VIZUIZI VYA KUSHINDWA KUFANYA HUDUMA YA MUNGU IPASAVYO.* sehemu ya mwisho*



Mtumishi Gasper Madumla


(Ili kupata mtililiko mzuri wa fundisho hili,tafadhali pitia sehemu zilizopita.Na sehemu hizo zinapatikana hapa hapa haina haja ya kuangaika kutafuta fundisho hili sehemu nyingine. )

Kumbuka kwamba tunachoangalia katika fundisho hili ni sababu za msingi zinazowafanya watumishi au mkristo yeyote Yule kushindwa kufanya kazi ya Mungu ipasavyo.
Sababu hizo zinazomzuia au kumfanya mtu aliyeyebeba huduma ya Mungu isiweze kuifanya katika viwango vya juu hujulikana kama VIZUIZI au VIKWAZO.Basi sasa nianze kwa kukusalimu wewe mpendwa,nikikuambia,

Bwana Yesu asifiwe…
Haleluya…

Andiko letu la kusimamia fundisho hili ni Mathayo 17 :20-21
“ 20 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
21 [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]”

Na tuliangalia kiundani juu ya sababu hizo mbili zinazomfanya mtu kutokufikia kiwango cha juu cha huduma,na mara nyingi kushindwa kabisa kutoa huduma ya ki-Mungu kwa wahitaji,na kwa watu wote wa mataifa.
Mfano kupitia andiko hilo hapo juu (Mathayo 17 :14-21),
tulijifunza jinsi gani wanafunzi wa Bwana Yesu walishindwa kufanya huduma ya kumtoa pepo mchafu Yule kijana aliyepagawa kwa pepo.

Sababu hizo ni ;
• Upungufu wa imani
• Kushindwa kuishi maisha ya kufunga na kuomba.

(Pitia sehemu zilizopita ujifunze zaidi juu ya sababu hizo mbili.)

-Mtu aliyeokoka nina mfananisha na mtu aliyenunua gari nzuri akiwa mtaani kwake. Ambapo mtaani kwake yamkini wanaweza kumcheka kwa kejeli,na kusema kuwa;

“ Eeheee!.. hilo gari lenyewe hata halimpendezi,tena atakuwa anatudanganya tu, kwa kutuambia eti amenunua gari kwa pesa zake! Loh..!
Sababu hana uwezo wa kumiliki gari,
Au hata kama kanunua,gari lenyewe ndio hilo,
hata bure mimi silichukui..!!
Au ni lazima atakuwa amekopeshwa tu,Au kaazima,Au gari litakuwa ni la shemeji yake….n.k ”

Lakini endapo tatizo likitokea kwa gafla hapo mtaani labda tuseme ndio tatizo la kuuguliwa na mtoto wa jirani yake kipindi cha majira ya usiku,
Ni dhahili kabisa,
lazima watamtafuta na kumfuata mtu yule yule waliokuwa wanamsema na gari yake ili awapeleke hospitali kwa matibabu ya mto to wao.

Na kwa sababu mtu huyo ana gari,basi yuko ladhi amchukue mgonjwa na kumpeleka hospitali.
Ni sawa sawa na mtu aliyeokoka.
Ukweli ni kwamba kama kusemwa utasemwa sana kwa sababu ya ulokole wako,
hata mtaani watakubeza kwa maneno ya kejeli,
Lakini siku ikitokea shida ya mgonjwa hata kama ni majira ya usiku,hakika watakuita,nawe kwa sababu umeokoka ,utawasaidia kumuombea mgonjwa.

Sikia;
Ile namna ya wewe kuwasaidia kumuombea mgonjwa na mgonjwa huyo akapata kupona,
Ni sawa sawa na Yule aliyechukua gari yake na kumpeleka mgonjwa hospitalini kwa uponyaji.Maana hata wewe ulipokuwa unamuombea huyo mgonjwa naye akaponywa basi si wewe umponyaye bali ni Yesu aliyemponya,
Bali wewe umetumika tu kama chombo/kama gari la kumpeleka mgonjwa hospitalini,kwa matibabu ya uponyaji,Hospitali hiyo ndio Bwana Yesu ambaye ni daktari bingwa wa mabingwa.

Sasa angalia;
Endapo mtu huyo aliyenunua gari tena pasipo kuifanyia service,kisha akawa anaendelea kuitumia kila siku,kila mwezi,na hata kila mwaka,Mwaka hadi mwaka.
Ni ukweli kwamba gari hiyo itakongo’loka na kuharibika kabisa kiasi kwamba hata kama kuna mgonjwa akijitokeza kwa gafla ili apelekwe hospitalini,
basi mtu huyo atashindwa kulitumia gari hilo,kwa kumpeleka mgonjwa hospitalini.

Tena anaweza kusababisha kifo kwa mgonjwa kwa sababu gari lipo lakini ni bovu,limekosa kufanyiwa services.alikadhalika mtu aliyokoka asipo fanya mazoezi ya kiroho,basi ulokole wake ni bure maana hata ikitokea gafla mgonjwa ni ukweli kwamba atashindwa kumuombea kwa jina la Bwana Yesu na kupata majibu kwa maombi yaliyoomba.

Oooh!Haleluya…
Jina la Bwana liinuliwe sana….

*Kushindwa kufanya mazoezi ya kiroho ni kizuizi /sababu kubwa inayopelekea kushindwa kufanya huduma ya Mungu.

Maana hata maandiko yanatuambia kuwa
“Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.” 1 Timotheo 4 :8

Zipo sababu nyingine ambazo ni kama ukuta wa kushindwa kutekeleza kusudi la Mungu ndani yetu,
Sababu hizo zinaonekana ni ndogo sana kiasi kwamba twazizalau,Lakini mimi leo hii ninakuambia kwamba hakuna jambo dogo mbele za Bwana,maana lile ulidhanialo kuwa ni dogo basi kumbe ndio huwa ni kubwa.

Tuangalie kwa ufupi sababu hizo ambazo ni :
01.Mzaha kwa watumishi wa Mungu
02.Kulizoelea Neno la Mungu.

01.MZAHA
Watumishi wengi wanajikuta hawana upako kwa sababu wameruhusu mizaha katika utumishi wao,maana watu wa namna hii wamesahau kuwa MIZAHA ni dhambi maana Biblia imekataza kabisa mizaha kwa watumishi wa Bwana,Tunasoma
Zab.1:1
“ Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.”

02.KULIZOELEA NENO LA MUNGU.
Ulokole wa zamani unatofautiana sana na ulokole wa sasa. Maana watumishi wengi wa zamani pindi wamuonapo mtu mwenye dhambi mfano mlevi,mzinzi,N.K.Basi utakuta Watumishi/Mtumishi hulia sana maana hata kabla hajamuombea anajisikia kuugua moyoni mwake juu ya dhambi za Yule mtu.

Leo hali hii iko tofauti sana na maisha ya ulokole wa sasa maana mtu mlokole ambaye ni mtumishi hata amuonapo mtu mwenye dhambi kupitiliza,mtumishi huyo utamuona yuko tayari kumuacha aangamie na dhambi zake.

Kwa hali hii inaonesha kuwa neno la Bwana haliko ndani ya watumishi kwa sababu ya kulizoelea Neno la Mungu.
Biblia inasema ;
“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. ”Waebrania 4 :12

Kama tutafahamu hayo ya kuwa neno la Bwana lina nguvu iokowayo,basi kamwe hatuta tamani kuishi kama watu wa mataifa.

MWISHO
UBARIKIWE.

Comments