JAMBO LINALOLAZIMISHWA KUWEPO KWENYE MAISHA YA MTU BILA RIDHAA YA MHUSIKA(sehemu ya Mwisho)

na Mwl Ernet Mbuya
                                                                                            Madhabahu ya Shekemu ilikuwa ni kutokutahiriwa.

Mwanzo 34:13 -17
Madhabahu ya wana wa Yakobo ilikuwa lazima watahiriwe.
Wana wa Yakobo wakawajibu Shekemu na Hamori babaye, kwa hila, maana amemharibu Dina, umbu lao, wakawaambia, Hatuwezi kufanya neno hili, tumpe umbu letu mtu asiyetahiriwa; ingekuwa aibu kwetu. Lakini kwa sharti hii tu tutapatana nanyi; mkiwa kama sisi,
akitahiriwa kila mwanamume wenu, ndipo tutawapa ninyi binti yetu, na sisi tutatwaa binti zenu tutakaa pamoja nanyi, nasi tutakuwa watu wamoja. Lakini kama hamtusikii na kutahiriwa, basi tutamtwaa umbu letu, nasi tutakwenda zetu.

Mwanzo 34:24-31
Wana wa shekemu wanajikuta wanaingia katika mauti kwa kuwa moja aliingia katika madhabahu ambayo haikumuhusu.
Wakawasikia Hamori na Shekemu mwanawe, wote watokao katika lango la mji wake. Wakatahiriwa kila mwanamume, wote watokao katika lango la mji wake. Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua waume wote.

Msiingize matatizo yenu binafsi na familia angusha chini madhabahu.
I Kor 6:1-6
Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa? Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake? Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini.

Madhabahu ya familia ndiyo inayoamua inabidi ivunjwe au iangushe chini.
Ezek 16:44
Tazama, kila mtu atumiaye mithali atatumia mithali hii kinyume chako, akisema, Kama mama ya mtu alivyo, ndivyo alivyo binti yake.

Malaika alimwambia Gidioni wewe ni shujaa lakini madhabahu ya baba yake ilikataa huo ushujaa.
Waamuzi 6:11-13
Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani. Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa. Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.

Mungu akamwambia iangushe kwanza madhabahu yabahali ambayo baba yako anaitumikia.
Waamuzi 6:25-26
Ikawa usiku uo huo Bwana akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; ukamjengee Bwana, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.

Hadi uangushe madhabahu ya baali ndio madhabahu ya mungu ianze kutenda kazi.
Kutoka 23:24
Usiisujudie miungu yao, wala kuitumikia; wala usitende mfano wa matendo yao; bali utaiangamiza kabisa, na nguzo zao utazivunja vipande vipande.

II Falme 10:26-30
Wakazitoa nguzo zilizokuwamo nyumbani mwa Baali, wakaziteketeza. Wakaibomoa nguzo ya Baali, na kuiangusha nyumba ya Baali, wakaifanya choo hata leo. Ndivyo Yehu alivyomharibu Baali katika Israeli. Walakini katika makosa yake Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli, Yehu hakutoka katika kuyafuata, yaani, ndama za dhahabu zilizokuwako katika Betheli na Dani. Bwana akamwambia Yehu, Kwa kuwa umetenda vema kwa kufanya vilivyo haki machoni pangu, kuitendea nyumba ya Ahabu sawasawa na yote yaliyomo moyoni mwangu, wana wako wa kizazi cha nne watakaa kitini mwa Israeli.

Kinachokutesa leo ni kile ambacho wazazi wako walikiacha wakati ule.
Maneno ya uovu yanayonenewa katika familia yako hayakupati moja kwa moja tu bali yanapitia na kuvuviwa nguvu na madhabahu ya familia yenu.
Ayub 5:21
Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.

Jeremia 18:18
Hapo ndipo waliposema, Njoni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njoni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yo yote.

Unapobaki ukiwa na mshikamano na madhabahu ya familia.
Hakuna neon baya watakalolisema dhidi yako likakosa kukupiga.
Kuna watu mateso wanayopitia leo ni matokeo ya madhabahu za familia walizotokea.
Biashara haisimami.
Familia yako haina msimamo.
Malengo yako hayafikiwi.

Ni kazi kuangusha madhabahu za familia.
Ulikozaliwa
Ulikoo au kuolewa.

Una kazi kubwa sana hata kama una imani kiasi gani, kazi ni kbwa.
Kuangusha hizo madhabahu na kusimamisha nyingine.
Jeremia 1:10
angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.

Laana idumuyo katika madhabahu ya familia ni laana iliyorithiwa na inaendelea kurithiwa katika vizazi.
Kushindwa ni tunda la kukataliwa.
Kukatizwa ni tunda la kukataliwa.
Maumivu ni tunda la kukataliwa.
Hofu ya kifo ni tunda la kukataliwa.

Ebr 2:14-15
Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.

Kukosa usalama ni tunda la kukataliwa.
Kujihurumia ni tunda la kukataliwa.
Upweke ni tunda la kukataliwa.
Uchungu ni tunda la kukataliwa.
Kujikataa mwenyewe ni tunda la kukataliwa.
Huzuni ni tunda la kukataliwa.
Kuvunjwa moyo ni tunda la kukataliwa.
Manunguniko ni tunda la kukataliwa.
Kuchanganyikiwa ni tunda la kukataliwa.

Hakuna mtu ambaye hapaswi kuangusha madhabahu wa familia.
Kwa sababu wanadamu wote wamerithi kukataliwa kutoka kwenye famila zao za kwanza na madhabahu ya kwanza ya familia.
Mwazo3:7
Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Mwanzo 3:15
nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Mwanzo 3:20-24
Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai. Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.

Hata kama umeokoka adui anafutilia hati za familia.
Kol 2:13-14
Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

Kwa mtu moja kukataliwa kulirithiwa katika dunia ya walio hai.
Warumi 5:12
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

Hata wale ambao hawajafanya uovu bado walipatwa na maovu.
Kwa sababu walilithi laan ya madhabahu ya familia.
Warumi 5:14
walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.
Warumi 5:16
Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki.
Kwa makosa ya familia moja familia zote zimerithi na kuingizwa kwenye madhabahu ya familia.
Warumi 5:19
Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.

Adamu hakuuza nchi tu bali aliuza uzao wake ambao ni sisi.
Warumi 7:14-20
Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu

Kushinda ni matokeo asiyotarajia mtu.
Paul anafafanua ya kuwa katika maisha yake ya kiro anampenda na kumtumikia Bwana.
Lakini matunda yangu ya shughuli za mwilini madhabahu ya familia niliyoridhi inaamua tofauti.
Warumi 7:23-25
lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.

Madhabauhu ya familia tuliyorithi kwa Adamu ndio iliyoharibu nchi.
Mwanzo 3:17
Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

Uzao wa Adamu uliipokea hiyo laana ya madhabahu.
Mwanzo 4:11-12
Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

Kumbukumbu 28:23-24
Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.

Ipo nguvu inayoharibu ulimwengu wako itokanayo na madhabahu ya familia.
Yoel 1:7
Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.

Madhabahu za ukoo au familia tulizotoka ndio chanzo cha ufukara na kushindwa kwa kila kitu.
Yoel 1:10-12
Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka. Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba yamepotea. Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka;

Famila nyingi zina nguvu za ishara inayoitwa nyeusi au madhabahu nyeusi.
(1)katika ukoo au wewe binafsi unaweza kuona tukio Fulani kiroho au kimwili.
Hilo tukio linaweza kuwa kushindwa katika kizazi chenu chote .
(2)Unaweza kuona mti unaanguka au unaweza kuota kitu kinazama katika maji.
Unaweza kuota chakula chako kinagawanywa, au unaota unapokonywa kitu.
Yuko mtu ameota anapata ajali na baada ya muda katika famila mtu anapata ajali na anakufa.
Baada ya muda hata watoto wake naao wanakufa.
Ishara nyeusi unaweza kulala na mtu ukiamka unakuta amekufa.
Mtu anaweza kukufia mkononi.
Zipo taarifa ambazo ni mbaya umezisikia nawe hukuzitendea kazi hizo ni roho au madhabahu za familia na baada ya muda hujidhihirisha kwa kuwa asilia hivyo mara uonapo kitu katika ndoto fanya maamuzi sahihi ya kujua nini hilo jambo.
Inawezekana kuna matukio mengi umekutana nayo na ukaona ni kwaida tu kumbe ni hizo madhabahu zinafanya kazi.
AMENI.
MUNGU awabariki sana.
 By Mwl Ernest Mbuya

Comments