ANDAA MOYO WAKO ILI JAWABU LAKO LITOKE KWA BWANA.*sehemu ya kwanza *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…

Mithali 16 :1,
Katika andiko hilo tunaona moyo umetajwa,kama inavyofahamika kuwa moyo ni kiungo cha muhimu sana katika maisha ya kiumbe hai.

Maisha ya mwanadamu yamefichwa katika moyo,maana hakuna uhai pasipo moyo kuwapo.
Endapo moyo wa mwanadamu ukisimama kufanya kazi yake,basi ni dhahili kabisa na maisha ya mwanadamu huyo husimama,yaani hufa.

*Lakini moyo unaozungumziwa hapo katika andiko,huwakilisha roho.Na wala sio moyo kama moyo wa mwanadamu.
Kwa sababu moyo kama kiungo kingine katika mwili wa mwanadamu,hakiwezi kumuandaa mwanadamu ili apokeee jawabu kuotoka kwa Bwana.

*Hivyo basi mtu anaposema maandalio ya moyo ni ya mwanadamu ni sawa na kusema maandalio ya roho ni ya mwanadamu.
Labda tuangalie mfano mmoja wa andiko lenye kufanana na hiki nikisemacho.
Warumi 10:10;
“ Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”

-Kinachozungumziwa katika andiko hilo ni kwamba, roho ya mtu ndio huamini hata kupata haki,kwa sababu IMANI ni tendo la rohoni.Hivyo moyo kama kiungo cha mwili hakina uwezo wa kuamini hata kupata haki.

*Neno maandalio, maana yake ni maandalizi(The preparations )
Hivyo basi mwanadamu amepewa jukumu la kuandaa roho yake. Kwa msaada wa roho mtakatifu.

Kwa maana hiyo basi, jawabu la Bwana huja baada ya maandalio ya moyo wa mtu kufanyika kiukamilifu.
Kumbe!
kosa letu moja tunalolifanya kila siku wakati wa maombi linalopelekea tusipokee majibu yetu kwa wakati sahihi wa Bwana ni kushindwa kuuandaa roho zetu.

Mtu anapouandaa moyo wake/anapo-andaa roho yake, jawabu la ulimi kwa kile alichokiomba hutoka kwa Bwana

• Hakuna kazi iliyo ngumu Duniani kama kazi ya kuandaa roho ya mwanadamu,ili kusudi jawabu la Bwana lije.

Kwa sababu ipo gharama ya kufanya maandalizi ya moyo.
Moyo ukifanyiwa maandalizi ya kutosha,ujue neno la Bwana litapata nafasi ndani ya moyo huo,na kuluhusu jawabu la Bwana kupitia ulimi wa mtu mwenye moyo huo.

Kutoka 3;3-4 ;
“Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.”

Kilichofanyika hapo katika hilo andiko ni kwamba;
Bwana Mungu alikuwa akiuandaa moyo wa Musa ili neno lake Mungu lipate nafasi ndani ya Musa.Ndio maana tunaona Bwana akamfanyia kitu cha kumshang’aza Musa kusudi aweze kumsikilizisha neno lake,

Biblia inatuambia;
“ Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.”Kutoka 3:4

*Ilikuwa sio rahisi kwa Musa kuweza kusikia neno la Mungu kwa wakati ule,ndio maana tunaona Mungu akitumia njia mbadala ya kumuweka sawa kwa kukiwasha kijiti cha moto pasipo kuungua.

Kisha sasa neno la Mungu likapata nafasi likamtuma ,Musa arudi kwa Farao ili awaokoe ndugu zake.

*Hayo yote yalikuwa ni maandalizi ya moyo wa Musa.Lakini wakati wa sasa hali ni tofauti kabisa kwa maana Bwana ameachilia NEEMA yake ya pekee kwamba wewe umwendeaye Mungu ,yakupasa uandae moyo wako.

ITAENDELEA...

Comments