BINTI ARUDISHWA KUTOKA BAHARI YA ATLANTIC.

Photo: BINTI ARUDISHWA KUTOKA BAHARI YA ATLANTIC.

Jumapili hii ya tarehe 13.7.2013 imekuwa ya miujiza sana katika kanisa la Ufufuo na Uzima - Morogoro lililo chini ya Mchungaji Kiongozi, Dr Godson Issa Zacharia. 

Ujumbe unaohusu Matukio ya Kichawi ndio uliokuwa moto kamili wa kuwafuata wote ambao, kwa matukio hayo waliwekwa katika vifungo vya shetani. Na kufanya miujiza isiyokuwa ya kawaida kufanyika siku hiyo ya jumapili.

Jambo Moja wapo lililotokea ninkurudishwa kwa binti ambaye alikuwa katikati ya bahari ya Atlantic katika ulimwengu wa roho. Akielezea ushuhuda huo, binti huyo aitwaye Jackline alisema kuwa, "yeye alichukuliwa na kuwekwa katika bahari ya Atlantic kama malkia wa mfalme wa giza (Efe 6:12), ingawa duniani mwili wake ulikuwepo, hakuwa yeye bali ni roho ya mtu aliyekufa zamani ndani ya bahari hiyo ndiyo iliyokuwa ikitenda kazi ndani ya mwili wake."

Akiendelea kusimulia Jackline alisema, ndani ya mwili wake aliwekwa mtu ambaye alikufa baharini hapo zamani, aitwaye Nataria, lakini yeye (roho yake) hakuwemo ndani ya mwili wake. Huyo nataria aliutumia vibaya mwili wa Jackline, ili kutimiza mission au mikakati ya huyo mfalme wa giza aliyeko baharini.

Akiwa baharini alizaa mtoto wa rohoni aitwaye Adrian. Jackline akashuhudia kuwa jumapili hii, akiwa baharini; aliona mtu mweupe amemfuata kule, alishangaa kwa kuwa si kawaida kumuona mtu mweupe kuzimu. Mtu huyo mweupe, alimwangamiza yule mfalme wa kule baharini, ambaye alisikika akipiga kelele kutaka asinyang'anywe malkia wake. Baada ya muda Jackline akajikuta yupo kanisani, njia panda ya Veta - Morogoro, Kihonda. 

Bahati nzuri, kumbe mama yake naye alikuwepo kanisani siku ya jumapili ikiwa ni mara yake ya kwanza kuhuduria ibada pale, alisema kuwa Walikuwa wanamshangaa Jackline, maana alikuwa anazimia hata wiki nzima mara kadhaa shuleni na nyumbani. Jambo ambalo lilimpelekea kufikia kuacha shule aliyokuwa anasoma yaani Kigurunyembe Secondary School. Mama yake akiendelea alisema kuwa siku nyingine alikuwa anazimia hata wiki nzima bila kula wala kunywa ila hafi, kumbe ndani ya mwili wake alikuwa anaishi Natalia, aliyekufa kwa ajali baharini hapo zamani.

Ashukuruwe Mungu baada ya kurudishwa sasa Jackline anaendelea na shule, na Mch. Godson akamtamkia neno la kinabii kuwa atasoma na kufanikiwa katika maisha yake.

MUNGU WETU NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTINI ZINA YEYE.
Jackline akitoa ushuda kanisani ufufuo na uzima morogoro na pembeni yake ni Mchungaji Kiongozi  Dr Godson Issa Zacharia.

Comments