
Jina langu ni Sifa John. Nilizaliwa katika familia ya kiislamu na ni mtoto wa tano kuzaliwa ila
kwa upande wa mama mimi ni mtoto wa pili, na wa kwanza alifariki ambaye alikua
anaitwa Mwamvita. Nikiwa muislam nilikua naitwa Tiba Hamadi na baada ya kuokoka
siku ambayo nilibatizwa ndipo nikapewa jina la Sifa, na baada ya kuolewa
nikawa naitwa Sifa John(John ni Jina la Mume wangu). Baba yangu alitengana na mama yangu baada ya mama kurudi
kwenye dini yake awali ya kikristo alikotokea kabla ya kuslim na kuolewa na
baba. Baada ya mama kuondoka, baba yangu alioa mke mwengine na ambaye ndiye aliendelea kunilea baada ya
kuachwa na mama.
Nilikaa kwa baba yangu mda mrefu bila kumjua mamaangu
kwa sababu aliniacha nikiwa mdogo sana mana nilikua na miaka miwili tu,
na
baada ya kufikisha miaka kumi na nne nilikutana na mkutano wa injili
hivyo
nikaokoka kupitia mkutano huo. Ugomvi wangu na babaangu mzazi ulianzia
hapo. Baba
alikasirika sana na akanitenga kabisa na akakataa kuniendeleza
kimasomo, na aliniambia hata akifa nisifike na mimi nikifa hatofika
kwenye Mazishi. Lakini pamoja na yote baba yangu ananipenda sanaaaaana.
na niliwahi
kupata ajali ya mguu, mfupa ukakatika mara mbili na kupishana ikawa
kwamba
nikatwe mguu. Baba yangu alikua analia sanaaa kila akija hospitali.
Madaktari walikua wakimtoa nje mara kwa mara kwajili ya kulia, lakini alipambana kiume
na kukwangua acount yake yote ili mimi nisikatwe mguu, mana aliambiwa kwamba
ili nipone dawa inatakiwa iagizwe Ufaransa. Baba hakusita juu ya hilo kwani
dawa iliagizwa hivyo nikatibiwa mpaka sasa nina miguu yote miwili. Hii yote ni kwaajili
ya upendo wa baba yangu, hata mimi nampenda sanaaa baba yangu, lakini
ninachomshukuru Mungu baba yangu amerejeza Moyo na sasa tunaishi nae kwa
upendo sanaaa.
HISTORIA YAKE KIUIMBAJI
Nilianza huduma ya uimbaji Mwaka 1983 katika kwaya moja ya kanisa la
Mchungaji Lukindo Kawe, na wakati huo nilikua nasoma Shule ya Msingi
Kawe
darasa la 4. Badae niliimba kwaya ya Yerusalem ya kanisa la Pentecoste
Kawe-Mbezi kwa Mchungaji Kibingu Marandura ambae kwa sasa ni
marehemu.Nipoolewa nilianza kuimba kwaya ya kanisa la EAGT Imani Choir
ambayo ilikua chini ya kanisa la Mch. Ernesti Nyanda aliyekuwa Waziri wa
Mawasiliano na Uchukuzi, na hapo nilikua Sololist niliyevuma sana na
wimbo wa Kigeugeu. Hiyo ilikuwa ni katika mkoa wa Mwanza.
Badae nilichukuliwa na Kwaya
ya Calvary EAGT Nyamanoro kwa Mch Kapera nikiwa Sololist na nilivuma sana
kwa wimbo wa Malaika katika Kanisa la Efeso. Hapo sasa nilipata mtu mmoja
anaitwa Gahutu akanidhamini nikatoa Album yangu ya kwanza ya Wateule Tutakwenda. Kwa sasa nimetoa album yangu ya pili ujulikanayo kama Usililie
Moyoni Yupo Mungu.

Namshukuru sana Mungu ananipigania sana katika
huduma hii mana nimekuwa nikisafiri huku na huko kwa ajili ya huduma na ananilinda
sana. Pia kupitia huduma ya uimbaji nimefanikiwa kuanzisha huduma ya
kusaidia watoto yatima na watoto waishio katika mazingira magumu. Pia
ninao vijana ambao walikua wamekata tamaa tunaowapa mafunzo mbali
mbali kama kushona, uigizaji, na computer.
Watoto hao nilionao
wanapata misaada mbali mbali kama vile elimu mana kuna walimu wanawafundisha
hapo kituoni mana walikua hawajawahi kusoma kwajili ya matatizo na shida walizonazo na kukosa msaada.

Comments