LINDA SANA NAFASI YAKO


  1. Mwl SOSPETER SIMON S. NDABAGOYE
    New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania


    Wala msimpe ibilisi nafasi (Efeso 4:27)
    Kanisa la leo, haliogopi dhambi....linachukulia dhambi kama kitu cha kawaida! Wokovu hauna maana. Watu hawajishushi mbele za Mungu, watu hawanyenyekei, watu ni wakaidi; kanisa limeasi, kanisa limekuwa sehemu ya kufanyia maasi, ni biashara, limekua sehemu ya kufichia maovu, ibada zimekuwa fasheni; umutishi umekwisha, binadamu wanajipenda kuliko Mungu, mtu yuko tayari kuona huduma inaangamia ili mradi yeye apate anacho kitaka. KANISA LINATAKIWA KUTUBU KWA MUNGU “Kanisa limempa Ibilisi nafasi”
    Leo, mtu yuko tayari kumwacha Yesu kwaajili ya mali, utajiri wa kitambo tu, unakutenga na Mungu....ni mara ngapi tumeshuhudia vijana wetu wakiamua kuolewa au hata kuoa (na)wapagani kwa kufuata mafanikio ya muda tu, ndoa iankutenga na Mungu? Mtu anamwabudu shetani kwa kuyafuata mafanikio ya muda mfupi tu. Ebu ngoja ni kwambie mpendwa, shetani hawezi kukutoa hapo ulipo na kukuweka sehem nzuri hata siku moja, yeye anakutaka akuteke na kukupeleka kuzimu
    Hivi majuzi zimetoka taarifa kwenye vyombo vya habari juu ya fomu ya usajili kwa wale ambao wangependa kujiunga na uabudu wa shetani chini ya mtandao wao ujulikanao kama freemason (wajenzi huru). Watu walikuwa wangombania...kila mtu alitamani angekuwa wa kwanza kupata ile fomu eti, kwa kuwa kila anaejiunga na mtandao huo, maisha yake huwa mazuri sana. Anafanikiwa kimaisha, anaachana na uamasikini.
    Hata, hivyo nchi za magharibi ziliadhimia juu ya kupitishwa kwa sheria ya ndoa ya jinsia moja kama mkakati mmoja wapo wa kutekekeleza haki za binadamu ulimwenguni, na kutangaza kusitisha misaada kwa nchi zitakazokwamisha sheria hii. Kitendo ambacho ni kinyume na maagizo ya Mungu (Mambo ya walawi 19:22, 20: 13) (Warumi 1:25, 32)
    Ndg zangu, Biblia katika 1Yohana 2:15 inaeleza; “ msiipende dunia wala mambo yaliyomo...mtu akiipenda dunia, kumpenda Mungu hakumo ndani yake. Tena anasema, kilichomo duniani ni tamaa ya mwili, tamaa ya macho, kiburi cha uzima ambavyo ni matokeo ya kuupenda ulimwengu ambao leo upo ila kesho haupo”
    Biblia inatutahadharisha juu ya nyakati za mwisho na ishara zake (1Yohana 2:18). Watoto ni wakati wa mwisho, na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo ni wengi wamekwisha kuwapo. Kwasababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.
    Je, wewe unalichuuliaje hili?
    Nimetumwa nikwambie leo, juu ya kuzitafakari njia zako. Ufanye marekebisho juu ya mienendo yako ya kimaisha, uyaangalie mahusiano yako na Mungu, ujitafakari, ujisahihishe na kuendelea mbele. Kumbuka neno linasema” adhaniaye anaiokoa nafsi yake, basi huyo anaipoteza” na ni kheri kuwa mtumwa wa Kristo kuliko kuwa mtumwa wa dhambi na mwasi siku zote za maisha yako!

    Mwl SOSPETER SIMON S. NDABAGOYE
    New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania

Comments