ANDAA MOYO WAKO ILI JAWABU LAKO LITOKE KWA BWANA.*sehemu ya pili *

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Karibu mpendwa katika Kristo tuendelee kujifunza siri za Ufalme wa Mungu,Tunaendelea tulipokuwa tumeishia...

...Sawa sawa na neno la Mungu katika Zaburi 111:2 ;
“ Matendo ya Bwana ni makuu,
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.”

*Biblia inasema kwamba ,
wale wanaopendezwa na Bwana huyafikiri sana matendo ya Bwana,
Hii ikiwa na maana kwamba ,
Wale wanaopendezwa na Bwana HUYASOMA /HUJIFUNZA kupitia matendo makuu ya Bwana.

*Hivyo kumbe ipo shule ya kujifunza kupitia matendo makuu ya Bwana.
Nalipenda andiko hilo katika tafsiri ya New King James Version(NKJV),
Imeandikwa hivi;
“ The works of the LORD are great, STUDIED by all who have pleasure in them.” Zaburi 111:2(Psalms 111:2)

Ndio maana hata Musa ilimbidi aingie shule ya kusoma matendo makuu ya Bwana pale alipoona mwali wa moto katikati ya kijiti kisicho teketea.
Na baada ya hapo tunaona Mungu anampa agizo la kurudi kwa FARAO kwa ajili ya kuwakomboa ndugu zake.

*Wale ambao wamefanya maandalizi ya roho zao,hupewa maneno ya kusema katikati ya mbwa mwitu,maana si wao ,

Mathayo 10:19-20
“ Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.”

*Watu wa namna hii wasio fikiri-fikiri jinsi watakavyosema kati ya watu wa mataifa,ni watu walio ndani ya Kristo ambao wanaongozwa na Roho wa Mungu/Roho mtakatifu,
Hivyo watu wa namna hiyo ni watoto wa Mungu

“ Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.” Warumi 8:14

*Mwanadamu amepewa jukumu la kuandaa roho yake kwa njia ya ;

01.TOBA
*Mungu hapendi mtu yeyote apotee bali afikilie toba,kwa maana palipo na msamaha kunakuachiliwa kutoka katika vifungo.
“Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.” 2 Petro 3 :9

Nasema hivi,kupitia toba halisi kuna uponyaji wa kipekee katika moyo wa mtu,kwa sababu TOBA ni moja ya maandalizi ya wa MOYO/ROHO ya mwanadamu kusudi jawabu la Bwana liachiliwe.

Tunasoma ;
Zaburi 103:3
“ Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,”

*Ili Bwana akusamehe inakubidi wewe mwenyewe uamue kuomba msamaha kwake,
Yaani uchukue jukumu la kutubu.Kupitia toba hiyo magojwa nayo huondoka
Kwa sababu magonjwa mengi ni dalili ya dhambi.
Dhambi ni kichaka cha magonjwa mengi.

Note.
*Sisemi kwamba kila mwenye magonjwa ametenda dhambi,la hasha!
Kwa maana wapo wengine wenye kupitishwa katika majaribu kwa njia ya magonjwa,
Mfano Ayubu mtumishi wa Mungu aliye mkamilifu.Yeye Ayubu hakupata magonjwa kwa sababu alimtenda Bwana Dhambi,Bali kwake ilikuwa kama mtihani (Soma Ayubu 2:6-7)

*Toba ni kujisalimisha mbele za Bwana kwa kuomba msamaha kwa KUJITIA DHAMBI ZOTE kwa lengo la kuziacha na kumgeukia Mungu.

*Toba ni kuzingatia moyoni mwako kuacha dhambi kwa msaada wa Roho mtakatifu,ukisihi huruma za Bwana ziachiliwe kwako,ili uwe safi.

ITAENDELEA
UBARIKIWE.

Comments