JE WAJUA MAANA YA JINA LA FARAO ?




Bwana Yesu asifiwe…

*Watu wengi hawafahamu maana halisi ya jina la Farao,na hata hawafahamu ni FARAO wangapi wanaotajwa katika Biblia takatifu,

Lakini leo nataka usiwe mmoja wa watu wasiojua maana ya jina la Farao,pia uweze kuwatofautisha pindi uwasomapo.

*Kwanza kabisa Jina la FARAO,sio jina kama majina mengine bali ni cheo kilichotumika Misri kumuelezea mtu Fulani kwamba ni MFALME,Hivyo basi kiusahihi kabisa ni jina la kimisri lililotolewa katika lugha ya Kiyahudi lenye maana ya MFALME.

Tunapoliona jina hili popote pale,maana yake ni ile ile ya MFALME.
Wafalme wa Misri hawapungui kumi na mbili au kumi na tatu,wale waliotajwa katika maandiko,ambao hao wote waliitwa kwa jina la FARAO,isipokuwa wale wane (Wakina-Herode)

Miongoni mwa cheo hiki,Wafalme wengine wawili walikuwa na majina yao tofauti na jina hili,Wafalme hao ni Necho and Hophra.
Bali wengine walibakia na cheo hicho cha Farao.Mtililiko ufuatao unatupa picha nzuri ya Farao kama walivyotajwa katika maandiko matakatifu;

01. FARAO ,
Tunasoma ,mwanzo 12:14-15,
“ Basi ikawa Abramu alipofika Misri, Wamisri wakamwona huyo mwanamke ya kwamba yeye ni mzuri sana.
Wakuu wa Farao wakamwona, nao wakamsifu kwa Farao; basi yule mwanamke akachukuliwa nyumbani mwa Farao.”
*Huu ulikuwa ni wakati wa Abrahamu B.C.1920

02. FARAO.(mwingine)
*Huyu alikuwa ni Farao ambaye akida wake alikuwa ni Potifa
Tena alikuwa ni mwalimu wake Yusufu kwa sababu Yusufu alikuwa chini yake kimadaraka,
Tunasoma Mwanzo 37 :39
“ Nao Wamidiani wakamwuza huko Misri, kwa Potifa, akida wa Farao, mkuu wa askari.”
Pia soma Mwanzo 39 :1,Matendo 7:10,13
*Ilikuwa ni kabla ya Kristo, B. C. 1728.
* Hata hivyo wengine husema kwamba FARAO huyu ni mtoto wa FARAO Yule wa katika Mwanzo 37:36

03. FARAO(mwingine) *Huyu ni Farao mwingine aliyeinuka juu ya Misri asiyemfahamu Yusufu Matendo 7 :18
“ hata mfalme mwingine akainuka juu ya Misri, asiyemfahamu Yusufu.”Pia Soma Kutoka 1 :8,Soma tena Waebrania 11 :23,

Hata hivyo,kuna FARAO mwingine aliyeinuka katika kipindi cha Musa alipokimbilia Midiani na ndio Farao ambaye alikufa kabla ya Musa kufikisha umri wa miaka themanini aliporudi kutoka Midiani kwenda Misri,Soma Kutoka 2:11-23,Kutoka 4:19,na Matendo 7:23

04. FARAO(mwingine)
*Huyu ni Farao ambapo aliwazuia Waisraeli wasitoke Misri.Soma Kutoka 5:1-14,Kutoka sura ya 31,2Wafalme17 :7,Nehemia 9:10,Zaburi 135:9
Rumi 9:17; Waebrania 11:27, alitawala B. C. 1491.(Kabla ya Kristo)

05. FARAO(mwingine)
*Huyu alikuwa ni Farao katika kipindi cha Daudi 1Wafalme 11:18-22; B. C. 1030.

06. FARAO(mwingine)
*Huyu alikuwa ni Farao ambaye ni baba mkwe wake Selemani, 1Wafalme 3:1; 7:8; 9:16,24, B. C. 1010.

PAMOJA NA FARAO HAO,WAPO WENGINE KAMA VILE;
07. SHISHAKI-B. C. 975, 1Wafalme 11:40; 1Wafalme 14:25; 2 Nyakati12:2

08. ZERAH,-Alikuwa ni mfalme wa Misri na pia alikuwa ni mfalme a Ethiopia katika kipindi cha Asa , B. C. 930;

09. SO,
-Huyu alikuwa akiitwa SO hivyo hivyo na ndilo jina lake.Ilikuwa Katika kipindi cha Ahazi, B. C. 730,Soma 2 Wafalme 17:4.

10.TIRHAKA( Tirhakah, )
*Huyu alikuwa ni mfalme wa Ethiopia na Misri(KUSHI)Katika muda wa Hezekia B. C. 720, Soma2 Wafalme 19:9; Isaya 37:9.

11.FARAO-NEKO
*Alikua ni mfalme wa Misri katika kipindi cha Yosia B. C. 612, Soma 2 Wfalme23:29-30; 2 Nyakati35:20-24, etc.

MWISHO .
UBARIKIWE.   imeandaliwa na mtumishi wa MUNGU. Gasper madumla

mtumishi Gasper Madumla

Comments