JAMBO LINALOLAZIMISHWA KUWEPO KWENYE MAISHA YA MTU BILA RIDHAA YA MHUSIKA(sehemu ya 1)

Na mwl  Ernest Mbuya 


 


Ni kitendo cha kushindwa; ni kukosa ,anguko la aibu,ni tunda linalolazimishwa kuwepo kwenye maisha ya mtu bila ridhaa yake mhusika.

Kushindwa ni kuanza vizuri na kumaliza vibaya.

Kushindwa ni kuanza na kuishia njiani.

Kushindwa ni kuonekana unakimbia lakini huonekani ukimaliza.

Kushindwa ni kuonekana unasoma lakini huonekani ukimaliza.

Kushindwa ni kuonekana unatenda jambo hilo hilo lakini huonekani ukimaliza.

Kushindwa ni nguvu na matokeo mabaya yasiyoshikika kwa mikono lakini umbo la kushindwa huonekana kwa macho.

Kushindwa ni nguvu isiyoshikika kwa mikono lakini umbo lake ni nguvu yenye uvumi unaosikika kwa masikio.

Hali ya kushindwa haiji tu bali husababishwa na huchochewa kama moto.

Yapo masababisho makuu ya kushindwa.

Usipomgundua huyo msababishaji hutakaa ushinde kamwe.

Wakristo wanapambana na matokeo ya kushindwa na sio msababishaji wa kushindwa.

Huwezi kulishinda hili jitu endapo huna ufahamu wa juu ya ukombozi.
Jitu la kushindwa huishi ndani ya mtu na kufanyakazi zake za kushindwa kupitia hati za utambulisho wako.
Kol 2:13-14
Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

Ndio maana hata kama tutakuwa tumekodisha timu ya washauri kutoka eneo lolote lenye washauri bingwa.Mtu mwenye shida ya kushindwa bado hatasaidika.
Hata kama tutakodisha waombaji bingwa wa maombi kuja kuendesha maombi.Bado mwenyeshida ya kushindwa hawezi kuwa huru.

Ndio maana ushahuru wa mwisho wa mtu anayeteshwa napepo ni huu:-
1.AWE CHINI YA NENO LA MUNGU.
Kwa sababu kila siku na kila mara aomapo na kufundishwa neon pekee ndilo linaloweza kujipenyeza sehemu yenye hati.
Kol 3:16
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Zaburi 119:144
Haki ya shuhuda zako ni ya milele, Unifahamishe, nami nitaishi.

Mathayo 28:19-20
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Matendo Mitume 2:42
Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

Yohane 8:31-32
Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Hawa wanaofanya ukombozi bila mafundisho ya Neno , hakuna wanachokifanya.
Ebr 4:12-16
Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

2.UGUNDUZI
Ukombozi si maombize au ushauri tu ukombozi ni safari ya ugunduzi na muhusika.
Ezek 16:2-5
Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa. Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa.

Huwezi kwenda popote na kumwambia mtu nimekuja unifanyie ukombozi.
Hata kama umeokoka unaweza kuwa chini ya mapepo hadi unapogundua chanzo cha mateso yako.
Luka 15:14-20
Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.
Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana.

Huwezi kushindwa kabla hujagundua chanzo cha kwanini nishindwe.
Kazini huwezi kudumu.
Kwenye kanisa zuri huwezi kudumu.
Kwenye kuaminika huwezi kudumu.
Kwenye uongozi huwezi kudumu.

Inawezekan tatizo lako wewe ni muingiliano wa vitu vinavyokuhusu.

Endapo wewe una uzoefu wa kuingilia mambo ya watu, hutadumu kwenye hiyo ofisi.
II Sam 17:23
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.

Lipo jitu lililolala ndani yak oleo halionekani hadi utakapopata ofisi au nafasi ndipo linainuka.
II Sam 5:17-18,vs 22
Na hao Wafilisti waliposikia kwamba wamemtia Daudi mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akapata habari, akashuka akaenda ngomeni. Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai.
Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai.

Ili kuizima sauti yako isisikike kabisa kwenye mlima wowote.
II Sam 8:13
Basi Daudi akajipatia jina, aliporudi kutoka kuwapiga Waedomi katika Bonde la Chumvi, watu kumi na nane elfu.
Ezek 19:8-9
Ndipo mataifa wakajipanga juu yake pande zote toka nchi zote; wakaunda wavu wao juu yake; akanaswa katika rima lao.Wakamtia katika tundu kwa kulabu, wakamleta kwa mfalme wa Babeli wakamtia ndani ya ngome, sauti yake isisikiwe tena juu

3.SHUGHULIKIA TATIZO HUSIKA.
Baada ya kugundua tatizo lazima ulishughulikie hadi liishe kabisa.

Mungu alishughulikia tatizo pale Edeni hasdi likamalizika kabisa.
Mwanzo 3:8-13
Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.

Mwanadamu yeye alilificha tatizo bila kulishughulikia.
Shughulikia tatizo hadi ulimalize kabisa
Linyokee na duma kwenye hilo tu.
II Falme 2:19-22
Watu wa mjini wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akasema, Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.

Hutaponywa hadi ukibainisha wazi , fichua tatizo lako ndipo utapata ufumbuzi wako hilo ndio jitu linalokusumbua kwa ndani.
II Falme 6:3-7
lisha akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha, Basi wakashuka mpaka Betheli. Basi wana wa manabii, waliokuwako Betheli, wakatoka kuonana na Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akasema, Naam, najua; nyamazeni. Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana Bwana amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko. Basi wana wa manabii, waliokuwako Yeriko, wakamkaribia Elisha, wakamwambia, Je! Unajua ya kuwa Bwana atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako? Akajibu, Naam, najua, nyamazeni. Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea mbele wote wawili. Basi watu hamsini wa wale wana wa manabii wakaenda wakasimama, kuwakabili kwa mbali; na hao wawili wakasimama karibu na Yordani.

Kushindwa ni nguvu ya kukunyamazisha usiwepo na usisikike tena.
Ukishindwa na yaliyopita utaendelea kuwa mtumwa wa yaliyopita.
Kuna tabia iliyopo ndani yako hiyo inasababishwa na jitu lililopo ndani yako.

Ahithofeli alikuwa na tabia yake kwamba kila kinachosemwa nay eye, watu wote hupokea na kutendea kazi.
II Sam 16:23
Na shauri lake Ahithofeli, alilokuwa akilitoa siku zile, lilikuwa kama mtu aulizapo kwa neno la Mungu; ndivyo yalivyokuwa mashauri yote ya Ahithofeli, kwa Daudi, na kwa Absalomu.

Siku ile aliposema na ushauri wake haukufutwa alizira na alijiua.
II Sam 17:23
Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye.

(i)Angusha madhabahu ya kushindwa iliyoko kwenye familia yenu.
Baaada ya wokovu madhabahu ya familia lazima iangushwe.
Mwanzo 12:1-2
Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

Kila familia inayo madhabahu inayowaunganisha na kuamua hatima watu wa hiyo familia.
Mwanzo 24:59-60
Ndipo wakampeleka Rebeka ndugu yao, na yaya wake, na mtumishi wa Ibrahimu, na watu wake. Wakambarikia Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.

Ezek 16:2-5
Mwanadamu, uujulishe Yerusalemu machukizo yake, useme, Bwana MUNGU auambia Yerusalemu hivi; Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti. Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa. Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa.

Madhabahu ya familia ndiyo inayoamua hatima ya watu wa hiyo familia wawe wa namna gani.
Wawe na sifa gani huko nje.
Wawe na kiwango gani cha mafanikio.
Wawe ni washauri, wagonvi au waongo nk.

Ukiwafanyia watu ushauri utagundua madhabahu za familia zao bado zimesimama hazijaangushwa chini.

Endapo utamwita mtu umkemee kwa uovu wake,kesho utaona familia nzima inakuchukia.

Bosi anakukemea kwa kosa la kweli lakini bosi huyo atachukiwa na familia nzima.
“mbaya zaidi ni pale mnapopishana na mkristo mwenzako kanisani,na tatizo hilo unalipeleka kuwa shida ya ukoo mzima.

Lazima uangalie ni rafiki wa namna ipi unaambatana nae.
Mith 13:20
Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
Mwanzo 30:1-12
Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi. Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba? Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye. Basi akampa Bilha mjakazi wake kuwa mkewe. Yakobo akaingia kwake. Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana. Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali. Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe. Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana. Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi. Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili.
Hii familia ilifanya hila wakati Yakobo anataka kuoa hivyo hii hila iliendelea hadi kwa watoto wao pia.

By Ernest Mbuya
MUNGU akubariki sana na itaendelea

Comments