Posted by
Peter Mabula
- Get link
- X
- Other Apps
![]() |
|
Bwana Yesu asifiwe…
Haleluya…
Kumbuka kwamba tunachoangalia katika fundisho hili ni sababu za msingi
zinazowafanya watumishi au mkristo yeyote Yule kushindwa kufanya kazi ya
Mungu ipasavyo
.Sababu hizo zinazomzuia au kumfanya mtu aliyeyebeba huduma ya Mungu asiweze kuifanya katika viwango vya juu.
Sababu hizi hujulikana kama VIZUIZI au VIKWAZO.
Karibu tuendelee tulipokuwa tumeishia:
Bwana Yesu aliwaambia hivyo kwa sababu maisha yao yalikuwa ni kula na
kunywa muda wote maana wakitumainia uwepo wa Bwana Yesu aliyekuwa
akitembea nao muda wote,Hata kujiuliza kwamba, ya nini kufunga na kuomba
ikiwa Bwana harusi tuko naye ? ndio maana Yesu anawaambia “ [Lakini
namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.] ”
Yaani kwa maneno mengine ni sawa na kusema
“ iliwapasa muishi katika kufunga na kuomba siku zote ”
Na hiyo ndio maana halisi ya mstari huo (Mathayo 17 :21)
• Hivyo kushindwa kuishi maisha ya kufunga na kuomba ni sababu imfanyayo mtu kushindwa kuitimiza kazi ya Bwana kiukamilifu
• Sababu kufunga na kuomba ni mazoezi ya UTAUWA ambayo mazoezi hayo
yanakufanya kutunisha misuli ya kiroho,nayo yanafaa zaidi ya mazoezi ya
kimwili maana imeandikwa ;
“ Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za
mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo
ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.”1 Timotheo 4:8
Kumbuka andiko hili tulilolisoma hapo awali Mathayo 17 :21 “ [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]”
Lenye maana ya kufunga na kuomba kama desturi ya maisha ya Mkristo na
wala sio kufunga na kuomba kwa kusubili tatizo sugu lije ndio ufunge na
kuomba
Au labda kwamba upatapo tatizo ambalo yamkini uliliombea kwa
muda mlefu,pasipo majibu kisha ndio ufunge na kuomba,hiyo sio maana
halisi ya andiko hilo.
• Lakini ifahamike kuwa sio vibaya wala
sio dhambi,wala hajikatazwa kabisa katika Biblia kwamba, endapo utaamua
kufunga na kuomba kwa tatitizo uliloliombea pasipo majibu,nayo ni
sahihi kabisa,ila:
• Wito wangu kwako ni kuishi maisha ya
UTAUWA ya kufunga na kuomba kwanza,maana hata kama tatizo sugu litokeapo
basi utakuwa na nguvu ya kulishinda kiurahisi,tofauti na kuishi maisha
ya kawaida kisha ndipo uanze kufunga na kuomba wakati wa matatizo tu.
Maana ukifanya hivyo yamkini matatizo hayatatoka kwa sababu kiwango
chako cha nguvu juu ya matatizo hayo kitakuwa ni kidogo,na kupelekea
kuomba pasipo kupata majibu. Hautakuwa na nguvu ya kutosha ya kuyashinda
hayo majaribu pindi yajapo.
Haleluya…
Jina la Bwana libarikiwe…
Kushindwa kuishi maisha ya kufunga na kuomba ni kizuizi kikubwa cha
kushindwa kutumika vizuri kwa habari ya mambo ya Mungu.Kiwango chako cha
ujazo wa roho mtakatifu kinategemea mazoezi yako ya kiroho.
Mfano mmoja wapo ambao roho mtakatifu anapotaka kujaa ndani ya roho ya
mtu ni pale mtu huyo anapokuwa anamfanyia Bwana Ibada ya Kufunga na
Kuomba. Tunasoma Luka 4 : 1:
“ Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, ”
Andiko hilo linatupa picha halisi ya namna Roho mtakatifu alipomjaa
Bwana Yesu baada ya Bwana Yesu Kufunga na kuomba huko nyikani.
Bwana
Yesu aliifahamu Siri hii ya ujazo wa roho Mtakatifu,na ndio maana pale
alipojazwa roho mtakatifu mara nyingi alikuwa akifunga na kuomba.
Tazama hata pale kabla ya kuwachagua wanafunzi wake,aliingia katika kufunga na kuomba.
• Ipo siri ya mpenyo katika ibada za kufunga na kuomba.Mfano tunaona
Ibada ya kufunga ilivyowakomboa wakina Esta na akina Mordekai baada ya
kutaka kuuwawa ,iliwabidi kuingia katika kufunga mbele za Bwana maana
ndio ilikuwa njia ya pekee kwao ya kuokoa maisha yao.
Tunasoma Esta 8 :16 :
“16 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, MKAFUNGE
kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana,
nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme,
kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.”
Pia tazama habari za mji wa mkubwa wa NINAWI uliokuwa umejaa dhambi,
Biblia inasema watu hawa wa mji huu waliposikia neno la Mungu kupitia
Yona wote waliiingia katika toba ya Mfungo na kuomba mbele za Bwana,na
kwa njia hiyo ndio ikawa mpenyo wao wasiaangamie kwa hasira ya
Bwana,Naye Bwana akawasamehe maovu yao.
Tunasoma :
Yona 3 :5 “
Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika
nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.”
•
Kumbe tunajifunza neno la msingi hapo ya kuwa, Mungu anaweza kukusamehe
endapo utaingia katika toba halisi ya kufunga na kuomba kwa kumaanisha.
Kwa sababu kwa maombi ya namna hii ,yanakuwa yanamgusa sana Bwana Mungu
wetu,naye huwa tayari kuachilia msamaha kwetu kwa toba ya kufunga na
kuomba.
Yeye aishie katika maisha ya kufunga na kuomba hafilisiki kiimani. Naye muda wote anakuwa ni mshindi zaidi ya mshindi.
ITAENDELEA…
UBARIKIWE.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments