JE WAJUA NINI KUHUSUMFALME HERODE ?




Bwana Yesu asifiwe…

Leo nimeonelea tujifunze juu ya habari ya Herode mfalme.
Mara nyingi watu hawamuelewi vizuri Herode.

Wengi tumekuwa tunapomsoma Herode katika Biblia tunashindwa kumtofautisha Herode kwamba ni Herode gani anayezungumziwa wengi tunajua kwamba Herode ni Herode tu.
Kumbe kuna mengi ya kujifunza.

Karibu…
*Kwanza kabisa napenda ufahamu kuwa jina la Herode ni jina la Wafalme linalowakilisha Wafalme wanne waliotawala kati ya sehemu ndogo
au sehemu yote katika ya Yuda (Judea) chini ya utawala wa WARUMI na wanaelezewa vizuri katika agano jipya.
Sasa tuanze kumuangalia HERODE wa kwanza;

01 HERODE MKUU(. HEROD THE GREAT,)
*Huyu alikuwa ni mtoto wa Antipater ambaye alikuwa na kibali kikubwa kwa Juliasi Sizelia (Julius Caesar.)
Katika umri wake wa miaka kumi na mitano,HERODE alikabidhiwa kikatiba na baba yake aitawale GALILAYA chini ya Hyrcanus II,

ambaye alikuwa ni kiongozi wa Taifa la WAYAUDI.
Madaraka ya Hyrcanus yalikuwa yakipingwa na kaka yake Aristobulus.
*Habari za Herode mkuu zimeelezwa pia katika Mathayo 2:1-23,na Luka ,1:5.

Hata hivyo Herode alihofia utawala huo na kuamua kwenda RUMI na huko ndiko akajulikana kama mfalme wa YUDA , ( B. C. 37. )

*Na ikumbukwe kuwa huyu Herode ndie Yule aliyeamuru mauaji ya watoto wote wenye umri wa miaka miwili,ili aweze kumuangamiza Yesu huko Betrehemu ya Uyahudi.

*Mara tu baada ya kifo cha Herode ,Nusu ya ufalme wake ,ikijumuisha Yuda, Ideumaea, na Samalia,ulitwaliwa na mtoto wake Archelaus,mbapo ufalme wake uliobakia uligawanywa katikati ya watoto wake wengine wawili Herod Antipas na Philip.

2. HEROD PHILIP.
*Huyu alikuwa ni mtoto wa Herode mkuu,naye hujulikana kama HERODE lakini ili kuwatofautisha yeye na baba yake ni lazima umuite baba yake kuwa ni Herode mkuu,na huyu umuite Herode Philip

3. HEROD ANTIPAS,
Huyu Herode wa tatu alikuwa pia ni mtoto wa Herode mkuu,ambaye alitoka kwa mwanamke Malthace ,
Msamaria.Soma Luka 3:1,

*Antipas alipata elimu yake huko Rumi.Baada ya kufa baba yake (Herode mkuu) aliteuliwa na kuiangalia Galilaya na Perea ,sehemu ya kusini mwa nchi na ni mashariki mwa Yordani.
*Herode Antipas ndiye Yule Herode aliyepelekea kifo cha Yohana mbatizaji kwa kukatwa kichwa chake akiwa gerezani. Soma Mathayo 14 :1-12,
Pia Herode Antipas anaonekana kuwa ni mfuasi wa Masadukayo Mathayo 16:6 .

4.(i) HERODE AGRIPPA MKUU.(Au Agrippa wa kwanza)
Huyu alikuwa ni mjukuu wa Herode mkuu,(Herod the great)
Waweza kusoma habari zake pia katika Matendo 12: :1-25,
Na ndie aliyemua Yakobo ndugu yake YOHANA

Tunasoma Matendo 12 :1-21
“ Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.
Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga.”

*Agrippa mkuu alikuwa ni mtu aliyeshika YUDA na Samaria ambazo babu yake alikuwa ndio muanzilishi A.D.43

(ii). HERODE AGRIPPA MDOGO (au Herode Agrippa wa pili)
*Huyu ni mtoto wa Agrippa wa kwanza,(Herode Arippa mkuu)Naye alipata elimu yake huko Rumi chini ya usimamizi wa Claudio ( Claudius.)

*Pia habari zake zinaonekana katika Matendo 25 :1-26,Tena katika mstari wa 13 Linalomeka hivi hilo andiko ;

“ Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita,AGRIPA MFALME na Bernike wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo.”

Katika kifo cha baba yake ambapo alikuwa na umri wa miaka kumi na saba (17).
Alikufa akiwa na umri wa miaka sabini katika mwaka wa tatu wa Trajan (Trajan's reign,)

MWISHO.
UBARIKIWE. imeandaliwa na mtumishi Gasper Madumla

Mtumishi Gasper Madumla

Comments