MAOMBI NI CHANZO CHA MAISHA YA USHINDI

Mwl Nickson Mabena akifundisha neno la MUNGU na hapo ni Mruvango, wilayani Siha mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha!!

Kwa kuwa tumeamua kumfuata Yesu (KUWA WAKRISTO), hatuwezi kukwepa kuomba...
"Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa." LUKA 18:1
"Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani." KoLOSAI 4:2
KUOMBA ni maisha ya Mkristo, Kwani YESU mwenyewe aliomba; "Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, ketini hapa, hata niende kule nikaombe." Mathayo 26:36
Pia alitaka aombe na wanafunzi wake; "Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami." Math 26:38
MITUME waliomba; "Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao". MDO 13:3
"na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile neno" MDO 6:4
pia ona MDO 14:23

YESU ametuagiza tuwe waombaji;
"Ombeni, nanyi mtapewa;tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea;naye atafutaye huona; naye abishaye hufunguliwa." Math 7:7-8

MAOMBI ni silaha;
"kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote" Efeso 6:18

KUMBUKA; kadri unavyozidi kuomba ndivyo nguvu za Mungu zinavyozidi kuongezeka ndani yako. MAOMBI KIDOGO na NGUVU KIDOGO.
YESU alitaka wanafunzi wake waombe pamoja na Yeye angalau saa moja tu!
"Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha nami hata saa moja?." Math 26:40-43
( ALIWASISITIZA HIVYO MARA TATU)

Kama YESU na MITUME waliomba, sisi ni wakina nani hata tusiombe!?
Kama Yesu alitaka wanafunzi wake waombe angalau saa moja (saa moja kiwango cha chini) Je sisi tunaomba angalau saa ngapi!!?
<<<<<< BILA MAOMBI NDUGU YANGU HAKUNA MAISHA YA USHINDI>>>>>
MUNGU awabariki sana
By Mwl Nickson Mabena

Comments