YESU YUPO KAZINI, ANAMTAFUTA MMOJA TU, AABUDUYE KATIKA ROHO NA KWELI.


21. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. 23Lakini saa inakuja, nayo saa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba Katika Roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.24. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo, imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli.Yesu akamwambia, Mimi ninayesmea nawe, ndiye. (Yohana 4:21-25).

Ndugu, Neno hilo likufundishe jambo jipya siku ya leo, Mungu hamtafuti Mkristo Jina wala hamtafuti mtu wa Dini. Hamtafuti Mtu wa dhehebu flani au flani, ila anamtafuta mmoja tu, amwabuduye katika Roho na kweli, huyo ndiye Yesu alikuja kwaajili yake.

Yesu hajaja kwaajili ya TAG, EAGT, AIC, ACT, PHM, EFATHA, ELSHADDAI,EMAU, FPCT, CATHORIC,LUTHERAN, MORAVIAN wala sujui nini! Acha kupoteza Muda kueneza Dini, mweneze Yesu, achana na tabia hiyo ya kusimama na Kanisa pembeni, hakuna mbingu ya Dhehebu wala Dini, ila ipo mbingu ya waabuduo katika Roho na kweli.
Hata ukijiita jina zuri kivipi, hata ukijiita KANISA LA YEHOVA, YESU, SIJUI MARIA, IBRAHIMU,YAKOBO,YERUSALEM, haisaidii, wewe mtafute Mungu katika Roho na kweli. SAA IPO UTAKAYO MWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI, WALA DHEHEBU LAKO NA MCHUNGAJI WAKO HAWATA KUWEPO. SIJUI ASKOFU SIJUI SHEMASI, MWALIMU WAKO NA NABII, HAWATAKUWEPO, KILA MTU ATAKUWA ANAMTAFUTA MUNGU KIVYAKE.

JIFUNZE KUMTAFUTA MUNGU KWA ROHO NA KWELI......MUNGU ATUSAIDIE.

Comments