“ANGALIENI,MIMI NAWATUMA KAMA KONDOO KATI YA MBWA-MWITU”(Mathayo10 :16) *Sehemu ya pili*

Mtumishi Gasper Madumla


BwanaYesu asifiwe….

Katika andiko hilo tunaona wanyama wanne wakizungumziwa ,yaani;
01.Kondoo.
02.Mbwa-mwitu.
03.Nyoka.
04.Hua.

Katika wanyama hao wanne sisi tumefananishwa na Kondoo.
*Kondoo,wanawakilisha wale waliotumwa na Bwana Yesu kwa ajili ya kazi yake ya injili.Luka 10:3
*Mbwa-mwitu wanawakilisha wana wa uovu.
Ekekieli 22-27
“ Wakuu wake kati yake wamekuwa kama mbwa-mwitu wakirarua mawindo; ili kumwaga damu, na kuharibu roho za watu, wapate faida kwa njia isiyo halali.”

Matendo 20: 29;
“ Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi;”

*Nyoka anawakilisha ujanja/welevu.
Mwanzo 3 :1 “ Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?”

*HUA anawakilisha amani,mwenye upendo na asiyedhuru.
Mathayo 3 :16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

*Sasa,Bwana Yesu anatufananisha kama kondoo kati ya mbwa-mwitu,kwa sababu hizi zifuatazo;
01.Kwanza ,KONDOO,
hana maamuzi yake binafsi,Hutegemea sana maamuzi ya mchungaji wake.
Mfano ,Ukimchukua kondoo yule anayefugwa kisha ukamuuacha mahali fulani,
alafu labda ukaodoka,ujue kwamba ukirudi utamkuta mahali pale pale ulipomuacha.

Kwa sababu yeye muda wote hukaa akitegemea mchungaji amuongoze.Tabia hii ni tabia iliyokuwa ya tofauti kabisa na baadhi ya wanyama wengine.
Karibia Wanyama wote hufanya maamuzi ya haraka wao wenyewe,

mfano kuku na baadhi ya wanyama wengine ambao mara nyingi uamua mambo yao wenyewe,tazama sasa,
Kuku ukimuacha sehemu fulani kisha ukaondoka ujue yeye pia ataondoka tu katika ile sehemu ile uliyomuacha,hata kwa ng’ombe na wengine hufanana kwa tabia hiyo ya kujiamulia wao wenyewe. Lakini sivyo kwa habari ya kondoo,kondoo umfuata mchungaji wake.

Sikia;
*Siku ya leo Bwana Yesu anatufananisha sisi kama watu wenye tabia hiyo ya kondoo,tuwe ni watu tusiokuwa na maamuzi yetu wenyewe ,
tukitegemea sana kuongozwa na Yeye Ambaye Yeye ndio kichwa,

Wakolosai 1:18 ;
“ Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.”
Tena,
Yeye Bwana Yesu ndie mchungaji.Tazama hata DAUDI aliitambua siri hii akasema ;
“ Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.” Zaburi 23 :1-2

Daudi anaposema “ Bwana huniongoza”Ana maanisha kwamba ;
yeye mwenyewe Daudi hana uwezo wa kijiongoza mwenyewe,Hana maamuzi yoyote yale ya kujiongoza.

Daudi anatupa mfano mzuri wa KONDOO.
Kwa lugha nyingine Kondoo ni Yule anayemtegemea Bwana katika mambo yake yote.
Nasema mambo yake yote maana yeye mwenyewe hana maamuzi yake binafsi.Na ndio maana hata Paulo naye akasema ;
“Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Wafilipi 4 :13.

*Kondoo anachungika chini ya mchungaji mmoja.
-Kondoo anayo tabia ya kuchungika chini ya mchungaji mmoja,Hivyo basi ikiwa anaweza kuchungika basi pia anaweza kuisikia sauti ya mchungaji wake.
Mfano jaribu kuwachukua kondoo ambao wewe sio mchungaji wao,kisha ujaribu tena kuwaita kwamba waje ,wakufuate.

Mimi nina kuambia hawatakuja maana wenyewe wanaijua sauti ya mchungaji wao.Hivyo basi kondoo huweza kumjua mchungaji wao,na mchungaji wao huwajua kondoo zake,

Tunasoma Yoh 10 :14
“Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;”

Bwana Yesu anatutuma kama kondoo kwa sababu Kondoo amepewa uwezo wa kuishi katika mazingira magumu tofauti na ng’ombe.
Mfano Kondoo anaweza kuishi au kufugwa katika mazingira magumu ya ukame au maradhi,pasipo kumkimbia Mchungaji wake.

katika tabia hii,tunajifunza jambo moja kubwa kwa habari ya uvumilivu,kwamba hata kama njaa ijapo,au maradhi yajapo kwako,yakupasa uvumilie tu,maana kumbuka wewe umetumwa kati ya mbwa –mwitu,kwamba endapo utashindwa kustahimili njaa,au maradhi yajapo,

basi kwa kufanya hivyo utakuwa umempa nafasi mbwa-mwitu kukudhuru.Katika uvumilivu,yatupasa tusitengwe na upendo wa Kristo kwa kitu chochote kile kijacho.Na ndio maana Paulo akauliza kuwa ;

“ Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? ” Warumi 8 :35

ITAENDELEA…
UBARIKIWE.

Comments