MATOKEO YA DHAMBI


Mwl Nickson Mabena akifundisha neno la MUNGU na hapo ni Mruvango, wilayani Siha mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha.


1.Hututenga na Mungu ( Mwanzo 3:23,24 ; Isaya 59:2)
"Lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na DHAMBI zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia". Isaya 59;2

2. Wenye dhambi hukataliwa mbinguni.
(1Kor 6:9-11, ; Gal 5:19-21; Efeso 5:3-7, ufunuo 21:27)

"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji,........" 1Kor 6:9-11

3. Dhambi huleta hasira ya Mungu
(Kumb 25:16; Mith 6:16-19, 1Falme 16:2)

"Kwa kuwa wote wayatendao yasio haki, ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako". Kumb 25:16

dhambi ni mbaya sana
4. Dhambi huleta laaana ya Mungu

a) Ardhi inalaaniwa kwa sababu ya dhambi.
"Akamwambia Adamu, kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nlikuagiza,nikasema, usiyale; Ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako......" Mwanzo 3:17-18

b) Kazi ngumu kwa jasho kwa sababu ya dhambi.
"Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi..." Mwanzo 3:16,17,19
"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu" Ayubu 14:1

c) Uchungu wakati wa kujifungua kwa sababu ya dhambi.
"Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.

Tukipata muda mwingine, kadri Mungu atakavyotujalia, tutaendelea na somo. Ubarikiwe!
By mwl Nickson Mabena




Comments