Mwinjilist wa Kimataifa Reinhard Bonnke kufanya Mkutano mkubwa wa injili jijini Dar es Salaam

Muinjilist wa kimataifa Reinhard Bonnke anatarajia kufanya mkutano mkubwa wa injili jijini Dar es salaam, Tanzania kuanzia tarehe 21August  hadi tarehe 25August 2013 mkutano unatarajiwa kufanyikia katika viwanja vya nje ya uwanja wa taifa wa zamani / uwanja wa uhuru.

mpaka sasa maandalizi mbalimbali  kwa ajili ya mkutano huo mkubwa ,yameshaanza ikiwa ni pamoja na  Maombi, kikundi cha kusifu na kuabudu, watu wa matangazo, wasimamizi wa wahudumu na idara mbalimbali. 
Muandaaji mkuu wa mikutano hiyo ukanda wa africa alisha wasili hapa tangu wiki iliyopita ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa,na  kumekuwa na vikao vya mara kwa mara vya wachungaji wenyeji wa mkutano huo wa makanisa ya hapa Dar es salaam. 
upande wa matangazo kutakuwa na cinema za mikanda ya mwijilisti huyo itakayoonyweshwa kwenye mitaa mbalimbali ya hapa Dar.

Bonnke anakuja Tanzania baada ya kupata mwaliko na askofu mkuu wa TAG ampaye alikutana naye mapema mwaka huu huko marekani,

kwa mara ya mwisho mkutano wa mtumishi huyu ulifanyika mwaka 1998 ambapo maelfu ya watu waliokoka na kufunguliwa. vipeperushi ambavyo vimeshatoka vinamtaka kila muumini aalike watu wasiopungua watu 10 ili waje kwenye huo mkutano.

Awali mkutano huo ulikuwa ufanyike katika viwanja vya jangwani lakini kutokana na ujenzi wa barabara unaoendelea kwa sasa ilionekana itakuwa usumbufu kwa watakaokuwa wakitumia barabara ya morogoro.

kama unataka kuwa mhudumu kwenye mkutano huo onana na mchungaji wa kanisa lako ili upewe maelekezo. ikumbukwe mwezi uliopita Bonnke alikuwa nchi ya Kenya na alifanya mkutano mkubwa sana katika viwanja vya uhuru na sasa ni zamu ya Tanzania na utafanyika viwanja vya nje ya uwanja wa uhuru. 

story kwa hisani ya Martin Malecela/http://martmalecela.blogspot.com

Comments