KWELI SITA(6) ZA MIZIMU

Somo hili ni mwendelezo wa somo liitwalo KUFUNGULIWA KUTOKA ROHO ZA MIZIMU na hii ni sehemu ya pili iitwayo


           KWELI SITA(6) ZA MIZIMU

1;
Mizimu ni malaika walioasi mbinguni

2;Mizimu  ni  wapelelezi wa shetani 

3;Mizimu inauwezo wa kutoa nyaraka au taarifa ya mtu 

4;Mizimu  inafanya kazi kupitia wafu.
 waebrania 9;27 ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu''
5;Mizimu  inafanya  kazi kupitia waganga  wa kienyeji 

6;Mizimu inauwezo wa kutunza taarifa za mtu, ukoo au kabila

*Kuhusu wafu mtu akifa kuna sehemu mbili tu za kwenda.

a.Paradiso –ni mahali  pa mangojeo kwa uzima  wa milele.

b.Kuzimu –ni mahali pa mangojeo pa jehanamu
Mtu akifa anatengana na wewe ukiomba mtakatifu yeyote ni kuomba mizimu, ibada za wafu ni kuabudu mizimu Luka 16:22-26{
Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.}

 Ndugu zangu hakuna mawasiliano baina ya mfu na walio hai hivyo mizimu hubeba sura ya mtu aliyekufa na sauti yake na kumtokea mtu kwa ndoto au maono au hata kumtokea moja kwa moja,
Jambo jingine la kutambua ni kwamba shetani huwafanya watu waamnini kwamba hata wao wakifa watakuja kuwatokea watu na hata wakiendelea na uovu hata wakifa wapo watu watawaombea na MUNGU atawatoa kuzimu na kuwapeleka mbinguni kitu ambacho hakipo na sio kweli. Hebu tafakari viongozi wengi wakuu wa serikali kuna siku maalumu umetengwa kwa mwaka kwamba ni siku yao na kila siku hiyo ikifika tunaenda kwenye makaburi yao na kuwaombea MUNGU awasamehe. Je wale wavuvi wanaokufa baharini na hakuna hata mmoja anayejua makaburi yao yalipo na hakuna hata mmoja anayewaombea je MUNGU siku hizi anaupendeleo? Yaani ukiwa raisi wa nchi lazima uingie pema peponi maana utakua na waombeaji wengi tena watakua na juhudi kukuombea kila mwaka siku yako ikifika jambo ambalo sio la kweli, MUNGU atusaidie na tutambue kuwa muda wa kumpa YESU maisha ni sasa wala sio baada ya kufa maana tukifa tu ni kuzimu au mbinguni na sio vinginevyo. Katika Isaya 8:19 Biblia inasema

''Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?''
Ndugu zangu pazia limekwisha kupasuka hivyo tunanaingia patakatifu moja kwa moja bila kuombewa na mtakatifu wa zamani maana BWANA YESU aliondosha kile kiambaza kilichokuwapo baina ya MUNGU na wanadamu ndiyo maana kupitia yeye(YESU) tnapata uzima bure kwa njia ya imani matendo 4:12 ''
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo''.
 ila uzima huo tunaupata tungali hai sio tukifa

MAGOJWA YANAYOSABABISHWA NA MIZIMU

Kuna magonjwa ya ukoo ya kuhama kutoka kizazi hadi kizazi na magonjwa haya husababisha na mizimu.
Pia kuna baadhi ya magonjwa yanasababishwa na mizimu mfano Pumu, kuumwa miguu, miguu kufa ganzi, vivimbe mbalimbali katika mwili, kutokukua kiroho, matumizi mabaya ya pesa  na kutokupona magonjwa. Ndugu kimbilia maombezi na utakuwa huru mbali na uonevu huu wa shetani.

Mizimu pia hutumia manabii wa uongo kwa udanganyifu au upotoshaji, mizimu pia hutumiwa na wachawi na wapandisha pepo, Mizimu pia hutumiwa na dini za uongo.

MUNGU awabariki sana

Comments