MAOMBI NI SILAHA YA KIPEKEE YENYE UTIISHO.

Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Napenda niitangazie Uma kwamba, MAOMBI KATIKA KRISTO YESU ni silaha yenye utiisho hata kuangusha ng’ome katika ulimwengu wa roho.
Tunasoma Nehemia 2:4 ;
“Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni.”

Ukisoma kuanzia sura ya kwanza ya kitabu cha Nehemia,utaona Nehemia akifanya maombi ya nguvu mara baada ya kupewa ujumbe kutoka kwa Hanani mmoja wa ndugu yake pamoja na baadhi ya ndugu zake waliompasha habari juu ya dhiki nyingi ya ndugu zake waliopo uhamishoni. (Nehemia 1:3-4)
*Nehemia alikuwa ni mnyweshaji wa mfalme.Hivyo ilikuwa ni vigumu sana kwake kusikilizwa na mfalme kwa mahitaji au matakwa yake.
Lakini baada ya maombi hayo aliyoyafanya kwa ajili ya KUWAKOMBOA ndugu zake waliokuwa katika hali ya dhiki nyingi.

*Tazama baada ya maombi ya Nehemia,yalivyo kuwa na UTIISHO hata kupelekea kupata kibali mbele za mfame,kitu ambacho sio cha kawaida.
Katika sura ya pili ya kitabu cha Nehemia (Nehemia 2 :1) tunaona divai ikiwa imewekwa mbele ya mfalme.

Kwa sababu kazi ya Nehemia ilikuwa ni ya unyweshaji,naye akampelekea ile divai kama ilivyokuwa desturi yake,
Lakini Kumbuka siku hiyo Nehemia hakuonekana kama Nehemia wa siku zote,
Bali alikuwa ni watofauti mno, alikuwa na mng’aro wa utukufu wa kipekee kwa sababu ya MAOMBI aliyokuwa ameyafanya,Hivyo MAOMBI yakawa ni silaha ya kumsukuma mfalme kumpa KIBALI tena hata akamwambia Nehemia;
“ Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. (Nehemia 2:4)”

*Ilikuwa sio rahisi mfalme aseme maneno haya. Kilichomsukuma Mfalme kutamka maneno kama haya ni ile nguvu ya maombi ya Nehemia,
Tazama Nehemia alikuwa akiomba kwa ajili ya ndugu yake hali yeye ni kama mtumwa tu.
Maana alikuwa hana uwezo wa kutoka kwa mfalme kwa kutumia akili zake.
Lakini Mungu akafanya njia pasipo njia.

Ooh Haleluya..
Nehemia aliomba pasipo shaka ya kujiuliza uliza kwamba atatokaje katika hali ya utumwa ule ili aende kuwaombolezea ndugu yake huko Yerusalemu.
Lakini jambo moja alilolijua Nehemia ni KUOMBA TU.
Habari ya kupata njia ya kutoka mahali pale ilikuwa ni juu ya Mungu mwenyewe,Bali yeye ni kuomba tu.

Sikia;
Divai iliyoandaliwa kwa ajili ya Mfalme haikuwa mbali naye kiasi kwamba amuhitaji Nehemia kwenda kumchukulia,.
Bali divai ilikuwa mbele tu kidogo,nasema mbele kidogo tu,Mungu akamtaharakisha amuite Nehemia ili amletee ile divai ambayo hata yeye mwenye ang’eweza kuichukua.

*Lakini Maombi ya Nehemia yakamtaharakisha mfalme amuite Nehemia,na alipompelekea tu,tunaona akanza kutamka ;
“ Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni.” Nehemia 1:4
• Yeyote atakaye ishi ndani ya Kristo,kisha akaomba kwa KUOMBOLEA kwa kufunga na kuomba katika roho,MAOMBI YA MTU HUYO NI SILAHA YA KIPEKEE YENYE UTIISHO.

Comments