MAADUI WA NDOA






           

1: Kusikiliza wa wengine/wa nje ya ndoa.
Ndoa ni watu wawili tu walio mwili mmoja.

2:  Kutokua muwazi katika ndoa.

3:Kutokua na uaminifu katika ndoa.

4: Wivu wa kupindukia.
Wivu unaomfanya mtu kuwa mtumwa.

5:Kuolewa na mapepo/ majini mahaba.
Katika vita   yeyote  wataalamu wa vita wanasema kuwa vita ya ndani(civil war)  ni mbaya sana kuliko vita ya nje{External war}.  Na katika ndoa pia vita ya ndani ya vita ya wanandoa wenyewe ni mbaya sana na inaweza kupelekea mmoja wa wanandoa kufikia hatua ya kutembea na talaka mfukoni yaani ‘’bado neno moja tu nampa talaka’’. Katika BIBLIA kitabu cha Mathayo 19:7-9.''
Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?   Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.  Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
Talaka ilianzishwa baada ya dhambi ya ugumu wa moyo. Lakini MUNGU tangu mwanzo hakupendezwa na talaka maana talaka haiko katika mpango wa MUNGU kwa mwanadamu ila MUNGU anataka kila Adamu aishi na Eva wake hadi kifo. MUNGU awabariki sana
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula

ndoa ya kimungu ni mke mmoja kwa mme mmoja



Comments

Anonymous said…
inakuwaje sasa! mbona siku hizi watu wanaharalisha kuachana hata kanisani?
Peter Mabula said…
wanaofanya hivyo hawamjui tu MUNGU wao maana MUNGU hapendi wanandoa kuachana .