBELE ZAKE HATA AKAKURITHISHA KITU CHA THAMANI NAMNA HIYO.

HII NI KWA WALE WOTE WALIOBARIKIWA KUWA NA WATOTO.

Comments