“ANGALIENI,MIMI NAWATUMA KAMA KONDOO KATI YA MBWA-MWITU”(Mathayo10 :16) *Sehemu ya mwisho*



 Na Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe….

Ninakukaribisha tuendelee kujifunza katika sehemu ya mwisho ya Fundisho hili zuri,
Katika andiko hilo hapo juu (Mathayo 10:16)
Tunafananishwa kama kondoo kati ya mbwa mwitu,ikiwa na maana kuwa ;

*Kondoo anao uwezo wa kuisikia sauti ya bwana wake na kuitii pindi anapochungwa.

-Leo Bwana Yesu anatutaka tuweze kuisikia sauti yake na kuiitii tukiwa kati ya mbwa-mwitu,hii ina maana kwamba wenyewe hatuna uwezo wa kupigana na mbwa-mwitu kisha tukawashinda pasipo kuisikia sauti ya Bwana.

*Maana siku zote yeye asikiaye sauti ya Bwana ni mtendaji wa kile alichokisikia.
*Mkristo asiyesikia sauti ya mchungaji wake basi yeye siye kuondoo,Bali kondoo ni Yule asikiaye sauti ya mchungaji wake.

Kondoo asiyesikia sauti ya Bwana sio mtiifu,tazama mfano wa Sauli aliposhindwa kuisikia sauti ya Bwana akakosa UTII,
Ndipo Samweli akasema;
“ Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia,KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.” 1 Samweli 15 : 22

*Hivyo basi tuna pofananishwa na kondoo,tuna fananishwa na watu tusiokuwa na uwezo wetu wenyewe wa kupambana na mbwa –mwitu tena hapo sasa ndipo tunahitaji mchungaji wetu ili atushindie tupiganapo na mbwa-mwitu.Lakini kwanza tuweze kuwa watii wa sauti yake.

Tazama hata mchungaji wetu ambaye ndie Kristo namna alivyokuwa mtii naam mtii hata mauti ya msalaba,
Waefeso 2:8
“ tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.”

*Kondoo yoyote Yule aliyekuwa msikivu,ni lazima atakuwa mnyenyekevu,kisha hapo ndipo kuna maisha ya ushindi dhidi ya mbwa-mwitu.

Haleluya…

Sikia;
• Dunia ya leo wapo mbwa-mwitu,kwa dhumuni la kuharibu kile kitu cha ki-Mungu ndani yako wewe uliye kondoo,Wapo kwa ajili ya kutolihurumia kundi (Matendo 20:29)

• .Uwepo wa mbwa-mwitu ni mzuri kabisa kwa maana kupitia hao ndipo jina la Bwana linatukuzwa.Mbwa-mwitu ni wakali hawana kusamehe kabisa lengo lao pia ni kumwaga damu,
lakini kupitia wao sisi ndio tunavuka.Mfano Wamisri walikuwa kama mbwa-mwitu kwa Waisraeli,
Sasa tazama uwepo wa Wamisri ulivyowafanya kuvuka bahari ya shamu,maana ni ukweli kabisa pasipo wale wamisri kuwafuatia kwa nyuma hawa Waisraeli wasing’evuka bahari ya shamu.

Lakini ile namna ya uwepo wa mbwa-mwitu uliwafanya waokoke,Mimi sijui leo hii wewe unapitia kati ya mbwa-mwitu wa namna gani?
Huyo mbwa-mwitu uliyekuwa naye yupo kwa ajili ya wewe uvuke hapo ulipo.Hivyo yatupasa hata kumshukuru Mungu kwa ajili ya uwepo wa mbwa-mwitu katika maisha yetu ya kila siku,
kwa maana wana tuimarisha kiimani hata kusonga mbele.

Kumbuka;
Tumeambiwa tuwe na busara kama NYOKA.
*Ikiwa na maana kuwa ,anatuambia tuwe na ujanja wa kufahamu pindi tuwapo kati ya mbwa-mwitu.Maana tukishindwa kuwa na ujanja wa ufahamu hakika tutashambuliwa na mbwa-mwitu.

*Ujanja wa ufahamu ni ule wa kuelewa kile asemacho Bwana,maana ikiwa kama hatutaelewa nacho basi ni dhahili kabisa adui huja na kukinyakua pale kilipopandwa.
Mathayo 13 :19 ;
“ Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”

*Kushindwa kuelewa mambo ya ufalme wa Mungu ni silaha ya maangamizi ya adui wetu anayoitumia.Maana adui wa kwanza wa mkristo sio shetani bali ni KUSHINDWA KUELEWA SIRI ZA UFALME WA MUNGU,
ndipo shetani huja na kuchukua nafasi kwa yule asiyeelewa habari za Mungu.Lakini shetani hana nafasi kabisa kwa yule mwenye kuzijua siri za ufalme wa Mungu.

Iweni wapole kama HUA.
-hapa sasa anatutaka tuwe watu wenye amani,watu tusiodhuru wengine iwe kwa maneno ,au hata matendo yetu.
*Ni kweli tupo kati ya mataifa,
lakini yatupasa tusiwe watu wa kuwaumiza kwa maneno machafu au kuwafanyia vitendo vichafu,BALI YATUPASA KUWACHUKULIA KAMA BINADAMU WENGINE maana hata sisi tulikuwa kama wao,

-lakini tukaokolewa kwa neema tu ya Bwana.Maana kama si Bwana na useme sasa ! Yatupasa kusema nao kwa utaratibu kwa maana ipo siku ya Bwana iliyokusudiwa ambayo wao wataokoka kupitia upendo uliopo ndani yetu.

MWISHO…
UBARIKIWE.

Comments